Yoeli 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Yoeli 1:1-20

11:1 2Pet 1:21; Ebr 1:1; Yer 1:2; Mdo 2:16Neno la Bwana ambalo lilimjia Yoeli mwana wa Pethueli.

Uvamizi Wa Nzige

21:2 Yoe 2:2, 16; Hos 4:1; 5:1; Isa 7:17; Kum 4:32; Dan 12:1; Mt 24:21Sikilizeni hili, enyi wazee;

sikilizeni, ninyi nyote mnaoishi katika nchi.

Je, jambo kama hili lilishawahi kutokea

katika siku zenu au katika siku za babu zenu?

31:3 Kut 10:2; Za 78:4Waelezeni watoto wenu,

na watoto wenu wawaambie watoto wao,

na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata.

41:4 Kut 10:4, 14-15; Amo 7:1; Neh 3:15; Kum 28:39Kilichosazwa na kundi la tunutu

nzige wakubwa wamekula,

kilichosazwa na nzige wakubwa

parare wamekula,

kilichosazwa na parare

madumadu wamekula.

51:5 Isa 24:7; 32:10; Yoe 3:3Amkeni, enyi walevi, mlie!

Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo,

pigeni yowe kwa sababu ya mvinyo mpya,

kwa kuwa mmenyangʼanywa

kutoka midomoni mwenu.

61:6 Yoe 2:2, 11, 25; Ufu 9:8; Mit 30:25; Za 105:35Taifa limevamia nchi yangu,

lenye nguvu tena lisilo na idadi;

lina meno ya simba,

magego ya simba jike.

71:7 Isa 5:8; Amo 4:9Limeharibu mizabibu yangu

na kuangamiza mitini yangu.

Limebambua magome yake

na kuyatupilia mbali,

likayaacha matawi yake yakiwa meupe.

81:8 Isa 22:2; Amo 8:10; Mit 2:17Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia

anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake.

91:9 Yoe 2:14; Hos 9:4; Isa 22:12Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji

zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana.

Makuhani wanaomboleza,

wale wanaohudumu mbele za Bwana.

101:10 Isa 5:6; 24:4; Yer 3:3; Hos 9:2; Hes 18:12; Yer 12:11Mashamba yameharibiwa,

ardhi imekauka;

nafaka imeharibiwa,

mvinyo mpya umekauka,

mafuta yamekoma.

111:11 Yer 14:3; Ay 6:20; Amo 5:16; Kut 9:31; Isa 17:11Kateni tamaa, enyi wakulima,

lieni, enyi mlimao mizabibu;

huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,

kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.

121:12 Isa 15:6; Kut 28:33; Isa 16:8; Hos 9:1-2; Hag 2:19; Yer 48:33Mzabibu umekauka

na mtini umenyauka;

mkomamanga, mtende na mtofaa,

miti yote shambani, imekauka.

Hakika furaha yote ya mwanadamu

imeondoka.

Wito Wa Toba

131:13 Mwa 37:34; Yer 4:8; 2:17; Hos 9:4; Yoe 2:14Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze;

pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni.

Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha,

enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu;

kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji

zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.

141:14 2Nya 20:3-4; Yon 3:8; Hos 4:1Tangazeni saumu takatifu;

liiteni kusanyiko takatifu.

Iteni wazee

na wote waishio katika nchi

waende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu,

wakamlilie Bwana.

151:15 Yer 30:7; 46:10; Isa 2:12; Eze 30:3; Amo 5:8Ole kwa siku hiyo!

Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu;

itakuja kama uharibifu

kutoka kwa Mwenyezi.1:15 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

16Je, chakula hakikukatiliwa mbali

mbele ya macho yetu:

furaha na shangwe

kutoka nyumba ya Mungu wetu?

17Mbegu zinakauka

chini ya mabonge ya udongo.

Ghala zimeachwa katika uharibifu,

ghala za nafaka zimebomolewa,

kwa maana hakuna nafaka.

18Jinsi gani ngʼombe wanavyolia!

Makundi ya mifugo yanahangaika

kwa sababu hawana malisho;

hata makundi ya kondoo yanateseka.

19Kwako, Ee Bwana, naita,

kwa kuwa moto umeteketeza

malisho ya mbugani

na miali ya moto imeunguza

miti yote shambani.

20Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku;

vijito vya maji vimekauka,

na moto umeteketeza

malisho yote ya mbugani.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

约珥书 1:1-20

1以下是耶和华对毗土珥的儿子约珥所说的话。

严重的蝗灾

2长老们啊,要听此言!

此地所有的居民啊,要留心听!

在你们或你们祖先的时代可曾发生过这样的事?

3要把这事告诉你们的子子孙孙,

传到世世代代!

4蝗虫吃剩的,蝻子来吃;

蝻子吃剩的,蚱蜢来吃;

蚱蜢吃剩的,蚂蚱来吃1:4 蝗虫、蝻子、蚱蜢蚂蚱”四个希伯来词语的确切意思很难考证。

5醉酒之徒啊,醒过来哭泣吧!

贪杯的人啊,哀号吧!

你们再无美酒可饮了。

6有一群强大的队伍侵犯我的国土,

它们不计其数,

有雄狮的獠牙和母狮的利齿。

7它们毁坏我的葡萄树和无花果树,

剥光树皮,然后丢弃,

只留下光秃的树枝。

8我的子民啊,你们要哀哭,

像身披麻衣的少女哭她的未婚夫。

9耶和华殿中的素祭和奠祭都停止了,

事奉耶和华的祭司都哀伤。

10田园荒废,遍地凄凉,

五谷尽毁,

再也没有新酒和油了。

11农夫啊,你们要忧伤!

照料葡萄园的人啊,

你们要哀号!

因为田间的大麦和小麦全毁了。

12葡萄树枯死,

无花果树凋残,

石榴树、棕树、苹果树等田野的一切树木枯干。

人间的欢乐消逝了。

13祭司啊,披上麻衣痛哭吧;

在祭坛前事奉的人啊,要哀号;

我上帝的仆人啊,要披上麻衣过夜;

因为再无素祭和奠祭献到你们上帝的殿中了。

14你们要宣布禁食的圣日,

举行庄严的聚会,

召集长老和当地所有居民,

到你们的上帝耶和华的殿中,

向耶和华呼求。

15那日可怕呀!耶和华的日子近了,

那是全能者施行毁灭的日子。

16我们亲眼看着粮食断绝,

我们上帝殿中的欢乐消失。

17种子在土里腐烂,

五谷枯死,仓库荒废,

谷仓被拆毁。

18牲畜哀鸣,

牛群因无草场而彷徨,

羊群也受苦。

19耶和华啊,我向你呼求,

因为火焰吞灭了旷野的草场,

烈火烧光了田野的树木。

20田野的走兽向你呼求,

因为溪水已经枯干,

火也烧尽了旷野的草场。