Yoshua 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 14:1-15

Mgawanyo Wa Nchi Magharibi Mwa Yordani

114:1 Yos 11:23; Za 16:6; 136:21; Kut 6:23; Yos 21:1; Hes 26:53; 34:17-18; Yos 19:51Basi haya ndiyo maeneo Waisraeli waliyopokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliwagawia. 214:2 Law 16:8; Hes 34:13; Za 16:5; Mit 16:33; 18:18Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kama Bwana alivyoamuru Mose. 314:3 Hes 32:33; 34:14; 35:2; Yos 13:14Mose alikuwa amewapa yale makabila mawili na nusu urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi miongoni mwa hao wengine, 414:4 Mwa 41:54; Amu 1:29; Hes 35:2-3; Yos 21:2kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe wao. 514:5 Hes 34:13; 35:2; Yos 21:2; Eze 45:1-8; 48:8, 22Kwa hiyo Waisraeli wakagawana ile nchi, kama vile Bwana alivyomwagiza Mose.

Kalebu Anapewa Mji Wa Hebroni

614:6 Kum 11:30; Hes 13:6; 14:30; Kum 33:1; Hes 14:38; Yos 15:17; Kum 1:19Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo Bwana alimwambia Mose mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi. 714:7 Yos 15:6; Hes 13:17; 13:30; 14:6-9Nilikuwa na umri wa miaka arobaini, wakati Mose mtumishi wa Bwana, aliponituma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza hiyo nchi. Nami nikamletea taarifa kama kulingana na nilivyosadiki moyoni. 814:8 Hes 13:31; 14:24; 32:12; Kum 1:36; Ufu 14:4Lakini ndugu zangu tuliopanda nao waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu. Bali mimi, nilimfuata Bwana Mungu wangu kwa moyo wote. 914:9 Kum 11:24; Hes 14:24; Yos 1:3; Hes 13:22Hivyo katika siku ile, Mose akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata Bwana Mungu wangu kwa moyo wote.’

1014:10 Hes 11:28; 14:30; Yos 5:6; 13:1; Hes 14:30; Kum 31:2; Za 90:10“Sasa basi, kama vile Bwana alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano! 1114:11 Kum 34:7; Mwa 15:15Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule. 1214:12 Hes 14:24-28; 13:33; 1Sam 14:6; 2Nya 14:11, 12; Za 18:32; 44:3; Rum 8:31; Flp 4:13; Yos 15:14; Amu 1:10Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo Bwana aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada wa Bwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”

1314:13 Yos 22:6-7; 1Sam 30:14; Mwa 23:19; Yos 10:36; Amu 1:26; 1Nya 6:56Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune, na akampa Hebroni kama urithi wake. 1414:14 Hes 14:24Hivyo Hebroni imekuwa mali ya Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote. 1514:15 Mwa 23:2; Yos 15:13; 11:23; Amu 3:11; 1Fal 4:24; 5:4; 1Nya 22:9(Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kutokana na huyo Arba ambaye alikuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.)

Kisha nchi ikawa na amani bila vita.