Yohana 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 11:1-57

Kifo Cha Lazaro

111:1 Mt 21:17; Lk 10:38Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake. 211:2 Mk 14:3; Lk 7:38Huyu Maria, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye yule ambaye alimpaka Bwana mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake. 311:3 Yn 11:5, 36Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.”

411:4 Yn 11:40Lakini Yesu aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.” 5Pamoja na hivyo, ingawa Yesu aliwapenda Martha, Maria na Lazaro ndugu yao, 611:6 Yn 10:40baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi.

711:7 Yn 10:40Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Haya, turudi Uyahudi.”

811:8 Mt 23:7; Yn 8:59; 10:31Wanafunzi wake wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?”

911:9 Yn 9:4; 12:35Yesu akawajibu, “Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wala watembeao mchana hawawezi kujikwaa kwa maana wanaona nuru ya ulimwengu huu. 1011:10 Yn 12:35Lakini wale watembeao usiku hujikwaa kwa sababu hakuna nuru ndani yao.”

1111:11 Mt 9:24; Lk 8:52Baada ya kusema haya, Yesu akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.”

12Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala usingizi ataamka.” 1311:13 Mt 9:24Hata hivyo, Yesu alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.

14Kwa hiyo Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa. 15Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwepo huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.”

1611:16 Mt 10:3; Mdo 1:13Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.”

Yesu Ndiye Ufufuo Na Uzima

1711:17 Yn 11:6, 39Yesu alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne. 1811:18 Yn 11:1; Mt 21:17Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili,11:18 Maili mbili ni kama kilomita tatu. 1911:19 Yn 11:31; Ay 2:11na Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao. 2011:20 Lk 10:38-42Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani.

2111:21 Yn 11:32, 37Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa. 2211:22 Yn 11:41, 42Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”

23Yesu akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.”

2411:24 Dan 12:2; Mdo 24:15Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.”

2511:25 Yn 1:4Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi 2611:26 Yn 3:15; Mt 25:46na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?”

2711:27 Lk 2:11; Mt 4:3; 16:16; Yn 6:14Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo,11:27 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.”

Yesu Alia

2811:28 Mt 26:18; Yn 13:13Baada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.” 29Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu. 3011:30 Yn 11:20; 13:13Yesu alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha. 3111:31 Yn 11:19; 8:59Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.

3211:32 Yn 11:21; 5:18Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa, alipiga magoti miguuni Pake na kusema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.”

3311:33 Yn 11:38; 12:27; 13:21Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana. 34Akauliza, “Mmemweka wapi?”

Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.”

3511:35 Lk 19:41Yesu akalia machozi.

3611:36 Yn 11:3Ndipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!”

3711:37 Yn 9:6, 7; 11:21, 32Lakini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”

Yesu Amfufua Lazaro

3811:38 Yn 11:33; Mt 27:60; Lk 24:2; Yn 20:1Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake. 3911:39 Yn 11:17Yesu akasema, “Liondoeni hilo jiwe.”

Martha ndugu yake yule aliyekuwa amekufa akasema, “Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne.”

4011:40 Yn 11:23-25Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”

4111:41 Yn 17:1; Mt 11:25Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka kaburini. Yesu akainua macho yake juu akasema, “Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. 4211:42 Yn 12:30; 3:17Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.”

4311:43 Lk 7:14Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti yake akaita, “Lazaro, njoo huku!” 4411:44 Yn 19:40; 20:7Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake.

Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”

Shauri La Kumuua Yesu

(Mathayo 26:1-5; Marko 14:1-2; Luka 22:1-2)

4511:45 Yn 11:19; 2:23; 14Hivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Maria, walipoona yale Yesu aliyoyatenda wakamwamini. 46Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo Yesu aliyoyafanya. 4711:47 Yn 2:11Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza.

Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.”

4911:49 Lk 3:2; Yn 18:14; Mdo 4:6Mmoja wao aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, akasema, “Ninyi hamjui kitu chochote! 5011:50 Yn 18:14Hamjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?”

5111:51 Mwa 50:20; Kut 28:30; Hes 27:21Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angelikufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi, 5211:52 Isa 49:6; Yn 10:16wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 5311:53 Mt 12:14Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Yesu.

5411:54 Yn 7:1Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake.

5511:55 Kut 12:13, 23, 27; Mk 14:1; 2Nya 30:17-18Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajitakase. 5611:56 Yn 7:11; 17:7Watu wakawa wanamtafuta Yesu, nao waliposimama kwenye eneo la Hekalu waliulizana, Je, mtu huyu hatakuja kamwe kwenye Sikukuu? 57Viongozi wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa yeyote atakayejua mahali Yesu aliko, lazima atoe taarifa ili wapate kumkamata.