Yohana 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 10:1-42

Mchungaji Mwema

110:1 Yn 10:8, 10“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwizi na mnyangʼanyi. 210:2 Mk 6:34; Yn 10:11, 14Yeye anayeingia kwa kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. 310:3 Yn 10:4, 5, 14Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 410:4 Yn 10:3Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake. 510:5 Yn 10:27Lakini kondoo hawatamfuata mgeni bali watamkimbia, kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.” 610:6 Yn 16:25; 16:25Yesu alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia.

710:7 Za 118:20; Yn 14:6; Mt 7:13; 14Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo. 810:8 Yer 23:1-2; Eze 34:2Wote walionitangulia ni wevi na wanyangʼanyi, lakini kondoo hawakuwasikia. 910:9 Za 118:20; Yn 14:6; 1Kor 3:15Mimi ndimi lango, yeyote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 1010:10 Yn 1:4; 3:15, 16; 5:40; 20:31; Za 65:11; Rum 5:17Mwizi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.

1110:11 Za 23:1; Mt 2:6; Yn 15:13; 1Yn 3:16“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 1210:12 Zek 11:16-17Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Amwonapo mbwa mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. 13Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo.

1410:14 Kut 33:12; 2Tim 2:19“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua. 1510:15 Mt 11:27; Yn 15:16Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 1610:16 Isa 56:8; Mdo 10:34-35; Yn 17:20-21; Efe 2:11-19; Eze 34:23; 1Pet 2:25Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 1710:17 Isa 53:7, 8, 12; Ebr 2:9Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 1810:18 Mt 26:53; Flp 2:8; Ebr 5:8Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”

1910:19 Yn 6:52Kwa maneno haya Wayahudi waligawanyika. 2010:20 Mk 3:22; Yn 7:20; 2Fal 9:11Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.”

2110:21 Mt 4:24; Kut 4:11; Yn 9:32-33Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?”

Yesu Akataliwa Na Wayahudi

22Wakati huo ilikuwa Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu10:22 Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu ni Hanukkah kwa Kiebrania. huko Yerusalemu, nao ulikuwa wakati wa majira ya baridi. 2310:23 Mdo 3:11; 5:12Naye Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Solomoni. 2410:24 Yn 1:19; Lk 22:67Wayahudi wakamkusanyikia wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo10:24 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. tuambie waziwazi.”

2510:25 Yn 4:26; 4:11Yesu akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia. 2610:26 Yn 8:47Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 2710:27 Yn 10:4, 14Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata, 2810:28 Yn 6:39nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. 2910:29 Yn 17:2, 6, 24; 14:28Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. 3010:30 Kum 6:4; Yn 17:21-24Mimi na Baba yangu tu umoja.”

3110:31 Yn 8:59Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, 32lakini Yesu akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?”

3310:33 Law 24:16; Mt 26:63-66Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.”

3410:34 Rum 3:19; 1Kor 14:21; Za 82:6Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Sheria ya kwamba, ‘Nimesema kuwa, ninyi ni miungu?’ 3510:35 Rum 13:1; Mt 5:17, 18Kama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka, 3610:36 Yer 1:5; Yn 6:69; 3:17je, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ 3710:37 Yn 15:24Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini, 3810:38 Yn 14:10-11; 20:17-21lakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ndani yake.” 3910:39 Yn 7:30; Lk 4:30; Yn 8:59Ndipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao.

4010:40 Yn 1:28Akaenda tena ngʼambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yohana alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. 4110:41 Yn 2:1; 1:26-34Watu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yohana hakufanya muujiza wowote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 4210:42 Yn 7:31Nao wengi wakamwamini Yesu huko.