Yoshua 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 23:1-16

Yoshua Anawaaga Viongozi

123:1 Kum 12:9; Yos 21:44; 13:1Baada ya muda mrefu kupita, naye Bwana akawa amewapa Israeli pumziko mbele ya adui zao wote waliowazunguka, Yoshua, wakati huo akiwa mzee na umri ukiwa umeendelea sana, 223:2 Yos 7:6; 24:1; 13:1; Kum 31:28; 1Nya 28:1akawaita Israeli wote, wazee wao, viongozi, waamuzi na maafisa Yoshua akawaambia: “Mimi ni mzee na umri wangu umeendelea sana. 323:3 Kut 14:14; Kum 20:4Ninyi wenyewe mmeona kila kitu Bwana Mungu wenu, alichowatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Ilikuwa ni Bwana Mungu wenu aliyewapigania. 423:4 Yos 19:51; Hes 34:2-6; Za 78:55Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari kuu upande wa magharibi. 523:5 Amu 2:21; Za 44:5; Yer 46:15; Kut 23:30; 33:2Bwana Mungu wenu mwenyewe atawaondoa watoke mbele yenu. Atawafukuza mbele yenu, nanyi mtamiliki nchi yao, kama vile Bwana Mungu wenu alivyowaahidi.

623:6 Kum 28:6; 17:20; Yos 1:7; Kum 5:32“Kuweni hodari sana, kuweni waangalifu kutii yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria ya Mose, pasipo kugeuka upande wa kuume au kushoto. 723:7 Kut 23:13; Yer 5:7; 12:16; Kut 20:5Msishirikiane na mataifa yaliyobakia katikati yenu, wala msiombe kwa majina ya miungu yao au kuapa kwayo. Msiitumikie wala kuisujudia. 823:8 Kum 10:20Bali mtashikamana kwa uthabiti na Bwana, Mungu wenu, kama vile ambavyo mmefanya mpaka sasa.

923:9 Kum 11:23; 7:24Bwana amewafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu, mpaka siku ya leo hakuna yeyote aliyeweza kusimama mbele yenu. 1023:10 Law 26:8; Amu 3:31; Kut 14:14; Kum 3:22Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawapigania, kama alivyoahidi. 1123:11 Kum 4:15; Yos 2:15Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpenda Bwana Mungu wenu.

1223:12 Mwa 34:9; Kut 34:16; Za 106:34-35“Lakini ikiwa mtageuka na kushikamana na mabaki ya mataifa haya yaliyosalia katikati yenu na kama mtaoana na kushirikiana nao, 1323:13 Kut 10:7; Hes 33:55; Kum 1:8; 2Fal 25:21basi mwe na hakika kuwa Bwana Mungu wenu hatawafukuza tena mataifa hayo mbele yenu. Badala yake, watakuwa tanzi na mitego kwenu, mijeledi migongoni mwenu, na miiba machoni mwenu, mpaka mwangamie kutoka nchi hii nzuri, ambayo Bwana Mungu wenu amewapa.

1423:14 1Fal 2:2; Za 119:140; 145:13; Yos 21:25“Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njema Bwana Mungu wenu alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia. 1523:15 1Fal 8:56; Yer 33:14; 1Fal 14:10; 2Fal 22:16; Isa 24:6; 34:5; 43:28; Yer 40:2; 11:8; 35:17; 39:16; Mal 4:6; Yos 24:20; Law 26:17; Kum 28:15; Yer 40:2Lakini kama vile kila ahadi njema ya Bwana Mungu wenu imekuwa kweli, vivyo hivyo Bwana ataleta maovu yote kama alivyo onya, mpaka awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa. 1623:16 Kum 4:25-26Kama mkilivunja agano la Bwana Mungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira ya Bwana itawaka dhidi yenu, nanyi mtaangamia kutoka nchi nzuri aliyowapa ninyi.”