Yoshua 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 17:1-18

Mgawo Wa Nusu Nyingine Ya Manase Upande Wa Magharibi

117:1 Hes 1:34; 1Nya 7:14; Mwa 41:51; 50:23; Yos 12:2, 5Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu. 217:2 Hes 26:30; Amu 6:11, 34; 8:2; 1Nya 7:14-19; Hes 27:1Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wale wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yosefu kwa koo zao.

317:3 Hes 27:1; 26:33Basi Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase hakuwa na wana waume ila mabinti tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. 417:4 Hes 27:5-7; Yos 14:1Wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “Bwana alimwagiza Mose atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la Bwana. 517:5 Yos 13:30-31Fungu la Manase lilikuwa na sehemu kumi za nchi, licha ya Gileadi na Bashani mashariki mwa Yordani, 6kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi miongoni mwa wana wa kiume. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wazao wa Manase waliobaki.

717:7 Yos 19:24, 31; 21:6, 30; Amu 1:31; 5:17; 6:35; 7:23; Yos 16:6; Mwa 12:6; Yos 21:12; 24:25Eneo la Manase lilienea kuanzia Asheri hadi Mikmeta mashariki mwa Shekemu. Mpaka ule ulielekea upande wa kusini kutoka pale kujumuisha watu walioishi En-Tapua. 817:8 Yos 12:17; 15:34(Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.) 917:9 Yos 16:8Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde na kuishia kwenye bahari. 1017:10 Mwa 30:18; Eze 48:5Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki.

1117:11 Amu 1:27; 1Sam 31:10; 2Sam 21:12; 1Fal 4:12; 1Nya 7:29; 2Fal 9:27; Yos 11:2; 1Sam 28:7; Za 83:10; Yos 12:21; 1Fal 9:15; Eze 48:4Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori,17:11 Ndiyo Nafoth-Dori. Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi).

1217:12 Yos 15:63; Hes 26:29; 32:39, 41Lakini Wamanase hawakuweza kuimiliki miji hii, kwa kuwa Wakanaani walikazana kuishi katika maeneo hayo. 1317:13 Amu 1:27-28; Kut 23:29-33; Amu 1:27, 28Hata hivyo, Waisraeli walivyoendelea kupata nguvu waliwatumikisha Wakanaani na kuwatia katika kazi za kulazimishwa, lakini hawakuwafukuza kabisa.

Kabila La Yosefu Lakataa

1417:14 Hes 26:28-37; Yos 16:4; Mwa 48:22; 48:19Watu wa Yosefu wakamwambia Yoshua, “Kwa nini umetupa sisi mgawo mmoja tu na sehemu moja tu kuwa urithi? Sisi tu watu wengi sana, na Bwana ametubariki kwa wingi.”

1517:15 2Sam 18:6; Yos 3:10; Mwa 14:5; Yos 15:8; 18:16; 2Sam 5:18; 23:13; 1Sam 17:5Yoshua akajibu, “Kama ninyi ni wengi sana, na kama nchi ya vilima ya Efraimu ni ndogo sana kwenu, pandeni msituni mkafyeke eneo kwa ajili yenu wenyewe huko kwenye nchi ya Waperizi na Warefai.”

1617:16 Amu 1:19; 4:3, 13; Yos 15:56; 1Sam 29:1; Amu 6:33; 1Fal 4:12; 18:46Watu wa Yosefu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wanayo magari ya vita ya chuma, wote wa Beth-Shani na miji yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.”

1717:17 Eze 48:5Lakini Yoshua akanena na nyumba ya Yosefu, yaani Efraimu na Manase: “Ninyi ni wengi sana na wenye nguvu sana. Hamtakuwa na mgawo mmoja tu, 1817:18 1Sam 1:1; Kum 20:1; Yos 11:4-6; 13:6; Rum 8:31; Ebr 13:6bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”