Yohana 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 5:1-47

Yesu Amponya Mtu Kwenye Bwawa La Bethzatha

15:1 Law 23:2; Kum 16:1; Yn 2:13Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu. 25:2 Neh 3:1; 12:39; Mdo 21:40; 26:14Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha,5:2 Bethzatha ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni Nyumba ya mizeituni; mahali pengine limetajwa kama Bethesda kwa Kiaramu, yaani Nyumba ya huruma, na pengine kama Bethsaida, yaani Nyumba ya uvuvi. ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano. 3Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe. 4Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao]. 5Mtu mmoja alikuwako huko ambaye alikuwa ameugua kwa miaka thelathini na minane. 6Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwa hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”

7Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.”

85:8 Mk 2:11; Lk 5:24Yesu akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.” 95:9 Mt 12:1-14; Yn 9:14Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea.

Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato. 105:10 Yer 17:21; Mt 12:2Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.”

11Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ”

125:12 Lk 5:21Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”

13Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo.

145:14 Mk 2:5; Yn 8:11; 8:11Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.” 155:15 Yn 1:19Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.

Uzima Kupitia Mwana

165:16 Mt 12:14Kwa hiyo Wayahudi wakaanza kumsumbua Yesu, kwa sababu alikuwa anafanya mambo kama hayo siku ya Sabato. 175:17 Yn 9:4; 14:10Yesu akawajibu, “Baba yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya kazi.” 185:18 Mt 12:14; Yn 10:30-33; 19:7Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumuua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.

Mamlaka Ya Mwana Wa Mungu

195:19 Yn 8:28; 14:24Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake, yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo. 205:20 Yn 3:35; 14:12Baba ampenda Mwana na kumwonyesha yale ambayo yeye Baba mwenyewe anayafanya, naye atamwonyesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa. 215:21 2Kor 1:9; Ebr 11:19; Yn 11:25Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda. 225:22 Amu 11:27; Mdo 10:42Wala Baba hamhukumu mtu yeyote, lakini hukumu yote amempa Mwana, 235:23 Lk 10:16; 1Yn 2:23ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Yeyote asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyemtuma.

245:24 Yn 3:18; 1Yn 3:14“Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani. 255:25 Yn 16:32; 8:43-47Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai. 265:26 Yn 12:14Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake. 275:27 Mdo 10:42; 17:31Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.

285:28 Yn 16:2“Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake. 295:29 Dan 12:2; Mt 25:46Nao watatoka nje, wale waliotenda mema watafufuka wapate uzima na wale waliotenda maovu, watafufuka wahukumiwe.

Shuhuda Kuhusu Yesu

305:30 Isa 28:6; Mt 26:39; Yn 4:34“Mimi siwezi kufanya jambo lolote peke yangu. Ninavyosikia ndivyo ninavyohukumu, nayo hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake yeye aliyenituma.

315:31 Yn 8:14“Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. 325:32 Yn 5:37; 8:18Lakini yuko mwingine anishuhudiaye na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli.

335:33 Yn 1:7“Mlituma wajumbe kwa Yohana, naye akashuhudia juu ya kweli. 345:34 1Yn 5:9Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa. 355:35 Dan 12:3Yohana alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake.

365:36 1Yn 5:9; Yn 14:11; 15:24; 3:17; 10:25“Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma. 375:37 Yn 8:18; Kum 4:12; 1Tim 1:17Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake, 385:38 1Yn 1:10; 2:4; Isa 26:10; Yn 3:17wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye. 395:39 Rum 2:17-18; Lk 24:27, 44; Mdo 13:27Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi. 405:40 Yn 6:44Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.

415:41 Yn 5:44; 5:34; 1The 2:6“Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu. 42Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. 43Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. 445:44 Rum 2:29Ninyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu?

455:45 Yn 9:28; Rum 2:17“Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba, mshtaki wenu ni Mose, ambaye mmemwekea tumaini lenu. 465:46 Mwa 3:15; Lk 24:27, 44Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu. 475:47 Lk 16:29-31Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?”