Orodha Ya Wafalme Walioshindwa
112:1 Za 136:21; Hes 32:19; 21:13; Kum 3:8; Yos 11:2Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
212:2 Yos 12:5; Hes 21:21-25; Yos 13:10; Amu 11:19; Hes 32:34; Yos 13:16; Mwa 19:38; 31:21; 32:22; Hes 32:26; Kum 2:36; 3:15; Yos 13:11, 25; 17:1; 20:8; 21:38; Amu 5:17; 7:3; 10:8Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 312:3 Yos 11:2; Mwa 14:3; Hes 33:49; Yos 13:20; Hes 21:20Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi12:3 Yaani Bahari ya Galilaya. hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi12:3 Yaani Bahari Mfu.), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
412:4 Hes 21:21; 33; Yos 13:30; Mwa 14:5; Kum 1:4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
512:5 Kum 3:10; Hes 32:33; Yos 17:1; 20:8; 21:27; 22:7; 13:2, 13; 1Sam 27:8; Kum 3:14Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
612:6 Kum 3:8; Hes 32:29-33; Yos 13:8Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
712:7 Yos 11:17Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: 812:8 Ezr 9:1; Kum 1:7; Yos 3:10; 11:17nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.