Yoshua 2 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 2:1-24

Rahabu Na Wapelelezi

12:1 Mwa 42:9; Hes 25:1; Yos 3:1; Yoe 3:18; Hes 21:32; Amu 18:2; Hes 33:48; Yos 6:17, 25; Ebr 11:31Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja jina lake Rahabu na kukaa humo.

22:2 Za 127:1; Mit 21:30Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” 32:3 Yos 6:23Hivyo mfalme wa Yeriko akatuma huu ujumbe kwa Rahabu: “Watoe wale watu waliokujia na kuingia nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi yote.”

42:4 Yos 6:22; 6:17; 2Sam 17:19-20; 2Fal 6:19Lakini huyo mwanamke alikuwa amewachukua hao watu wawili na kuwaficha. Akasema, “Naam, watu hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. 52:5 Amu 5:8; 9:35; 16:2; Ebr 11:31Kulipoingia giza, wakati wa kufunga lango la mji, watu hao waliondoka. Sijui njia waliyoiendea. Wafuatilieni haraka. Huenda mkawapata.” 62:6 Amu 15:14; Mit 31:13; Isa 19:9; Kut 1:19; Yos 6:25; 2Sam 17:19; Yak 2:25; Kut 1:17(Lakini alikuwa amewapandisha darini akawafunika kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini.) 72:7 Hes 22:1; Amu 3:28; 7:24; 12:5-6; Isa 16:2Basi hao watu wakaondoka kuwafuatilia hao wapelelezi katika njia ile inayoelekea vivuko vya Yordani, mara tu wafuatiliaji walipotoka nje, lango likafungwa.

82:8 Kum 22:8; Amu 16:27; 2Sam 16:22; Neh 8:16; Isa 15:3; 22:1; Yer 32:29Kabla wale wapelelezi hawajalala, Rahabu akawaendea huko juu darini, 92:9 Mwa 35:5; Kut 15:14-15; Mwa 35:5; Kum 2:25; 11:25akawaambia, “Ninajua kuwa Bwana amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote waishio katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu. 102:10 Mwa 8:1; Kut 14:21; Yos 3:17; Za 74:15; Hes 23:22; 21:21; Mwa 10:16; 14:7; Yos 9:10Tumesikia jinsi Bwana alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa. 112:11 Mwa 42:28; Kum 2:25; Za 107:26; Yon 1:5; Kut 15:14; Yos 5:1; 7:5; 2Sam 4:1; Za 22; 14; Isa 13:7; 19:1; Yer 51:30; Nah 2:10; 2Fal 5:15; 19:15; Dan 6:26; Mwa 14:19; Hes 20:14; Kum 4:39Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana Bwana Mungu wenu ni Mungu juu mbinguni na duniani chini. 122:12 Mwa 24:8; 47:31; 24; 12; Rut 3:10; Mwa 24:14; Kut 3:12; Yos 4:6; 1Sam 2:34; 2Fal 19:29Sasa basi, tafadhali niapieni kwa Bwana, kwamba mtaitendea hisani jamaa ya baba yangu, kwa kuwa mimi nimewatendea hisani. Nipeni ishara ya uaminifu 132:13 Yos 6:23kwamba mtayahifadhi maisha ya baba yangu na mama yangu, ndugu zangu wa kiume na wa kike, pamoja na wale wote walio wa kwao na kwamba mtatuokoa na kifo.”

142:14 1Fal 20:39-42; 2Fal 10:24; Mwa 47:29; Mt 5:7; Amu 1:24; Mt 5:7Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, wakati Bwana atakapotupa nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.”

152:15 Yer 38:6, 11; Mwa 26:8; Amu 5:28; 1Sam 19:12; Mdo 9:25; Ebr 11:31Kisha akawateremsha dirishani kwa kamba, kwa kuwa nyumba yake aliyokuwa anaishi ilikuwa sehemu ya ukuta wa mji. 162:16 Yak 2:25; Mwa 14:10; Ebr 11:31Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watakaporudi, hatimaye mwende zenu.”

172:17 Mwa 24:8; Kut 20:7Wale watu wakamwambia, “Hiki kiapo ulichotuapisha hakitatufunga, 182:18 Yos 6:23; Mwa 7:1; 19:12, 17; Es 8:6; Mdo 11:14; 2Tim 1:16isipokuwa, hapo tutakapoingia katika nchi hii, utakuwa umefunga hii kamba nyekundu dirishani pale ulipotuteremshia na kama utakuwa umewaleta baba yako na mama yako, ndugu zako na jamaa yako yote ndani ya nyumba yako. 192:19 Law 20:9; Eze 33:4; Hes 34:26, 27Ikiwa mtu yeyote atatoka nje ya nyumba yako akaenda mtaani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, hatutawajibika. Lakini yule ambaye atakuwa ndani pamoja nawe, kama mkono wa mtu yeyote ukiwa juu yake damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu. 202:20 Mwa 24:8; 47:31Lakini ikiwa utatoa habari ya shughuli yetu tunayofanya, tutakuwa tumefunguliwa kutoka kwenye kiapo hiki ulichotufanya tuape.”

21Naye akajibu, “Nimekubali. Na iwe kama mnavyosema.” Kwa hiyo akaagana nao, nao wakaondoka. Yeye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani.

22Walipoondoka, wakaelekea vilimani na kukaa huko siku tatu, hadi wale waliokuwa wakiwafuatilia wakawa wamewatafuta njia nzima na kurudi pasipo kuwapata. 23Ndipo wale watu wawili wakaanza kurudi. Wakashuka kutoka kule vilimani, wakavuka mto na kuja kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kumweleza kila kitu kilichowapata. 242:24 Yos 10:8; 11:6; Amu 3:28; 7:9; 20:28; 1Sam 14:10; Kut 15:15Wakamwambia Yoshua, “Hakika Bwana ametupa nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

約書亞記 2:1-24

喇合營救探子

1的兒子約書亞暗中從什亭派出兩個探子,去偵察那片土地,特別是耶利哥的情況。他們進到一個名叫喇合的妓女家中,就住在那裡。 2有人告訴耶利哥王說:「今晚有以色列人來這裡刺探。」 3耶利哥王便派人到喇合那裡,對她說:「把來到你家裡的人交出來,因為他們是來刺探這地方的。」 4喇合已經把二人藏起來了,她答道:「不錯,他們來過,可是我不知他們是從哪裡來的。 5天黑要關城門的時候,他們就離開了,我不知道他們去哪裡了。你們快去追吧,還可以追上。」 6其實喇合已經把二人帶到屋頂上,藏在那裡的麻稈堆裡了。 7追捕的人便沿著通往約旦河渡口的路追去,他們一出城,城門便關閉了。

8在兩個探子睡覺前,喇合上到屋頂對他們說: 9「我知道耶和華已經把這地方賜給你們,我們對你們充滿恐懼。這裡所有的居民都嚇得膽戰心驚。 10因為你們離開埃及過紅海的時候,耶和華怎樣使紅海在你們面前成為乾地,你們怎樣對付約旦河東的兩個亞摩利西宏,把他們徹底消滅,我們都聽說了。 11我們聽了這些事,感到心驚膽戰、勇氣盡失。你們的上帝耶和華是天地萬物的上帝。 12我既然恩待了你們,現在請你們憑耶和華向我起誓,你們同樣會恩待我家,並且給我一個可靠的憑據, 13保證放過我的父母、兄弟、姊妹和他們所有的親人,救我們脫離死亡。」 14二人便對她說:「只要你不洩露我們的事,我們願意用性命擔保,當耶和華把這地方賜給我們的時候,我們一定守信善待你。」

15喇合的房子就在城牆邊,她就住在城牆上,於是她用繩子把二人從窗口縋下去, 16並對他們說:「你們往山上去,免得被追捕的人發現。你們要在那裡躲三天,等追捕的人回城後再走。」 17二人對她說:「要讓我們信守誓言,你必須這樣做: 18我們來攻佔這座城的時候,你要把這條朱紅色繩子繫在縋我們下去的窗戶上,並且把你的父母、兄弟、姊妹和他們的親人都召集到你家裡。 19倘若有人離開這房子跑到街上遭遇不測,我們不負任何責任。我們一定保證屋內所有人的性命安全。 20如果你洩露我們的事,你要我們起的誓也就作廢了。」 21喇合說:「一言為定!」於是她送走他們,把朱紅色的繩子繫在窗戶上。

22二人到山上躲藏了三天,等追捕的人回去。追捕的人沿途搜索,毫無所獲,便回去了。 23二人便下山,過河回到的兒子約書亞那裡,向他稟告整個經過, 24又說:「耶和華確實將那整片土地交給我們了,那裡的居民聽到我們的消息,都嚇得膽戰心驚。」