Zaburi 102 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 102:1-28

Zaburi 102

Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu

Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Bwana.

1102:1 Za 4:1; Kut 2:23Ee Bwana, usikie maombi yangu,

kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.

2102:2 Za 22:24; 31:2; 88:2; 2Fal 19:16Usinifiche uso wako

ninapokuwa katika shida.

Unitegee sikio lako,

ninapoita, unijibu kwa upesi.

3Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi,

mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.

4102:4 Za 37:2; 90:5-6; 1Sam 1:7; Ezr 10:6; Ay 33:26Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani,

ninasahau kula chakula changu.

5102:5 Za 6:6Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu,

nimebakia ngozi na mifupa.

6102:6 Isa 34:11; Sef 2:14; Kum 14:15-17; Ay 30:29Nimekuwa kama bundi wa jangwani,

kama bundi kwenye magofu.

7102:7 Za 77:4; 38:11Nilalapo sipati usingizi,

nimekuwa kama ndege mpweke

kwenye paa la nyumba.

8102:8 Za 31:11; 42:10; Mdo 23:12Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki,

wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana.

9102:9 Isa 44:20; Za 6:6; 42:3; 80:5Ninakula majivu kama chakula changu

na nimechanganya kinywaji changu na machozi

10102:10 Za 7:11; 38:3; 30:7kwa sababu ya ghadhabu yako kuu,

kwa maana umeniinua na kunitupa kando.

11102:11 1Nya 29:15; Ay 14:2; 8:12; Za 39:6; Yak 1:10Siku zangu ni kama kivuli cha jioni,

ninanyauka kama jani.

12102:12 Kut 15:18; 3:15; Isa 55:13; 63:12; 40:2; Za 135:13Lakini wewe, Ee Bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele,

sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote.

13102:13 Za 119:126; 44:26; 77:7; Kum 32:36; 1Fal 3:26; Isa 54:8; 60:10; 40:2; Zek 10:6; Kut 13:10; Dan 8:19; Mdo 1:7Utainuka na kuihurumia Sayuni,

kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema;

wakati uliokubalika umewadia.

14102:14 Dan 9:2Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako,

vumbi lake lenyewe hulionea huruma.

15102:15 1Fal 8:43; Isa 2:2; Za 67:7; 76:12; 138:4; 148:11Mataifa wataogopa jina la Bwana,

wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako.

16102:16 Za 51:18; 8:1; Isa 60:1, 2Kwa maana Bwana ataijenga tena Sayuni

na kutokea katika utukufu wake.

17102:17 Neh 2:8; 1Fal 8:29; Za 4:1; 6:9Ataitikia maombi ya mtu mkiwa,

wala hatadharau hoja yao.

18102:18 Rum 4:24; 15:4; Za 22:31; 1Kor 10:1; Isa 43:21Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho,

ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana:

19102:19 Kum 26:15; Za 14:2; 53:2Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu,

kutoka mbinguni alitazama dunia,

20102:20 Za 68:6; Lk 4:19kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa

na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.”

21102:21 Za 22:22; 9:14Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni

na sifa zake katika Yerusalemu,

22102:22 Hos 1:11; Za 22:27; Isa 49:22, 23; Zek 8:20-23wakati mataifa na falme zitakapokusanyika

ili kumwabudu Bwana.

23102:23 Za 39:5Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu,

akafupisha siku zangu.

24102:24 Mwa 21:33; Ay 36:26; Za 90:2; Hab 1:12; Ufu 1:4, 8Ndipo niliposema:

“Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu;

miaka yako inaendelea vizazi vyote.

25102:25 Mwa 1:1; Ebr 1:10; 2Nya 2:12; Za 8:3; Kut 20:11; Ay 38:4-7Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia,

nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.

26102:26 Rum 8:20; Isa 51:6; 13:10, 13; 66:21; 34:4; Mt 24:35; Yoe 2:10; Eze 32:8; 2Pet 3:7-10; Ufu 20:11Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu,

zote zitachakaa kama vazi.

Utazibadilisha kama nguo

nazo zitaondoshwa.

27102:27 Hes 23:19; Ebr 13:8; Mal 3:6; Yak 1:17; Za 9:7Lakini wewe, U yeye yule,

nayo miaka yako haikomi kamwe.

28102:28 Za 69:36; 25:13; 89:4Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako;

wazao wao wataimarishwa mbele zako.”