Yoeli 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yoeli 3:1-21

Mataifa Yahukumiwa

13:1 Kum 30:3; Yer 16:15; 40:5; Eze 3:20; 38:8“Katika siku hizo na wakati huo,

nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu,

23:2 Zek 14:2; Isa 13:9; 2Nya 20:26; Isa 66:16; Yer 2:35; Sef 3:8; Mwa 11:4; Law 26:33nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta

katika Bonde la Yehoshafati3:2 Yehoshafati maana yake Bwana huhukumu.

Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao

kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli,

kwa kuwa waliwatawanya watu wangu

miongoni mwa mataifa

na kuigawa nchi yangu.

33:3 Oba 1:11; Amo 2:6; Ay 6:27; Eze 24:6Wanawapigia kura watu wangu

na kuwauza wavulana ili kupata makahaba;

waliwauza wasichana

ili wapate kunywa mvinyo.

43:4 Mwa 10:15; Mt 11:21; Yak 2:13; Lk 18:7; Amo 1:6-9; Isa 14:29-31; 34:8; Za 87:4; Eze 25:15-17“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda. 53:5 1Fal 15:18; 2Nya 21:16-17Kwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu. 63:6 Eze 27:13; Zek 9:13Mliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kwamba mpate kuwapeleka mbali na nchi yao.

73:7 Isa 43:5-6; 66:6; Yer 23:8“Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya. 83:8 Eze 23:42; Isa 14:2; 60:14; Mwa 10:7; Yer 30:16; 2Nya 9:1Nitawauza wana wenu na binti zenu kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Waseba, taifa lililo mbali.” Bwana amesema.

93:9 Isa 8:9; Yer 46:4Tangazeni hili miongoni mwa mataifa:

Jiandaeni kwa vita!

Amsha askari!

Wanaume wote wapiganaji

wasogee karibu na kushambulia.

103:10 Zek 12:8; Isa 2:4; Mik 4:3; Hes 25:7Majembe yenu yafueni yawe panga

na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki.

Aliye dhaifu na aseme,

“Mimi nina nguvu!”

113:11 Eze 38:15-16; Sef 3:8; Isa 13:3Njooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote,

kusanyikeni huko.

Shusha wapiganaji wako, Ee Bwana!

123:12 Za 96:13; 82:1; 2Nya 20:26; Isa 2:4“Mataifa na yaamshwe;

na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati,

kwa kuwa nitaketi mahali pale

kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.

133:13 Isa 17:5; Ufu 14:15-20; Amu 6:11; Mt 13:39; Mk 4:29; Yer 51:33; Hos 6:11Tia mundu,

kwa kuwa mavuno yamekomaa.

Njooni, mkanyage zabibu,

kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa

na mapipa yanafurika:

kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”

143:14 Isa 2:4; 13:4; 34:2-8; Sef 1:7; Yoe 1:15; Eze 36:5Umati mkubwa, umati mkubwa

katika bonde la uamuzi!

Kwa kuwa siku ya Bwana ni karibu

katika bonde la uamuzi.

15Jua na mwezi vitatiwa giza,

na nyota hazitatoa mwanga wake tena.

163:16 Amu 5:4; Isa 14:16; 25:4; 42:13; 2Sam 22:3; Zek 9:12; Eze 38:19Bwana atanguruma kutoka Sayuni

na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;

dunia na mbingu vitatikisika.

Lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake,

ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.

Baraka Kwa Watu Wa Mungu

173:17 Yoe 2:27; Za 74:2; Isa 4:3; 35:8; Ufu 21:27; Nah 1:15; Kut 6:7; Yer 31:40; Eze 44:9“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mungu wenu,

nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

Yerusalemu utakuwa mtakatifu;

kamwe wageni hawatavamia tena.

183:18 Kut 3:8; Eze 47:1; Zek 13:1; Wim 5:1; Isa 25:6; 30:25; 35:6; 44:3; Ufu 22:1-2; Hes 25:1; Yoe 2:24“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya,

na vilima vitatiririka maziwa;

mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji.

Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana

na kunywesha Bonde la Shitimu.3:18 Au: Bonde la Migunga.

193:19 Yer 51:35; Oba 1:10; Isa 11:14; 34:11Lakini Misri itakuwa ukiwa,

Edomu itakuwa jangwa tupu,

kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda,

ambao katika nchi yao

walimwaga damu isiyo na hatia.

203:20 Ezr 9:12; Amo 9:15Yuda itakaliwa na watu milele

na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.

213:21 Eze 36:25; 48:35; Isa 1:15; 59:20; Za 74:2; Zek 8:3Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe,

nitasamehe.”

Bwana anakaa Sayuni!