Yoshua 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 9:1-27

Udanganyifu Wa Wagibeoni

19:1 Hes 13:17; 34:6; Kum 3:25; Mwa 13:7; Yos 3:10; 11:19; Kut 3:17Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu,9:1 Yaani Bahari ya Mediterania. hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi), 29:2 2Nya 20:1; Mit 11:11; Isa 8:9-12; Yoe 3:9-12; Mdo 4:26-289:2 1Nya 8:29; 14:16; 16:19; 21:29; 2Nya 1:2; Neh 3:7; Isa 28:21; Yer 28:1; 41:12; Mwa 12:8; Yos 8:1wakajiunga pamoja ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli.

39:3 Yos 10:10; 11:19; 18:25; 21:17; 2Sam 2:21; 5:25; 20:8; 1Fal 3:4Hata hivyo, watu wa Gibeoni waliposikia juu ya hayo yote Yoshua aliyowatendea watu wa Yeriko na Ai, 4nao wakaamua kufanya hila: Wakajifanya kama wajumbe wakiwa na punda waliobebeshwa mizigo wakiwa na magunia yaliyochakaa na viriba vya mvinyo vikuukuu vyenye nyufa zilizozibwa. 5Walivaa miguuni mwao viatu vilivyoraruka na kushonwa kisha wakavaa nguo kuukuu. Chakula chao kilikuwa mkate uliokauka na kuingia koga. 69:6 Kum 11:30; Mwa 26:28; Yos 5:10Ndipo wakamwendea Yoshua kambini huko Gilgali wakamwambia yeye pamoja na watu wa Israeli, “Tumetoka katika nchi ya mbali, fanyeni mkataba nasi.”

79:7 Kut 23:32; 1Fal 5:12; Yos 11:19; Kum 7:2Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, “Lakini huenda mnakaa karibu nasi, twawezaje basi kufanya mapatano nanyi?”

89:8 Kum 20:11; 2Fal 10:5Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.”

Yoshua akawauliza, “Ninyi ni nani, nanyi mnatoka wapi?”

99:9 Kum 20:15; Hes 23:22; Yos 2:9; Ay 32:19; Mt 9:17; Lk 5:37-38; Amu 2:2Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa Bwana Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri, 109:10 Hes 21:24-25; 21:33-35; Yos 2:10pia yale yote aliyowatendea wafalme wawili wa Waamori mashariki ya Yordani; huyo Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani, aliyetawala huko Ashtarothi. 11Basi wazee wetu na wale wote wanaoishi katika nchi yetu walituambia, ‘Chukueni chakula cha safari; nendeni mkakutane na watu hao na kuwaambia, “Sisi tu watumishi wenu, fanyeni mapatano nasi.” ’ 12Mkate huu wetu ulikuwa wa moto tulipoufunga siku tulipoanza safari kuja kwenu, lakini sasa angalia jinsi ulivyokauka na kuota ukungu. 13Viriba hivi vya mvinyo vilikuwa vipya tulipovijaza, lakini ona jinsi vilivyo na nyufa. Nguo zetu na viatu vimechakaa kwa ajili ya safari ndefu.”

149:14 Kut 16:28; Hes 27:21; 1Sam 22:10; 2Sam 5:19; Isa 30:1-2Basi watu wa Israeli wakavikagua vyakula vyao bila kupata shauri kutoka kwa Bwana. 159:15 Yos 10:1, 4; 11:19; 2Sam 21:2; 24:1; Amu 1:21; Za 106:34; Kut 23:32Ndipo Yoshua akafanya mapatano ya amani pamoja nao kuwaacha waishi, nao viongozi wa kusanyiko wakathibitisha kwa kiapo.

16Siku ya tatu baada ya hao kufanya mapatano na Wagibeoni, Waisraeli wakapata habari kuwa hao watu ni jirani zao waliokuwa wanaishi karibu nao. 179:17 Yos 18:25; 2Sam 4:2; 23:37; Yos 15:9; 18:14-15; Amu 18:12; 1Sam 6:21; 7:2; Za 132:6; Yer 26:20Ndipo wana wa Israeli wakasafiri na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao ya Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu. 189:18 Amu 21:1, 7, 18; 1Sam 20:17; Za 15:4; Kut 15:24Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli.

Kusanyiko lote likanungʼunika dhidi ya hao viongozi, 19lakini viongozi wote wakawajibu, “Tumeshawaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli, kwa hiyo hatuwezi kuwagusa sasa. 209:20 Mwa 24:8; Eze 17:13-18; Zek 5:3-4Hivi ndivyo tutakavyowafanyia: Tutawaacha waishi, ili ghadhabu isije juu yetu kwa kuvunja kiapo tulichowaapia.” 219:21 Kum 29:11Wakaendelea kusema, “Waacheni waishi, lakini wawe wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii yote.” Hivyo ahadi waliyoweka viongozi kwao ikawa hivyo.

22Kisha Yoshua akawaita Wagibeoni na kuwaambia, “Kwa nini mmetudanganya kwa kutuambia, ‘Tunaishi mbali nanyi,’ wakati ambapo ninyi mnaishi karibu nasi? 239:23 Mwa 9:25Sasa mko chini ya laana: Daima mtakuwa wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.”

24Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi Bwana Mungu wenu alivyomwamuru mtumishi wake Mose kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwaangamiza wakazi wake wote toka mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili. 259:25 Mwa 16:6; Yer 26:14; Kut 23:32; Kum 20:15-17; Kut 15:14Sasa tupo mikononi mwako. Tufanyieni lolote mnaloona kuwa jema na haki kwako.”

26Kwa hiyo Yoshua akawaokoa mikononi mwa Waisraeli, nao hawakuuawa. 279:27 Kut 1:11; Kum 29:11; 12:5; 1Fal 8:29; 2Nya 7:12, 20; Za 78:68Siku hiyo Yoshua akawafanya Wagibeoni wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana mahali pale ambapo Bwana angepachagua. Hivyo ndivyo walivyo hadi hivi leo.