Yeremia 51 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 51:1-64

151:1 Isa 41:16; Mt 3:12; Yer 50:14; Isa 13:5-951:1 Yer 46:4; Isa 41:25; Yer 50:28, 45; Isa 13:3; Yer 50:9; Isa 21:5; 41:2Hili ndilo asemalo Bwana:

“Tazama nitaamsha roho ya mwangamizi

dhidi ya Babeli na watu wakaao Leb-Kamai.51:1 Leb-Kamai ni Ukaldayo, yaani Babeli, kwa fumbo.

2Nitawatuma wageni Babeli

kumpepeta na kuiharibu nchi yake;

watampinga kila upande

katika siku ya maafa yake.

351:3 Yer 50:29; 46:4Usimwache mpiga upinde afunge kamba upinde wake,

wala usimwache avae silaha zake.

Usiwaonee huruma vijana wake;

angamiza jeshi lake kabisa.

451:4 Isa 13:15-18; Yer 50:30Wataanguka waliouawa katika Babeli,

wakiwa na majeraha ya kutisha barabarani zake.

551:5 Law 26:44; Isa 54:6-8; Za 91:14; Hos 4:1Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa

na Mungu wao, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

ingawa nchi yao imejaa uovu

mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

651:6 Ufu 18:4; Isa 48:20; Yer 50:8, 15; Ay 21:19; Isa 1:24; Mao 3:64; Hes 16:26“Kimbieni kutoka Babeli!

Okoeni maisha yenu!

Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake.

Ni wakati wa kisasi cha Bwana,

atamlipa kile anachostahili.

751:7 Isa 51:22; Ufu 17:4; Yer 25:15-16; 49:12; Ufu 14:8-10Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa Bwana;

aliufanya ulimwengu wote ulewe.

Mataifa walikunywa mvinyo wake;

kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu.

851:8 Isa 14:15; Ufu 14:8; Yer 8:22; Ufu 18:9; Yer 46:11; Isa 21:9Babeli ataanguka ghafula na kuvunjika.

Mwombolezeni!

Tafuteni zeri ya kutuliza maumivu yake,

labda anaweza kupona.

951:9 Isa 13:14; 31:9; Ufu 18:4-5; Yer 50:16“ ‘Tungemponya Babeli,

lakini hawezi kuponyeka;

tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe,

kwa kuwa hukumu yake inafika angani,

inapanda juu hadi mawinguni.’

1051:10 Mik 7:8-9; Za 64:9; Yer 50:28“ ‘Bwana amethibitisha haki yetu;

njooni, tutangaze katika Sayuni

kitu ambacho Bwana Mungu wetu amefanya.’

11“Noeni mishale,

chukueni ngao!

Bwana amewaamsha wafalme wa Wamedi,

kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli.

Bwana atalipiza kisasi,

kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.

1251:12 Za 20:5; 2Sam 18:24; Eze 33:2Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli!

Imarisheni ulinzi,

wekeni walinzi,

andaeni waviziao!

Bwana atatimiza kusudi lake,

amri yake juu ya watu wa Babeli.

1351:13 Yer 50:38; Ufu 17:15; Eze 22:27; Hab 2:9; Isa 45:3Wewe uishiye kando ya maji mengi

na uliye na wingi wa hazina,

mwisho wako umekuja,

wakati wako wa kukatiliwa mbali.

1451:14 Mwa 22:16; Amo 6:8; Nah 3:15; Yer 50:15Bwana Mwenye Nguvu Zote

ameapa kwa nafsi yake mwenyewe:

‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige,

nao watapiga kelele za ushindi juu yako.’

1551:15 Ay 9:8; Isa 40:26; Mdo 14:15; Za 104:24; 136:5“Aliiumba dunia kwa uweza wake;

akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake

na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.

1651:16 Za 18:11-13; Kum 28:12; Yn 1:12; Ay 28:26; Za 135:7Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma,

huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia.

Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua,

naye huuleta upepo kutoka ghala zake.

1751:17 Isa 44:20; Hab 2:18-19; Yer 50:2“Kila mtu ni mjinga na hana maarifa;

kila sonara ameaibishwa na sanamu zake.

Vinyago vyake ni vya udanganyifu,

havina pumzi ndani yavyo.

1851:18 Yer 18; 15; Yn 2:8Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha,

hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia.

1951:19 Za 119:57; Kut 34:9Yeye Aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo,

kwani ndiye Muumba wa vitu vyote,

pamoja na kabila la urithi wake:

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

2051:20 Isa 10:5; Zek 9:13; Mik 4:13; Ay 34:24; Isa 45:1“Wewe ndiwe rungu langu la vita,

silaha yangu ya vita:

kwa wewe navunjavunja mataifa,

kwa wewe naangamiza falme,

2151:21 Kut 15:1; Isa 43:17; Yer 50:37kwa wewe navunjavunja

farasi na mpanda farasi,

kwa wewe navunjavunja

gari la vita na mwendeshaji wake,

2251:22 2Nya 36:17; Isa 13:17-18kwa wewe napondaponda

mwanaume na mwanamke,

kwa wewe napondaponda

mzee na kijana,

kwa wewe napondaponda

kijana wa kiume na mwanamwali,

23kwa wewe nampondaponda

mchungaji na kundi,

kwa wewe nampondaponda

mkulima na maksai,

kwa wewe nawapondaponda

watawala na maafisa.

2451:24 Kum 32:41; Mao 3:64; Yer 50:15; Isa 45:1“Mbele ya macho yako nitamlipiza Babeli na wote waishio Ukaldayo kwa ajili ya makosa yote waliyofanya katika Sayuni,” asema Bwana.

2551:25 Yer 21:13; 50:23; Kut 3:20; Zek 4:7“Mimi niko kinyume nawe, ee mlima unaoharibu,

wewe uangamizaye dunia yote,”

asema Bwana.

“Nitanyoosha mkono wangu dhidi yako,

nikuvingirishe kutoka kwenye kilele cha mwamba,

na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto.

2651:26 Isa 13:19-22; Yer 50:12Hakuna jiwe litakalochukuliwa kutoka kwako

kwa ajili ya kufanywa jiwe la pembeni,

wala jiwe lolote kwa ajili ya msingi,

kwa maana utakuwa ukiwa milele,”

asema Bwana.

2751:27 Isa 13:2; Za 20:5; Mwa 8:4; 10:3; Yer 25:14“Twekeni bendera katika nchi!

Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa!

Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,

iteni falme hizi dhidi yake:

Ararati, Mini na Ashkenazi.

Wekeni jemadari dhidi yake,

pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige.

28Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,

wafalme wa Wamedi,

watawala wao na maafisa wao wote,

pamoja na nchi zote wanazotawala.

2951:29 Isa 13:20; Yer 50:13; Amu 5:4; Yer 49:21; Za 33:11; Yer 48:9Nchi inatetemeka na kugaagaa,

kwa kuwa makusudi ya Bwana dhidi ya Babeli yanasimama:

yaani, kuangamiza nchi ya Babeli

ili pasiwe na yeyote atakayeishi humo.

3051:30 Yer 50:24; 2Sam 19:16; Mao 2:9; Nah 3:13; Isa 47:14; 45:2Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana,

wamebaki katika ngome zao.

Nguvu zao zimekwisha,

wamekuwa kama wanawake.

Makazi yake yameteketezwa kwa moto,

makomeo ya malango yake yamevunjika.

3151:31 Yer 50:24; 2Sam 18:19-31; Dan 5:30Tarishi mmoja humfuata mwingine,

na mjumbe humfuata mjumbe,

kumtangazia mfalme wa Babeli

kwamba mji wake wote umetekwa,

3251:32 Isa 47:14; Yer 50:36Vivuko vya mito vimekamatwa,

mabwawa yenye mafunjo yametiwa moto,

nao askari wameingiwa na hofu kuu.”

3351:33 Isa 21:10; 17:5; Hos 6:11; Mt 13:30; Isa 13:22Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:

“Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria

wakati inapokanyagwa;

wakati wa kumvuna utakuja upesi.”

3451:34 Yer 50:17; Nah 2:12; Hos 8:8“Nebukadneza mfalme wa Babeli ametula,

ametufanya tuchangayikiwe,

ametufanya tuwe gudulia tupu.

Kama nyoka ametumeza

na kujaza tumbo lake kwa vyakula vyetu vizuri,

kisha akatutapika.

35Jeuri iliyofanyiwa miili yetu51:35 Au: Jeuri tuliyofanyiwa sisi na watoto wetu. na iwe juu ya Babeli,”

ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni.

“Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,”

asema Yerusalemu.

3651:36 Za 140:12; Mao 3:58; Yer 20:12; Rum 12:19; Hos 13:15; Yer 50:34; Isa 11:15Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo:

“Tazama, nitatetea shauri lako

na kulipiza kisasi kwa ajili yako;

nitaikausha bahari yake

na kuzikausha chemchemi zake.

3751:37 Isa 13:22; Ufu 12:8; Yer 50:39; 18:16; Ufu 18:2; Nah 3:6; Mal 2:9Babeli utakuwa lundo la magofu

na makao ya mbweha,

kitu cha kutisha na kudharauliwa,

mahali asipoishi mtu.

38Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo,

wanakoroma kama wana simba.

3951:39 Isa 21:5; Yer 50:24; Za 13:3Lakini wakati wakiwa wameamshwa,

nitawaandalia karamu

na kuwafanya walewe,

ili wapige kelele kwa kicheko,

kisha walale milele na wasiamke,”

asema Bwana.

40“Nitawateremsha kama wana-kondoo waendao machinjoni,

kama kondoo dume na mbuzi.

4151:41 Yer 25:26; Isa 13:19; Dan 4:30; Yer 50:13“Tazama jinsi Sheshaki51:41 Sheshaki ni Babeli kwa fumbo. atakamatwa,

majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa.

Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani

kati ya mataifa!

4251:42 Za 18:4; Isa 8:7-8Bahari itainuka juu ya Babeli;

mawimbi yake yenye kunguruma yatamfunika.

4351:43 Isa 13:20; Yer 2:6; Isa 21:1Miji yake itakuwa ukiwa,

kame na jangwa,

nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake,

ambayo hakuna mtu anayepita humo.

4451:44 Isa 21:9; 2Fal 25:4; Isa 25:12; 46:1; Yer 50:15Nitamwadhibu Beli katika Babeli,

na kumfanya atapike kile alichokimeza.

Mataifa hayatamiminika tena kwake.

Nao ukuta wa Babeli utaanguka.

4551:45 Ufu 18:4; Yer 50:8; Isa 48:20; Za 76:10; 79:6“Tokeni ndani yake, enyi watu wangu!

Okoeni maisha yenu!

Ikimbieni hasira kali ya Bwana.

4651:46 Yer 46:27; 2Fal 19:7; Za 18:45Msikate tamaa wala msiogope tetesi

zitakaposikika katika nchi;

tetesi moja inasikika mwaka huu,

nyingine mwaka unaofuata;

tetesi juu ya jeuri katika nchi,

na ya mtawala dhidi ya mtawala.

4751:47 Isa 46:1-2; Yer 50:12; 27:7; 50:12Kwa kuwa hakika wakati utawadia

nitakapoziadhibu sanamu za Babeli;

nchi yake yote itatiwa aibu,

na watu wake wote waliouawa

wataangukia ndani yake.

4851:48 Isa 44:23; Ufu 18:20; Yer 25:26; Isa 41:25; Za 149:2; Ay 3:7Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake

vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli,

kwa kuwa kutoka kaskazini

waharabu watamshambulia,”

asema Bwana.

4951:49 Za 137:8; Yer 50:29“Babeli ni lazima aanguke kwa sababu ya kuwaua Waisraeli,

kama vile waliouawa duniani kote

walivyoanguka kwa sababu ya Babeli.

50Wewe uliyepona upanga,

ondoka wala usikawie!

Mkumbuke Bwana ukiwa katika nchi ya mbali,

na utafakari juu ya Yerusalemu.”

5151:51 Za 44:13-16; 79:4; Mao 1:10“Tumetahayari, kwa maana tumetukanwa

na aibu imefunika nyuso zetu,

kwa sababu wageni wameingia

mahali patakatifu pa nyumba ya Bwana.”

5251:52 Ay 24:12“Lakini siku zinakuja,” asema Bwana,

“nitakapoadhibu sanamu zake,

na katika nchi yake yote

waliojeruhiwa watalia kwa maumivu makali.

5351:53 Mwa 11:4; Isa 14:13-14; Ay 15:21; Yer 49:16Hata kama Babeli ikifika angani

na kuziimarisha ngome zake ndefu,

nitatuma waharabu dhidi yake,”

asema Bwana.

54“Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli,

sauti ya uharibifu mkuu

kutoka nchi ya Wakaldayo.

5551:55 Za 18:4; Isa 25:5Bwana ataiangamiza Babeli,

atanyamazisha makelele ya kishindo chake.

Mawimbi ya adui yatanguruma kama maji makuu,

ngurumo ya sauti zao itavuma.

5651:56 Ay 15:21; Mwa 4:24; Za 46:9; Hab 2:8; Za 94:1-2Mharabu atakuja dhidi ya Babeli,

mashujaa wake watakamatwa,

nazo pinde zao zitavunjwa.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa kisasi,

yeye atalipiza kikamilifu.

5751:57 Za 76:5; Yer 25:27; Isa 6:5; Yer 46:18; Ay 5:13; Isa 21:7Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe,

watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao;

watalala milele na hawataamka,”

asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote.

5851:58 2Fal 25:4; Isa 15:4; 47:14; Hab 2:13; Isa 13:2Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa,

na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto;

mataifa yanajichosha bure,

taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.”

5951:59 Yer 36:4; 52:1; 28:1Huu ndio ujumbe Yeremia aliompa afisa Seraya mwana wa Neria mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake. 6051:60 Kut 17:14; Yer 30:2; 36:2Yeremia alikuwa ameandika ndani ya kitabu kuhusu maafa yote yatakayoipata Babeli, yaani yote yaliyokuwa yameandikwa kuhusu Babeli. 61Yeremia akamwambia Seraya, “Utakapofika Babeli, hakikisha kwamba umesoma maneno haya yote kwa sauti kubwa. 6251:62 Isa 13:20; Yer 9:11; 50:13Kisha sema, ‘Ee Bwana, umesema utaangamiza mahali hapa ili mtu wala mnyama asiishi ndani yake, napo patakuwa ukiwa milele.’ 6351:63 Mwa 2:14Utakapomaliza kusoma hiki kitabu, kifungie jiwe kisha ukitupe ndani ya Mto Frati. 6451:64 Ay 31:40; Za 18:21; Eze 26:21; 28:19Kisha sema, ‘Hivi ndivyo Babeli utakavyozama na usiinuke tena, kwa sababu ya maafa nitakayoleta juu yake. Nao watu wake wataanguka.’ ”

Maneno ya Yeremia yanaishia hapa.