Yoshua 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoshua 1:1-18

Bwana Anamwagiza Yoshua

11:1 Kut 14:31; Kum 34:5; Ufu 15:3; Kut 17:9; 24:13; Hes 32:20; Yos 22:2-4Baada ya kifo cha Mose mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Mose: 21:2 Hes 13:29; 35:10; Mwa 15:14; 12:7; Kum 1:24-25“Mtumishi wangu Mose amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli. 31:3 Kum 11:24; Mwa 50:24; Hes 13:2; Kum 1:8Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Mose. 41:4 Kum 3:25; Mwa 2:14; 10:15; 23:10; Kut 3:8; Hes 34:2-12; Ezr 4:20Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa1:4 Yaani Bahari ya Mediterania. iliyoko upande wa magharibi. 51:5 Kum 7:24; Mwa 26:3; 39:2; Amu 6:12; 1Sam 10:7; Yer 1:8; 30:11; Mwa 28:1; Kum 4:31Hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.

61:6 2Sam 2:7; 1Fal 2:2; Isa 41:6; Yoe 3:9-10; Kum 1:21; 31:6; Amu 5:21; Yer 3:18; 7:7“Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa. 71:7 Kum 29:9; 1Fal 2:3; 3:3; Ezr 7:26; Za 78:10; 119:136; Isa 42:24; Yer 26:4-6; 32:23; 44:10; Hes 12:7; Ay 42:7; Kum 5:32; Yos 23:6; Kum 4:2; 5:33; 11:8; Yos 11:15Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Mose mtumishi wangu, usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote uendako. 81:8 Kum 28:61; Za 147:19; Kut 4:15; Isa 59:21; Mwa 24:63; Kum 29:9; 1Sam 18:14; Isa 52:13; 53:10; Yer 23:5Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi. 91:9 Kum 31:6; Yos 10:8; 2Fal 19:6; Isa 34:5; 37:6; Kum 1:21; Ay 4:5; Kum 31:8; Yer 1:8Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako.”

101:10 Kum 1:15Ndipo Yoshua akawaagiza maafisa wa watu akisema, 111:11 Yos 3:2; 1Sam 17:22; Isa 10:28; Mwa 40:13; Hes 35:10; 33:53“Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Wekeni tayari mahitaji yenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka hii Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa iwe yenu wenyewe.’ ”

121:12 Hes 32:33Lakini kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, Yoshua akasema, 131:13 Kut 33:14; Za 55:6; Isa 11:10; 28:12; 30:15; 32:18; 40:31; Yer 6:16; 45:3“Kumbukeni agizo lile Mose mtumishi wa Bwana alilowapa: ‘Bwana Mungu wenu anawapa ninyi raha, naye amewapa nchi hii.’ 141:14 Kum 3:19; Hes 32:26; Kut 13:18; Yos 4:12Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Mose aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi 151:15 Hes 32:20-22; Yos 22:1-4Bwana awape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile Bwana Mungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Mose mtumishi wa Bwana aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.”

161:16 Hes 27:20; 32:25Ndipo wakamjibu Yoshua, “Chochote ambacho umetuagiza tutafanya na popote utakapotutuma tutakwenda. 171:17 Hes 32:25; Kum 1:21; 31:6; Mwa 21:22; 26:24, 28; 1Sam 16:18; 20:13; 1Fal 1:37; Za 20:1-4, 9; Rum 8:31Kama vile tulivyomtii Mose kikamilifu, ndivyo tutakavyokutii wewe. Bwana Mungu wako na awe pamoja nawe tu kama vile alivyokuwa pamoja na Mose. 18Yeyote atakayeasi neno lako na kuacha kuyatii maneno yako, au chochote utakachowaamuru, atauawa. Uwe imara na hodari tu!”