Yoshua 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 11:1-23

Wafalme Wa Kaskazini Washindwa

111:1 Amu 4:2, 7, 23; Za 83:9; Yos 12:19; 15:23-25; 19:36; 1Sam 12:9; 1Fal 9:15; 2Fal 15:29; Neh 11:33; Yer 49:28, 33; Yos 12:20; 19:25Ikawa Yabini mfalme wa Hazori aliposikia habari za mambo haya, akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na kwa mfalme wa Akishafu, 211:2 Yos 12:1; 18:18; Hes 34:11; Kum 3:17; Yos 19:35; 1Fal 15:20; Yos 12:23; 17:11; Amu 1:27; 1Fal 4:11; 1Nya 7:29na pia kwa wafalme wa upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani, katika Araba upande wa kusini mwa Kinerethi, kwenye shefela, upande wa magharibi na katika miinuko ya Nafoth-Dori upande wa magharibi; 311:3 Yos 3:10; Hes 13:17; Kut 3:8; Kum 7:1; Amu 3:3-5; 1Fal 9:20; Kum 3:8; Mwa 31:49; Yos 15:38; 18:26; Amu 11:11; 20:1; 21:1; 1Sam 7:5-6; 1Fal 15:22; 2Fal 25:23kwa Wakanaani upande wa mashariki na magharibi; kwa Waamori, Wahiti, Waperizi na Wayebusi katika nchi ya vilima; na kwa Wahivi chini ya Hermoni katika eneo ya Mispa. 411:4 Mwa 12:2; Amu 7:12; 1Sam 13:5; Mwa 22:17; 32:12Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu kubwa ya farasi na magari ya kuvutwa na farasi, jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari. 511:5 Amu 5:19Wafalme hawa wote wakaunganisha majeshi yao na kupiga kambi pamoja kwenye Maji ya Meromu, ili kupigana dhidi ya Israeli.

611:6 Yos 2:24; Mwa 49:6Bwana akamwambia Yoshua, “Usiwaogope, kwa sababu kesho saa kama hii nitawatia wote mikononi mwa Israeli, wakiwa wameuawa. Utakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuyachoma moto magari yao ya vita.”

7Hivyo Yoshua pamoja na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula kwenye Maji ya Meromu kuwashambulia, 811:8 Mwa 10:15; Amu 18:7; Yos 13:6naye Bwana akawatia mikononi mwa Israeli. Wakawashinda na kuwafukuza hadi Sidoni Kuu na kuwafikisha Misrefoth-Maimu, hadi Bonde la Mispa upande wa mashariki, hadi pakawa hakuna yeyote aliyebaki. 9Yoshua akawatendea kama Bwana alivyoamuru. Akakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuchoma moto magari yao ya vita.

1011:10 Isa 3:25; Yer 41:2; 44:18Wakati huo Yoshua akarudi na kuuteka mji wa Hazori na kumuua mfalme wake kwa upanga. (Hazori ulikuwa mji mkuu wa falme hizo zote.) 1111:11 Kum 7:2; 20:16-17; Hes 31:10Kila aliyekuwa ndani yake wakamuua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza chochote chenye pumzi na akauchoma Hazori kwenyewe kwa moto.

1211:12 Hes 33:50-52; Kum 7:2Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake na kuwapiga kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, jinsi Mose mtumishi wa Bwana alivyowaagiza. 13Lakini Israeli hawakuichoma moto hata mojawapo ya miji iliyojengwa katika vilima vyao vidogo isipokuwa mji wa Hazori ambao Yoshua aliuchoma moto. 1411:14 Kum 20:16; Mwa 22:17; 32:12Waisraeli wakajichukulia nyara zote na mifugo yote ya miji hii, bali waliwaua watu wote kwa upanga hadi walipowaangamiza kabisa, pasipo kumbakiza yeyote mwenye pumzi. 1511:15 Kut 34:11; Kum 7:2; Yos 1:7Kama vile Bwana alivyomwagiza Mose mtumishi wake, vivyo hivyo Mose alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya kama vivyo, hakukosa kufanya lolote katika yale yote Bwana aliyomwagiza Mose.

1611:16 Hes 13:17; Kum 1:7; Yos 10:41Yoshua akaiteka nchi hii yote: nchi ya vilima, Negebu yote, eneo yote ya Gosheni, shefela ya upande wa magharibi, Araba na milima ya Israeli pamoja na shefela zao, 1711:17 Mwa 14:6; Hes 24:18; Kum 33:2; Yos 13:5; Kum 3:25; Yos 12:7-8; Kum 3:9; 7:24kuanzia Mlima Halaki ambao umeinuka kuelekea Seiri hadi Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni chini ya Mlima Hermoni. Akawateka wafalme wake wote, akawapiga na kuwaua. 18Yoshua akapigana vita dhidi ya wafalme hawa wote kwa muda mrefu. 1911:19 Yos 9:1-3; 9:15Hakuna mji wowote katika eneo hili uliofanya mkataba wa amani na Israeli, isipokuwa hao Wahivi wa Gibeoni. Wengine wote walishindwa katika vita. 2011:20 Kut 4:21; Rum 9:18; Kut 14:17; Kum 7:16; Amu 14:4; Kum 2:30; 1Sam 2:25; 1Fal 12:15; 22:20-23; Yak 1:13-17; Kum 20:16Kwa maana Bwana mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili apate kuwafutilia mbali pasipo huruma, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

2111:21 Hes 13:22, 33; Yos 10:3; 15:50; Kum 9:2; Amu 1:10; Yer 3:23Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka nchi yote ya vilima ya Yuda na kutoka nchi yote ya vilima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. 2211:22 Mwa 10:19; Yos 12:17; 19:13; 1Sam 5:8; 17:4; 1Fal 2:39; 2Fal 14:25; 1Nya 8:13; Amo 6:2; Yos 15:47; 1Sam 5:1; Isa 20:1Hawakubaki Waanaki wowote katika nchi ya Israeli, ila tu katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi. 2311:23 Yos 21:43-45; Neh 9:24; Kum 1:38; 12:9-10; 25:19; Yos 13:7; Hes 26:53; Za 105:44; Kut 33:14; Yos 14:15Hivyo Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kulingana na walivyogawanyika katika kabila zao.

Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.