Yohana 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 9:1-41

Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu

19:1 Mdo 3:2; 14:8Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 29:2 Lk 13:2; Mdo 28:4; Eze 18:20; Kut 20:5; Ay 21:19Wanafunzi wake wakamuuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?”

39:3 Yn 11:14Yesu akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. 49:4 Yn 1:9; 12:35Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. 59:5 Yn 8:12Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.”

69:6 Mk 7:33; 8:23Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. 79:7 2Fal 5:10; Lk 13:4; Isa 35:5; Yn 11:37Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.

89:8 Mdo 3:2-10Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, “Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?” 9Wengine wakasema, “Ndiye.”

Wengine wakasema, “Siye, bali wamefanana.”

Lakini yeye akawaambia, “Mimi ndiye.”

10Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?”

119:11 Yn 9:6, 7Yeye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu, ndipo nikanawa nami nikapata kuona!”

12Wale wakamuuliza, “Yeye huyo mtu yuko wapi?”

Akawajibu, “Sijui.”

Mafarisayo Wachunguza Kuponywa Kwa Kipofu

13Wakamleta kwa Mafarisayo yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali. 149:14 Mt 12:1-14; Yn 5:9Basi siku hiyo Yesu alipotengeneza tope na kuyafungua macho ya huyo mtu ilikuwa Sabato. 15Mafarisayo nao wakaanza kumuuliza alivyopata kuponywa. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho yangu, nikanawa na sasa ninaona.”

169:16 Mt 12:2; Yn 7:43; 10:19Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.”

Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika.

179:17 Mt 21:11; Yn 4:19Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho, wasemaje kuhusu mtu huyo?” Maana macho yako ndiyo yaliyofumbuliwa.

Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.”

189:18 Yn 1:19Wale Wayahudi hawakuamini ya kuwa mtu huyo alikuwa kipofu, akapata kuona, mpaka walipowaita wazazi wake. 19Wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu, ambaye mnasema alizaliwa kipofu? Imekuwaje basi sasa anaona?”

20Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu na ya kuwa alizaliwa kipofu. 21Lakini sisi hatujui ni kwa jinsi gani kwamba sasa anaona, wala hatujui ni nani aliyemfungua macho yake. Muulizeni, yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.” 229:22 Yn 7:13; Lk 6:22; Yn 16:2; 12:42Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Yesu kuwa ndiye Kristo9:22 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. atafukuzwa kutoka sinagogi. 239:23 Yn 9:21Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.”

249:24 Yos 7:19Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”

25Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.”

26Wakamuuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?”

279:27 Yn 9:15Akawajibu, “Tayari nimekwisha kuwaambia, nanyi hamtaki kunisikiliza. Mbona mnataka kusikia tena? Je, ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?”

289:28 Yn 5:45Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ndiwe mwanafunzi wake, Sisi ni wanafunzi wa Mose. 299:29 Yn 8:14Tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini kwa habari ya mtu huyu hatujui atokako.”

309:30 Yn 3:10Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu! 319:31 Za 66:18; Yak 5:16-18Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii. 32Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu. 339:33 Yn 3:2Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya lolote.”

349:34 Isa 66:5Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.

Upofu Wa Kiroho

359:35 Mt 14:33; 16:16; Mk 1:1; 1Yn 5:13Yesu aliposikia kuwa wamemfukuzia nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”

369:36 Rum 10:14Yule mtu akamjibu, “Yeye ni nani, Bwana? Niambie ili nipate kumwamini.”

379:37 Yn 4:26Yesu akamjibu, “Umekwisha kumwona, naye anayezungumza nawe, ndiye.”

389:38 Mt 28:9Yule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu.

399:39 Yn 5:22; 3:19; 12:47; Lk 4:18; Mt 13:13Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.”

409:40 Rum 2:19Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa karibu naye wakamsikia na kumwambia, “Je, kweli sisi ni vipofu?”

419:41 Yn 15:22-24Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, msingekuwa na hatia ya dhambi, lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi mna hatia.