Yeremia 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 8:1-22

18:1 Isa 14:19; Za 53:5“ ‘Wakati huo, asema Bwana, mifupa ya wafalme na maafisa wa Yuda, mifupa ya makuhani na manabii, na mifupa ya watu wa Yerusalemu itaondolewa kutoka makaburi yao. 28:2 Yer 44:19; Mdo 7:42; Za 83:10; 2Fal 23:5; Yer 19:13; Ay 31:27; Yer 14:16Itawekwa wazi kwa jua, na mwezi, na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia, na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyotapakaa juu ya ardhi. 38:3 Ay 3:22; Ufu 9:6; Kum 29:28Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’

Dhambi Na Adhabu

48:4 Mik 7:8; Mit 24:16; Yer 31:19; Za 119:67“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki?

Je, mtu anapopotea harudi?

58:5 Yer 5:27; Isa 1:20; Yer 7:24; Zek 7:11Kwa nini basi watu hawa walipotea?

Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?

Wanangʼangʼania udanganyifu

na wanakataa kurudi.

68:6 2Pet 3:9; Ufu 9:20; Za 14:1-3; Mal 3:16Nimewasikiliza kwa makini,

lakini hawataki kusema lililo sawa.

Hakuna anayetubia makosa yake

akisema, “Nimefanya nini?”

Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe

kama farasi anayekwenda vitani.

78:7 Kum 32:28; Wim 2:12; Yer 4:22Hata korongo aliyeko angani

anayajua majira yake yaliyoamriwa,

nao njiwa, mbayuwayu na koikoi

hufuata majira yao ya kurudi.

Lakini watu wangu hawajui

Bwana anachotaka kwao.

88:8 Rum 2:17; Hos 8:12“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara

kwa sababu tunayo sheria ya Bwana,”

wakati ambapo kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi

imeandika kwa udanganyifu?

98:9 Isa 29:14; Yer 5:16-19; 2Fal 19:26; Ay 5:13; Yer 6:19; 1Kor 1:20Wenye hekima wataaibika,

watafadhaika na kunaswa.

Kwa kuwa wamelikataa neno la Bwana,

hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?

108:10 Yer 6:12; Isa 56:11; Mao 4:13; Isa 28:7; Yer 14:14; Mao 2:14; Yer 23:11-15Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,

na mashamba yao kwa wamiliki wengine.

Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

wote wana tamaa ya kupata zaidi;

manabii na makuhani wanafanana,

wote wanafanya udanganyifu.

118:11 Yer 6:14; Eze 13:10; 7:25; Yer 4:10Wanafunga majeraha ya watu wangu

bila uangalifu.

Wanasema, “Amani, amani,”

wakati hakuna amani.

128:12 Za 52:5-7; Yer 3:3; Isa 3:9; Yer 6:15Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno?

Hapana, hawana aibu hata kidogo,

hawajui hata kuona haya.

Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,

watashushwa chini watakapoadhibiwa,

asema Bwana.

138:13 Hos 2:12; Mt 21:19; Yer 5:17; Lk 13:6“ ‘Nitayaondoa mavuno yao,

asema Bwana.

Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu.

Hapatakuwepo na tini kwenye mtini,

majani yake yatanyauka.

Kile nilichowapa

watanyangʼanywa.’ ”

148:14 Yos 10:20; Yer 23:15; Kum 29:18; Dan 9:5; Yer 35:11; 9:15; 14:7, 20“Kwa nini tunaketi hapa?

Kusanyikeni pamoja!

Tukimbilie kwenye miji yenye maboma,

tukaangamie huko!

Kwa kuwa Bwana, Mungu wetu

ametuhukumu kuangamia,

na kutupa maji yenye sumu tunywe,

kwa sababu tumemtenda dhambi.

158:15 Ay 19:8; Yer 14:19Tulitegemea amani,

lakini hakuna jema lililokuja,

tulitegemea wakati wa kupona,

lakini kulikuwa hofu tu.

168:16 Mwa 30:6; Yer 4:15, 29; 51:29; 5:17Mkoromo wa farasi za adui

umesikika kuanzia Dani,

kwa mlio wa madume yao ya farasi,

nchi yote inatetemeka.

Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo,

mji na wote waishio ndani yake.”

178:17 Hes 21:6; Kum 32:24; Isa 3:3; Za 58:5“Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali katikati yenu,

fira ambao hawawezi kulogwa,

nao watawauma,”

asema Bwana.

188:18 Mao 5:17Ee Mfariji wangu katika huzuni,

moyo wangu umezimia ndani yangu.

198:19 Kum 28:64; Yer 9:16; Mik 4:9; Yer 44:3; Isa 41:24; Kum 32:21Sikia kilio cha watu wangu

kutoka nchi ya mbali:

“Je, Bwana hayuko Sayuni?

Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”

“Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,

kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

20“Mavuno yamepita,

kiangazi kimekwisha,

nasi hatujaokolewa.”

218:21 Nah 2:10; Mao 2:13; Eze 6:9; Za 94:5; Isa 43:24; Yer 4:19Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia;

ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika.

228:22 Mwa 37:25; Yer 30:12; Ay 13:4; Isa 1:6Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi?

Je, hakuna tabibu huko?

Kwa nini basi hakuna uponyaji

wa majeraha ya watu wangu?