Yoshua 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 7:1-26

Dhambi Ya Akani

17:1 Yos 6:18; 1Nya 2:7; Yos 22:20; Hes 1:4; Kut 4:14; 32:20; Law 10:6Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyowekwa wakfu; Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alivichukua baadhi ya hivyo vitu. Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli.

27:2 Mwa 12:8; Yos 8:1, 28; 18:12; 1Sam 14:23; Hos 4:15; 5:8; 10:5; Mwa 12:8; Yos 12:16; 16:1; Amu 1:22; 1Sam 30:27; 2Fal 23:15; Yer 48:13; Amo 3:14; 4:4; 5:5-6; 7:10, 13; Hes 21:32Basi Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko waende Ai, karibu na Beth-Aveni mashariki ya Betheli, akawaambia, “Pandeni mkaipeleleze nchi.” Basi wale watu wakapanda wakaipeleleza Ai.

3Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Usiwachoshe watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.” 47:4 Law 26:17; Kum 28:25; 32:30; Isa 30:17; 59:2Basi wakapanda kama watu elfu tatu tu, lakini wakashambuliwa na watu wa Ai, 57:5 Yos 22:20; Mwa 42:28; Za 22; 14; Isa 13:7; Eze 21:7; Nah 2:10; Law 26:36ambao waliwaua watu kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu, nao wakawauwa huko kwenye materemko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka ikawa kama maji.

67:6 Mwa 37:29; 17:3; 1Nya 21:16; Eze 9:8; Amu 20:23; Yos 8:10; 9:11; 20:4; 23:2; 1Sam 4:12; 2Sam 13:19; 15:32; Neh 9:1; Ay 2:12; Eze 27:30; Ufu 18:19Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana, na akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo wakatia mavumbi vichwani mwao. 77:7 1Sam 4:3; Kut 5:22; Hes 14:16; 2Fal 3:10Yoshua akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, kwa nini umewavusha watu hawa ngʼambo ya Yordani ili kututia mikononi mwa Waamori watuangamize? Laiti tungeliridhika kukaa ngʼambo ile nyingine ya Yordani! 8Ee Bwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake? 97:9 Kut 32:12; Kum 9:28; 28:58; 1Sam 12:22; Za 48:10; 106:8; Yer 14:21Wakanaani na watu wengine wa nchi watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kutufutilia jina letu duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenyewe lililo kuu?”

10Bwana akamwambia Yoshua, “Simama! Unafanya nini hapo chini kifudifudi? 117:11 Kut 9:27; Kum 29:27; Yos 24:16-27; 2Fal 17:7; Hos 10:9; Yos 6:17-19; 23:16; Amu 2:20; 1Sam 15:24; Za 78:10; Mdo 5:1-2Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao. 127:12 Law 26:37; Za 18:40; 21:12; Law 26:17; Yos 6:18; Za 44:9; 60:10Ndiyo sababu Waisraeli hawawezi kusimama dhidi ya adui zao. Wanawapa visogo na kukimbia kwa kuwa wanastahili maangamizi. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka mwangamize kila kitu miongoni mwenu kilichotengwa kwa maangamizi.

137:13 Law 11:44; Yos 3:5; Kut 19:10“Nenda, ukawatakase watu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa kesho; kwa sababu hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Kitu kilichowekwa wakfu kipo katikati yenu, ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka mtakapokiondoa.

147:14 1Sam 10:19; Mit 16:33; 1Sam 14:41-42; Yn 1:7; Mdo 1:24-26“ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaa Bwana litakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaoutwaa Bwana utakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakuja mbele mtu kwa mtu. 157:15 Yos 6:18; Kum 7:25; 2Fal 25:9; 1Nya 14:12; Isa 37:19; Yer 43:12; Eze 30:16; 1Sam 14:39; Mwa 34:7Yule atakayekutwa na vitu vilivyowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, pamoja na vitu vyote alivyo navyo. Kwa kuwa amelivunja agano la Bwana na kufanya kitu cha aibu katika Israeli!’ ”

16Kesho yake asubuhi na mapema Yoshua akawaamuru Israeli kuja mbele kabila kwa kabila; na Yuda akatwaliwa. 177:17 Hes 26:20Koo za Yuda zikaja mbele, naye akawatwaa Wazera. Akaamuru ukoo wa Wazera kuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ya Zabdi ikatwaliwa. 187:18 Yos 7:1; Law 24:11; Yn 1:7; Mdo 5:1-10; Yer 2:26; Mit 13:21; Hes 32:23; Mwa 4:7Yoshua akaamuru watu wa jamaa ya Zabdi kuja mbele mtu kwa mtu, naye Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, akatwaliwa.

197:19 Kut 14:17; 1Sam 6:5; Za 96:8; Isa 42:12; Yer 13:16; Yn 9:24; Law 5:5; 1Sam 14:43Ndipo Yoshua akamwambia Akani, “Mwanangu, mtukuze Bwana, Mungu wa Israeli, nawe ukiri kwake. Niambie ni nini ulichotenda; usinifiche.”

20Akani akamjibu Yoshua, “Ni kweli! Nimetenda dhambi dhidi ya Bwana, Mungu wa Israeli. Hili ndilo nililofanya: 217:21 Mwa 34:29; 49:27; Kum 7:25; Efe 5:5; 1Tim 6:10; Kut 20:17; 1Fal 21:1; 2Fal 5:20-27; Mit 15:27; Hab 2:9; Lk 12:15; Rum 7:7, 8Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili7:21 Shekeli 200 za fedha ni sawa na kilo 2.3. za fedha, na kabari ya dhahabu ya uzito wa shekeli hamsini,7:21 Shekeli 50 ni sawa na gramu 600. nikavitamani na nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”

22Kwa hiyo Yoshua akatuma wajumbe, nao wakapiga mbio mpaka hemani, tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, pamoja na ile fedha chini yake. 23Wakavichukua vile vitu toka mle hemani, wakamletea Yoshua pamoja na Waisraeli wote, na wakavitandaza mbele za Bwana.

247:24 Hes 16:27; Yos 7:26; 15:7; Isa 65:10; Hos 2:15Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, lile joho, ile kabari ya dhahabu, wanawe na binti zake, ngʼombe, punda na kondoo wake, hema yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori. 257:25 Yos 6:18; Law 20:2; Kum 17:5; 1Fal 12:18; 2Nya 10:18; 24:21; Neh 9:26; Mwa 38:24; 1Nya 2:7; Gal 5:12Yoshua akasema, “Kwa nini umeleta taabu hii juu yetu? Bwana ataleta taabu juu yako leo hii.”

Ndipo Israeli yote ikampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto. 267:26 2Sam 18:17; Mwa 35:20; Hes 25:4; Kum 13:17; Isa 65:10; Hos 2:15; Yos 8:29; 2Sam 18:17; Mao 3:53; Kum 13:17; 2Sam 21:14Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo mpaka leo. Naye Bwana akageuka kutoka hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori7:26 Akori yamaanisha taabu. tangu siku hiyo.