Yohana 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 4:1-54

Yesu Azungumza Na Mwanamke Msamaria

14:1 Yn 3:22-26Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana, 24:2 1Kor 1:17ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. 34:3 Yn 3:22Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya.

44:4 Lk 9:52Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria. 54:5 Mwa 48:22; Yos 24:32Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu. 6Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

74:7 Mwa 24:17; 1Fal 17:10Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.” 84:8 Yn 4:5, 30(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)

94:9 Mt 10:5; Lk 9:52-53Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)

104:10 Isa 55:1; Ufu 21:6Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”

11Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi? 124:12 Yn 4:6; 8:53Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

134:13 Yn 6:58Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 144:14 Yn 6:35; Isa 12:3; Yn 7:38; Mt 25:46Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.”

154:15 Yn 6:34Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuteka maji!”

16Yesu akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.”

17Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.”

Yesu akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume. 18Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli.”

194:19 Mt 21:11Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 204:20 Kum 11:29; Yos 8:33; Lk 9:53; 4:21; 4:20; Yn 5:28; 16:2; 1Tim 2:8Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

214:21 Yn 5:28; 16:2; Mal 1:11; 1Tim 2:8Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 224:22 2Fal 17:28-41; Isa 2:3; Rum 9:4-5Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 234:23 Yn 5:25; 16:32; Flp 3:3Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. 244:24 Flp 3:3Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

254:25 Mt 1:16; Yn 1:41Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

264:26 Yn 8:24; 9:35-37Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”

274:27 Yn 4:8Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”

28Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu, 294:29 Mt 12:23; Yn 7:26, 31“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”4:29 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. 30Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.

314:31 Mt 23:7Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau chochote.”

324:32 Ay 23:12; Mt 4:4Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”

33Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 344:34 Mt 26:39; Yn 17:4; 19:30Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake. 354:35 Mt 9:37; Lk 10:2Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! 364:36 Rum 1:13; Mt 25:46Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja. 374:37 Ay 31:8; Mik 6:15Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”

Wasamaria Wengi Waamini

394:39 Yn 4:29Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.” 40Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. 41Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini.

424:42 Lk 2:11; 1Yn 4:14Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi wa ulimwengu.”

Yesu Amponya Mwana Wa Afisa

43Baada ya zile siku mbili, Yesu aliondoka kwenda Galilaya. 444:44 Mt 13:57; Lk 4:24(Basi Yesu mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.) 454:45 Yn 2:23Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu.

464:46 Yn 21:1-11Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwepo na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. 474:47 Yn 4:3, 54; Lk 7:2Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.

484:48 Dan 4:2-3; Ebr 2:4Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”

49Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.”

50Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.”

Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake. 51Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. 52Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.”

534:53 Mdo 11:14Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu.

544:54 Yn 4:8; 2:11Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Uyahudi.