Yohana 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 17:1-26

Yesu Ajiombea Mwenyewe

117:1 Yn 11:41; 12:23; 13:31, 32Baada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema:

“Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. 217:2 Dan 7:14; Yn 6:37, 39Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. 317:3 Flp 3:8; Yn 17:8, 18, 21, 23, 25; 3:17Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. 417:4 Yn 13:31; 19:30Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. 517:5 Flp 2:6; Yn 1:2Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwepo.

Yesu Awaombea Wanafunzi Wake

617:6 Yn 17:26; 1:18“Nimelidhihirisha jina lako kwa wale ulionipa kutoka ulimwengu. Walikuwa wako, nawe ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako. 7Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako, 817:8 Yn 8:26; 1:18kwa kuwa maneno yale ulionipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma. 917:9 Lk 22:32Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. 1017:10 Yn 16:15Wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. 1117:11 Yn 13:1; 17:13; 7:33; 17:21-23; Za 133:1; Yn 10:30Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. 1217:12 Yn 6:39; 6:70Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.

1317:13 Yn 3:29“Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao. 1417:14 Yn 15:19; 8:23; 1Yn 3:13; Yn 17:16Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu. 1517:15 Mt 5:37Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. 1617:16 Yn 17:14Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu. 1717:17 2Sam 7:28; Yn 15:3; 1Fal 17:24Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli. 1817:18 Yn 17:3, 8, 21, 23, 25; 20:21Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. 1917:19 Yn 17:17; 1Kor 1:2, 30; 1The 4:7; Ebr 10:10Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli.

Yesu Awaombea Wote Wamwaminio

2017:20 Yn 17:9“Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao 2117:21 Gal 3:28; Rum 12:5; Yn 10:38; 14:11ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiye uliyenituma mimi. 2217:22 Yn 14:20; 1Yn 1:2; 3:24Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. 2317:23 Yn 3:17; 16:27; Kol 3:14Mimi ndani yako na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi.

2417:24 Yn 12:26; 1:14; Mt 25:34; Yn 1:2“Baba, shauku yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

2517:25 Yn 15:21; 16:3; 3:17; 7:29“Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma. 26Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili kwamba upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”