Zaburi 104
Kumsifu Muumba
1104:1 Za 103:22; Ay 40:10Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana,
umejivika utukufu na enzi.
2104:2 Yer 43:12; 51:15; 1Tim 6:16; Ay 9:8; 37:18; Isa 44:24; 49:18, 22; 42:5; 40:22; Zek 12:1; Za 18:12; 19:4Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi,
amezitandaza mbingu kama hema
3104:3 Amo 9:6; Za 18:10; 24:2; Kum 33:26; Isa 19:1; Nah 1:3; 2Fal 12:11na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji.
Huyafanya mawingu kuwa gari lake,
na hupanda kwenye mbawa za upepo.
4104:4 Za 148:8; Mwa 3:24; 2Fal 2:11; Ebr 1:7Huzifanya pepo kuwa wajumbe104:4 Au: malaika. wake,
miali ya moto watumishi wake.
5104:5 Kut 31:17; Ay 26:7; Za 24:1, 2; 121:2; 102:25; 1Sam 2:8Ameiweka dunia kwenye misingi yake,
haiwezi kamwe kuondoshwa.
6104:6 Mwa 7:19; 1:2; 2Pet 3:6Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi,
maji yalisimama juu ya milima.
7104:7 Za 18:15; 29:3; Kut 9:23Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia,
kwa sauti ya radi yako yakatoroka,
8104:8 Za 33:7; Ay 38:10yakapanda milima, yakateremka mabondeni,
hadi mahali pale ulipoyakusudia.
9104:9 Yer 5:22; Za 16:6; 33:7; Ay 26:10; Mwa 1:9; 9:11Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka,
kamwe hayataifunika dunia tena.
10104:10 Za 107:33; Isa 41:16Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni,
hutiririka kati ya milima.
11104:11 Za 104:13; Mwa 16:12; Isa 32:14; Yer 14:6Huwapa maji wanyama wote wa kondeni,
punda-mwitu huzima kiu yao.
12104:12 Za 104:17; Mt 8:20; 13:32Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji,
huimba katikati ya matawi.
13104:13 Za 135:7; 147:8; Yer 10:13Huinyeshea milima kutoka orofa zake,
dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.
14104:14 Ay 38:27; 28:5; Mwa 1:30; Za 147:8; 136:25Huyafanya majani ya mifugo yaote,
na mimea kwa watu kulima,
wajipatie chakula kutoka ardhini:
15104:15 Mwa 14:18; Amu 9:13; Za 23:5; 92:10; Lk 7:46; Kum 8:3; Mit 31:6, 7; Yer 12:12; Mk 14:23; Mhu 10:19; Yn 2:9, 10divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu,
mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake,
na mkate wa kutia mwili nguvu.
16104:16 Mwa 1:11; Za 29:5; 72:16; Hes 24:6Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri,
mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
17104:17 Za 104:12Humo ndege hufanya viota vyao,
korongo ana nyumba yake kwenye msunobari.
18104:18 Mit 30:26; Kum 14:5Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu,
majabali ni kimbilio la pelele.
19104:19 Mwa 1:14; Za 19:6; Ay 38:12Mwezi hugawanya majira,
na jua hutambua wakati wake wa kutua.
20104:20 Isa 45:7; Amo 5:8; Za 74:16; 50:10Unaleta giza, kunakuwa usiku,
wanyama wote wa mwituni huzurura.
21104:21 Amo 3:4; Za 145:15; Mt 6:26; Yoe 1:20Simba hunguruma kwa mawindo yao,
na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.
22104:22 Za 37:8Jua huchomoza, nao huondoka,
hurudi na kulala katika mapango yao.
23104:23 Mwa 3:19; Amu 19:16Kisha mwanadamu huenda kazini mwake,
katika kazi yake mpaka jioni.
24104:24 Mwa 1:31; 1:20-22; Za 40:5; 24:1; 50:10, 11Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi!
Kwa hekima ulizifanya zote,
dunia imejaa viumbe vyako.
25104:25 Za 69:34; Eze 47:10Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele,
imejaa viumbe visivyo na idadi,
vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.
26104:26 Za 107:23; Eze 27:9; Yon 1:3; Ay 41:1; 40:20; Mwa 1:21Huko meli huenda na kurudi,
pia Lewiathani,104:26 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. uliyemuumba acheze ndani yake.
27104:27 Ay 36:31; Za 147:9; 145:15; Rum 11:36Hawa wote wanakutazamia wewe,
uwape chakula chao kwa wakati wake.
28104:28 Isa 58:11; Za 103:5; 145:16Wakati unapowapa,
wanakikusanya,
unapofumbua mkono wako,
wao wanashibishwa mema.
29104:29 Kum 31:17; Ay 7:21; Mhu 12:7Unapoficha uso wako,
wanapata hofu,
unapoondoa pumzi yao,
wanakufa na kurudi mavumbini.
30104:30 Mwa 1:2; Isa 32:15Unapopeleka Roho wako,
wanaumbwa,
nawe huufanya upya uso wa dunia.
31104:31 Kut 40:35; Rum 11:36; Mwa 1:4; Za 8:1Utukufu wa Bwana na udumu milele,
Bwana na azifurahie kazi zake:
32104:32 Kut 19:18; Hab 3:10; Za 97:4; 144:5yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka,
aigusaye milima, nayo ikatoa moshi.
33104:33 Kut 15:1; Za 108:1Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote;
nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.
34104:34 Za 2:11; 9:2; 32:11Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,
ninapofurahi katika Bwana.
35104:35 Ay 7:10; Za 28:6; 37:38; 105:45; 106:48Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia
na waovu wasiwepo tena.
Ee nafsi yangu, msifu Bwana.
Msifuni Bwana.104:35 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.