Yona 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yona 2:1-10

Maombi Ya Yona Katika Tumbo La Nyangumi

1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake. 22:2 Za 18:6; 120:1; 86:13; Mao 3:55Akasema:

“Katika shida yangu nalimwita Bwana,

naye akanijibu.

Kutoka kina cha kaburi2:2 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. niliomba msaada,

nawe ukasikiliza kilio changu.

32:3 Za 88:6; 42:7; 2Sam 22:5Ulinitupa kwenye kilindi,

ndani kabisa ya moyo wa bahari,

mikondo ya maji ilinizunguka,

mawimbi yako yote na viwimbi

vilipita juu yangu.

42:4 Za 31:22; Yer 7:15; Isa 49:14; 1Fal 8:38, 48Nikasema, ‘Nimefukuziwa

mbali na uso wako,

hata hivyo nitatazama tena

kuelekea Hekalu lako takatifu.’

52:5 Za 69:1-2Maji yaliyonimeza yalinitisha,

kilindi kilinizunguka;

mwani2:5 Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari. ulijisokota kichwani pangu.

62:6 Ay 28:9; 17:16; 33:18; Za 30:3Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,

makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.

Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,

Ee Bwana Mungu wangu.

72:7 Za 11:4; 18:6; 77:11-12; 34:6; 130:2; Yer 2:13; 2Nya 30:27“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,

nilikukumbuka wewe, Bwana,

nayo maombi yangu yalikufikia wewe,

katika Hekalu lako takatifu.

82:8 1Sam 12:21; Yer 10:8; 2Fal 17:15; Za 31:6; Kum 32:21“Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa

hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.

92:9 Hos 14:2; Ebr 13:15; Hes 30:2; Kut 15:2; Za 50:14; 116:14; 66:13-15; 3:8; 42:4Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

nitakutolea dhabihu.

Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

Wokovu watoka kwa Bwana.”

102:10 Yn 1:17; Mt 8:9Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.