Yona 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yona 1:1-17

Yona Anamkimbia Bwana

11:1 Mt 16:4; 12:39-41; 2Fal 14:25; Lk 11:29-32Neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amitai: 21:2 Mwa 10:11; 18:20; Yon 3:3; Nah 2:8; Mt 12:41; Ezr 9:6; Yak 5:4“Nenda katika mji mkubwa wa Ninawi ukahubiri juu yake, kwa sababu uovu wake umekuja juu mbele zangu.”

31:3 Za 139:7; Yos 19:46; Mdo 9:36-43; Mwa 4:16; 10:4; Kut 4:13; Isa 23:1; Yer 20:9Lakini Yona alimkimbia Bwana na kuelekea Tarshishi. Alishuka mpaka Yafa, ambapo alikuta meli iliyokuwa imepangwa kuelekea bandari ile. Baada ya kulipa nauli, akapanda melini na kuelekea Tarshishi ili kumkimbia Bwana. 41:4 Za 107:23-26Ndipo Bwana akatuma upepo mkali baharini, nayo dhoruba kali sana ikavuma hata meli ikawa hatarini kuvunjika. 51:5 Mdo 27:18-19Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.

Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito. 61:6 Yon 3:8; Mt 8:25; Za 78:34; 107:28Nahodha akamwendea na kusema, “Wewe unawezaje kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda akatuangalia, tusiangamie.”

71:7 Yos 7:10-18; Hes 32:23; Mit 16:33; Mdo 1:26; 1Sam 10:20; 14:43Kisha mabaharia wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tupige kura tumtafute anayehusika na maafa haya.” Wakapiga kura, kura ikamwangukia Yona.

81:8 Yos 7:19Kwa hiyo walimuuliza, “Tuambie, ni nani anayehusika kwa kutuletea tatizo hili lote? Unafanya kazi gani? Umetoka wapi? Nchi yako ni ipi? Wewe ni kutoka taifa lipi?”

91:9 Dan 2:18; Mdo 17:24; Za 146:6; 96:9; Neh 9:6Akajibu, “Mimi ni Mwebrania, nami namwabudu Bwana, Mungu wa Mbinguni, aliyeumba bahari na nchi kavu.”

10Hili liliwaogopesha nao wakamuuliza,

“Umefanya nini?” (Walijua alikuwa anamkimbia Bwana, kwa sababu alishawaambia hivyo.)

11Bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Kwa hiyo walimuuliza, “Tukutendee nini ili kufanya bahari itulie kwa ajili yetu?”

121:12 Mhu 9:18; 2Sam 24:17; 1Nya 21:17Akawajibu, “Niinueni mnitupe baharini, nayo itakuwa shwari. Ninajua mawimbi haya makubwa yamewatokea kwa ajili ya kosa langu.”

131:13 Mit 21:30Badala yake, wale watu walijitahidi kupiga makasia wawezavyo ili wapate kurudi pwani. Lakini hawakuweza, kwa kuwa bahari ilizidi kuchafuka kuliko mwanzo. 141:14 Kum 21:8; Za 115:3; Dan 4:35Ndipo wakamlilia Bwana, “Ee Bwana, tafadhali usituue kwa kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umefanya kama ilivyokupendeza.” 151:15 Za 107:29; Lk 8:24Kisha walimchukua Yona, wakamtupa baharini nayo bahari iliyokuwa imechafuka ikatulia. 161:16 Mk 4:41; Hes 30:2; Za 66:13-14Katika jambo hili watu wakamwogopa Bwana sana, wakamtolea Bwana dhabihu na kumwekea nadhiri.

171:17 Mt 12:40; 16:4; Lk 11:30; Yn 4:6-7Lakini Bwana akamwandaa nyangumi1:17 Yaani samaki mkubwa sana. kummeza Yona, naye Yona alikuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu, usiku na mchana.