Yoshua 18 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 18:1-28

Mgawanyo Wa Nchi Iliyobaki

118:1 Yos 19:51; 21:2; Amu 18:31; 21:12; 1Sam 1:3; 3:21; 4:3; 1Fal 14:2; Za 78:60; Yer 7:12; 26:6; 41:5; Kut 27:21; 40:2; Mdo 7:45Kusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao, 2lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao.

318:3 Amu 18:9; Sef 3:16; Mt 20:6; Yn 6:27; Flp 3:13-14Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa? 418:4 Mik 2:5Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi na kuniandikia mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Nao watanirudia. 518:5 Yos 15:1; 16:1-4Mtaigawanya hiyo nchi katika sehemu saba. Yuda atabaki katika eneo lake upande wa kusini na nyumba ya Yosefu katika nchi yake upande wa kaskazini. 618:6 Law 16:8; Yos 14:2Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura kwa kura mbele za Bwana Mungu wetu. 718:7 Yos 13:33; 13:8Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa Bwana ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Mose mtumishi wa Bwana aliwapa.”

8Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo kuihusu. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za Bwana.” 9Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi. Wakaandika maelezo yake kwenye kitabu, mji kwa mji, katika sehemu saba na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo. 1018:10 Hes 34:13; Yer 7:12; Hes 33:54; Yos 19:51; Mit 16:33Basi Yoshua akawapigia kura huko Shilo mbele za Bwana, na hapo akagawanya ile nchi kwa Waisraeli kufuatana na mgawanyo wa kabila zao.

Mgawo Kwa Benyamini

11Kura iliangukia kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yosefu.

1218:12 Yos 8:15; 7:2Upande wa kaskazini mpaka wao ulianzia pale Yordani, kupitia kaskazini ya mteremko wa Yeriko na kuendelea magharibi kuingia katika nchi ya vilima, ukitokea kwenye jangwa la Beth-Aveni. 1318:13 Mwa 28:19; Yos 12:9; Hes 32:3; Yos 16:5; Amu 1:23; Hes 18:20; Kum 10:9; Eze 44:28Kutoka hapo ulikatiza kwenye mteremko wa kusini mwa Luzu (yaani Betheli) na kushuka hadi Ataroth-Adari katika kilima kusini mwa Beth-Horoni ya Chini.

1418:14 Yos 10:10; 9:17; 1Nya 13:6Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.

1518:15 Yos 15:9Upande wa kusini mpaka ulianzia kwenye viunga vya Kiriath-Yearimu kwa upande wa magharibi, nao ukatokeza kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa. 1618:16 Yos 17:15; 15:7-8; 2Fal 23:10; 2Nya 28:3; 33:6; Isa 30:33; Yer 19:2; Yos 15:8Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Refaimu. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli. 1718:17 Yos 22:10; 15:6-7Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. 1818:18 Yos 15:6; 11:2; 16:1Ukaendelea upande wa mteremko wa kaskazini wa Beth-Araba ukateremka hadi Araba. 1918:19 Yos 15:6; Mwa 14:3Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini.

2018:20 1Sam 9:1; Yos 21:4, 17Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki.

Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.

2118:21 Yos 6:26; 1Fal 16:34; Lk 10:30Kabila ya Benyamini, ukoo kwa ukoo, ilikuwa na miji mikubwa ifuatayo:

Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi, 2218:22 Yos 15:6; 2Nya 13:4; Yos 16:1Beth-Araba, Semaraimu, Betheli, 2318:23 Kum 2:23; Amu 6:11, 24; 8:27, 32; 9:6; 1Sam 13:17Avimu, Para na Ofra, 2418:24 Yos 21:17; 1Sam 13:3, 16; 14:5; 1Fal 15:22; 2Fal 23:8; Isa 10:29; Amu 19:12-16; Ezr 2:26Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

2518:25 Yos 10:40; Amu 4:5; 19:13; 1Sam 2:11; 7:17; 25:1; Neh 11:33; 1Fal 15:17, 21; Neh 7:29Gibeoni, Rama na Beerothi, 2618:26 Yer 11:3; Yos 9:17; Ezr 2:25; Neh 7:29Mispa, Kefira, Moza, 27Rekemu, Irpeeli, Tarala, 2818:28 2Sam 21:14; Yos 15:8; 10:1; 15:57; 9:17; Eze 48:23; Mwa 46:21; Mdo 17:26Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na minne pamoja na vijiji vyake.

Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake.