Yoshua 24 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 24:1-33

Agano Lafanywa Upya Huko Shekemu

124:1 Mwa 49:2; 12:6; 1Sam 12:7; 1Fal 8:14; Yos 7:6; 23:2; Amu 9:1-3; Kut 18:25; 1Sam 10:10; Mdo 10:33Ndipo Yoshua akaita pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu. Akawaita wazee, viongozi, waamuzi na maafisa wa Israeli, nao wakaja mbele za Mungu.

224:2 Mwa 23:2; 11:32; Kum 26:5; Isa 51:2Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Abrahamu na Nahori, waliishi ngʼambo ya Mto nao waliiabudu miungu mingine. 324:3 Mwa 12:1; 1:28; 12:2; 21:3; Mdo 7:2; Za 127:3Lakini nilimwondoa baba yenu Abrahamu kutoka nchi hiyo ngʼambo ya Mto, nami nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani, nikampa wazao wengi. Nikampa Isaki, 424:4 Mwa 25:26; 14:6; Hes 24:18; Mwa 46:5-6; Kum 2:5; Mdo 17:26naye Isaki nikampa Yakobo na Esau. Esau nikampa nchi ya vilima ya Seiri, lakini Yakobo pamoja na wanawe wakashuka Misri.

524:5 Kut 3:10; 12:51“ ‘Kisha nikawatuma Mose na Aroni, nami nikawapiga Wamisri kwa kile nilichokitenda huko, tena nikawatoa ninyi huko. 624:6 Kut 14:22; 14:9; 4:23; Mik 6:4; Neh 9:11; Za 78:13; Isa 63:12, 13Nilipowatoa baba zenu Misri, mlifika kwenye bahari, nao Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka kwenye Bahari ya Shamu. 724:7 Kut 14:10, 20, 28; 19:4; Kum 1:46Lakini wakamlilia Bwana wakitaka msaada, naye akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu.

824:8 Kut 23:23; Hes 21:31“ ‘Nikawaleta katika nchi ya Waamori ambao waliishi mashariki mwa Yordani. Wakapigana nanyi, lakini nikawatia mikononi mwenu. Nikawaangamiza mbele yenu nanyi mkaimiliki nchi yao. 924:9 Hes 22:2, 6; 23:7Wakati Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, alipojiandaa kupigana dhidi ya Israeli, alimwita Balaamu mwana wa Beori apate kuwalaani. 1024:10 Hes 23:10; Kum 23:5Lakini sikumkubali Balaamu, kwa hiyo aliwabariki tena na tena, nami niliwaokoa toka mkononi mwake.

1124:11 Kut 14:29; Yos 6:1; 3:10; Mwa 15:18-21; Kut 23:23; Kum 7:1“ ‘Ndipo mlipovuka Yordani mkafika Yeriko. Raiya wa Yeriko wakapigana nanyi, kama walivyofanya Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi, lakini niliwatia mikononi mwenu. 1224:12 Kut 23:28; Za 44:3-7; Kut 23:31; Za 135:11; Kum 7:20Nikatuma manyigu mbele yenu, ambao pia waliwafukuza mbele yenu, hao wafalme wawili wa Waamori. Siyo upanga au upinde wenu wenyewe vilivyowapatia ushindi. 1324:13 Kut 6:8; Kum 6:10-11; Yos 11:13; Mit 13:22Hivyo nikawapa ninyi nchi ambayo hamkuitaabikia na miji ambayo hamkuijenga na mnaishi ndani yake na kula toka kwa mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.’

1424:14 1Sam 12:14; Ay 23:15; Za 19:9; 119:120; Kum 10:12; 18:13; 1Sam 12:24; 2Kor 1:20; Mwa 31:19; Kut 12:12; 18:11; 20:3; Hes 25:2; Kum 11:28; Amu 10:16; 10:16; Rut 1:15; Isa 55; 7; Eze 23; 3“Sasa basi mcheni Bwana na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ngʼambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieni Bwana. 1524:15 Amu 6:10; Rut 1:15-16; 2:12; Mwa 35:2; 1Fal 18:21; Dan 3:18Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana.”

1624:16 Yos 22:29Ndipo hao watu wakajibu, “Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Bwana na kuitumikia miungu mingine! 1724:17 Amu 6:8; Kut 10:1Bwana Mungu wetu mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao. 1824:18 Kut 23:31; Kum 33:27; Mdo 7:45; Mwa 28:21Bwana akayafukuza mbele yetu mataifa yote pamoja na Waamori, walioishi katika nchi hii. Hivyo sisi nasi tutamtumikia Bwana kwa kuwa yeye ndiye Mungu wetu.”

1924:19 Law 11:44; 20:26; Kut 20:5; 34:7; 23:21; Rut 1:15; Mt 6:24; Lk 14:25-33; Law 19:2; 1Sam 6:20; Za 99:5, 9; Isa 5:16; Kut 23:21Yoshua akawaambia watu, “Hamwezi kumtumikia Bwana. Yeye ni Mungu Mtakatifu, ni Mungu mwenye wivu. Hatasamehe uasi wenu na dhambi zenu. 2024:20 1Nya 28:9, 20; 2Nya 24:18; Mdo 7:42; 1Sam 12:25; Hos 13:11; Yos 23:15; Ezr 8:22; Isa 1:28; 63:10; Yer 17:13; Ebr 10:26-28Ikiwa mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, atageuka na kuwaleteeni maafa na kuwaangamiza, baada ya kuwa mwema kwenu.”

21Lakini watu wakamwambia Yoshua, “Sivyo! Sisi tutamtumikia Bwana.”

2224:22 Rut 2:10; Isa 8; 2; 43:10; 44:8; Yer 42:5; Mal 2:14; Za 119:30, 173; Kum 25:9Ndipo Yoshua akawaambia, “Ninyi mmekuwa mashahidi juu yenu wenyewe kuwa mmechagua kumtumikia Bwana.”

Nao wakajibu, “Ndiyo, tu mashahidi.”

2324:23 1Fal 8:58; Za 119:36; 141:4; Yer 31:33Yoshua akawaambia, “Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni iliyo katikati yenu, nanyi mtoleeni Bwana, Mungu wa Israeli, mioyo yenu.”

2424:24 Kut 19:8; Yer 42:6Nao watu wakamwambia Yoshua, “Tutamtumikia Bwana Mungu wetu na kumtii yeye.”

2524:25 Kut 24:8; Yos 17:7; Kut 15:25Siku ile Yoshua akafanya agano kwa ajili ya watu na hapo Shekemu ndipo alipowaandikia amri na sheria. 2624:26 Kum 17:18; 28:61; 31:24; Mwa 28:18; Kum 27:2; Mwa 12:6; Amu 4:11Naye Yoshua akayaandika mambo haya katika Kitabu cha Sheria ya Mungu. Ndipo akalitwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko chini ya mwaloni, karibu na mahali patakatifu pa Bwana.

2724:27 Mwa 28:18; 21:30; Yos 22:27; 7:11; Hes 11:20; Mit 30:9Yoshua akawaambia watu wote, “Angalieni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote Bwana aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.”

Kuzikwa Katika Nchi Ya Ahadi

2824:28 Amu 21:23-24Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe.

2924:29 Amu 1:1; Mwa 50:22Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. 3024:30 Yos 19:50; 2Sam 23:30; Amu 2:7Nao wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Sera24:30 Unajulikana pia kama Timnath-Heresi, ona Yos 19:50; Amu 2:9. katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima wa Gaashi.

3124:31 Yos 7:6Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kitu Bwana alichowatendea Israeli.

3224:32 Ebr 11:22; Mwa 47:29-30; 33:19; Yn 4:6; Mdo 7:16; Mwa 50:25; Kut 13:19Nayo ile mifupa ya Yosefu, ambayo Waisraeli waliipandisha kutoka huko Misri, wakaizika huko Shekemu kwenye eneo, ambalo Yakobo alilinunua kwa wana wa Hamori baba yake Shekemu, kwa vipande mia vya fedha. Eneo hili likawa ni urithi wa uzao wa Yosefu.

3324:33 Yos 22:13; 15:57; Kut 6:25; 1Sam 9:4; 1Fal 8:4; Kut 6:25; Amu 20:28Naye Eleazari mwana wa Aroni akafariki akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.

New International Version

Joshua 24:1-33

The Covenant Renewed at Shechem

1Then Joshua assembled all the tribes of Israel at Shechem. He summoned the elders, leaders, judges and officials of Israel, and they presented themselves before God.

2Joshua said to all the people, “This is what the Lord, the God of Israel, says: ‘Long ago your ancestors, including Terah the father of Abraham and Nahor, lived beyond the Euphrates River and worshiped other gods. 3But I took your father Abraham from the land beyond the Euphrates and led him throughout Canaan and gave him many descendants. I gave him Isaac, 4and to Isaac I gave Jacob and Esau. I assigned the hill country of Seir to Esau, but Jacob and his family went down to Egypt.

5“ ‘Then I sent Moses and Aaron, and I afflicted the Egyptians by what I did there, and I brought you out. 6When I brought your people out of Egypt, you came to the sea, and the Egyptians pursued them with chariots and horsemen24:6 Or charioteers as far as the Red Sea.24:6 Or the Sea of Reeds 7But they cried to the Lord for help, and he put darkness between you and the Egyptians; he brought the sea over them and covered them. You saw with your own eyes what I did to the Egyptians. Then you lived in the wilderness for a long time.

8“ ‘I brought you to the land of the Amorites who lived east of the Jordan. They fought against you, but I gave them into your hands. I destroyed them from before you, and you took possession of their land. 9When Balak son of Zippor, the king of Moab, prepared to fight against Israel, he sent for Balaam son of Beor to put a curse on you. 10But I would not listen to Balaam, so he blessed you again and again, and I delivered you out of his hand.

11“ ‘Then you crossed the Jordan and came to Jericho. The citizens of Jericho fought against you, as did also the Amorites, Perizzites, Canaanites, Hittites, Girgashites, Hivites and Jebusites, but I gave them into your hands. 12I sent the hornet ahead of you, which drove them out before you—also the two Amorite kings. You did not do it with your own sword and bow. 13So I gave you a land on which you did not toil and cities you did not build; and you live in them and eat from vineyards and olive groves that you did not plant.’

14“Now fear the Lord and serve him with all faithfulness. Throw away the gods your ancestors worshiped beyond the Euphrates River and in Egypt, and serve the Lord. 15But if serving the Lord seems undesirable to you, then choose for yourselves this day whom you will serve, whether the gods your ancestors served beyond the Euphrates, or the gods of the Amorites, in whose land you are living. But as for me and my household, we will serve the Lord.”

16Then the people answered, “Far be it from us to forsake the Lord to serve other gods! 17It was the Lord our God himself who brought us and our parents up out of Egypt, from that land of slavery, and performed those great signs before our eyes. He protected us on our entire journey and among all the nations through which we traveled. 18And the Lord drove out before us all the nations, including the Amorites, who lived in the land. We too will serve the Lord, because he is our God.”

19Joshua said to the people, “You are not able to serve the Lord. He is a holy God; he is a jealous God. He will not forgive your rebellion and your sins. 20If you forsake the Lord and serve foreign gods, he will turn and bring disaster on you and make an end of you, after he has been good to you.”

21But the people said to Joshua, “No! We will serve the Lord.”

22Then Joshua said, “You are witnesses against yourselves that you have chosen to serve the Lord.”

“Yes, we are witnesses,” they replied.

23“Now then,” said Joshua, “throw away the foreign gods that are among you and yield your hearts to the Lord, the God of Israel.”

24And the people said to Joshua, “We will serve the Lord our God and obey him.”

25On that day Joshua made a covenant for the people, and there at Shechem he reaffirmed for them decrees and laws. 26And Joshua recorded these things in the Book of the Law of God. Then he took a large stone and set it up there under the oak near the holy place of the Lord.

27“See!” he said to all the people. “This stone will be a witness against us. It has heard all the words the Lord has said to us. It will be a witness against you if you are untrue to your God.”

28Then Joshua dismissed the people, each to their own inheritance.

Buried in the Promised Land

29After these things, Joshua son of Nun, the servant of the Lord, died at the age of a hundred and ten. 30And they buried him in the land of his inheritance, at Timnath Serah24:30 Also known as Timnath Heres (see Judges 2:9) in the hill country of Ephraim, north of Mount Gaash.

31Israel served the Lord throughout the lifetime of Joshua and of the elders who outlived him and who had experienced everything the Lord had done for Israel.

32And Joseph’s bones, which the Israelites had brought up from Egypt, were buried at Shechem in the tract of land that Jacob bought for a hundred pieces of silver24:32 Hebrew hundred kesitahs; a kesitah was a unit of money of unknown weight and value. from the sons of Hamor, the father of Shechem. This became the inheritance of Joseph’s descendants.

33And Eleazar son of Aaron died and was buried at Gibeah, which had been allotted to his son Phinehas in the hill country of Ephraim.