Yeremia 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 5:1-31

Hakuna Hata Mmoja Aliye Mkamilifu

15:1 Eze 22:30; Mwa 18:24; Mik 7:2; Yer 2:29; 2Nya 16:9; Za 45:10“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu,

tazameni pande zote na mtafakari,

tafuteni katika viwanja vyake.

Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu

atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli,

nitausamehe mji huu.

25:2 Tit 1:16; Yer 4:2; Law 19:12Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kama Bwana aishivyo,’

bado wanaapa kwa uongo.”

35:3 2Nya 16:9; Yer 7:28; Isa 9:13; Sef 3:2; Zek 7:2; Eze 36:26; 3:8-9; Amo 4:6Ee Bwana, je, macho yako hayaitafuti kweli?

Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu,

uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo.

Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe

nao walikataa kutubu.

45:4 Yer 8:7; Mit 10:21; Yer 4:22Ndipo nikasema, “Hawa ni maskini tu;

wao ni wapumbavu,

kwa maana hawaijui njia ya Bwana,

sheria ya Mungu wao.

55:5 Mik 3:1, 9; Za 2:3; Yer 2:20Kwa hiyo nitakwenda kwa viongozi

na kuzungumza nao,

hakika wao wanaijua njia ya Bwana,

sheria ya Mungu wao.”

Lakini kwa nia moja nao pia walikuwa wameivunja nira

na kuvivunja vifungo.

65:6 Hos 13:7; Yer 4:7; 30:14; Za 7:12; Law 26:22Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia,

mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza,

chui atawavizia karibu na miji yao,

ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje,

kwa maana maasi yao ni makubwa,

na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.

75:7 Yos 23:7; Yer 12:16; Gal 4:8; Amo 8:14; Kum 32:21; Hes 25:1; Yer 2:11; 13:27“Kwa nini niwasamehe?

Watoto wenu wameniacha na kuapa kwa miungu ambayo si miungu.

Niliwapatia mahitaji yao yote,

lakini bado wamefanya uzinzi na kusongana katika nyumba za makahaba.

85:8 Eze 22:11; 2Sam 11:2-4; Eze 33:26; Yer 29:23Wamelishwa vizuri, kama farasi waume wenye tamaa nyingi,

kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine.

95:9 Yer 44:22; Eze 7:9; Isa 1:24; 57:6Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”

asema Bwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

juu ya taifa kama hili?

105:10 Yer 39:8; 4:27; Amo 9:8“Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu,

lakini msiangamize kabisa.

Pogoeni matawi yake,

kwa kuwa watu hawa sio wa Bwana.

115:11 1Fal 19:10; Yer 3:20; Za 73:27; Isa 24:16Nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda

wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,”

asema Bwana.

125:12 Yer 23:17; 2Nya 36:16; Yer 28:7; Isa 28:15; Yer 14:13Wamedanganya kuhusu Bwana.

Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote!

Hakuna dhara litakalotupata;

kamwe hatutaona upanga wala njaa.

135:13 Yer 14:15; 2Nya 36:16; Ay 6:26Manabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao,

kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.”

145:14 Hos 6:5; Yer 1:9; 23:9; Za 39:3Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote:

“Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,

nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,

na watu hawa wawe kuni

zinazoliwa na huo moto.

155:15 Kum 28:49; Isa 5:26; 2Fal 24:2; Isa 28:11; Mwa 11:7Ee nyumba ya Israeli,” asema Bwana,

“Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako,

taifa la kale na linaloendelea kudumu,

taifa ambalo lugha yao huijui,

wala msemo wao huwezi kuuelewa.

165:16 Ay 39:23Podo zao ni kama kaburi lililo wazi,

wote ni mashujaa hodari wa vita.

175:17 Yer 30:16; Law 26:16; Yer 50:7-17; Kum 28:31-33; Yer 8:16; Hes 16:14; Hos 2:12Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,

wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;

wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe,

wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.

Kwa upanga wataangamiza

miji yenye maboma mliyoitumainia.

18“Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana. 195:19 Kum 29:24-26; 4:28; Yer 15:4; 13:22; 1Fal 9; 9; Yer 16:13“Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Bwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’

20“Itangazie nyumba ya Yakobo hili

na ulipigie mbiu katika Yuda:

215:21 Isa 6:10; Eze 12:2; Mdo 28:26; Isa 42:20; Mk 8:18; Kum 32:6; Yer 4:22; Hes 2:18Sikieni hili, enyi watu wapumbavu, msio na akili,

mlio na macho lakini hamwoni,

mlio na masikio lakini hamsikii:

225:22 Kum 28:58; Ay 4:14; Isa 64:2; Za 46:3Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Bwana.

“Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu?

Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari,

kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita.

Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita;

yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.

235:23 Kum 21:18; Za 14:3Lakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi,

wamegeukia mbali na kwenda zao.

245:24 Mt 5:45; Yoe 2:23; Mwa 8:22; Mdo 14:17; Kum 6:24; Yak 5:7Wao hawaambiani wenyewe,

‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu,

anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,

anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’

25Matendo yenu mabaya yamezuia haya yote,

dhambi zenu zimewazuia msipate mema.

265:26 Za 10:8; Mit 1:11; Mt 7; 15; Mhu 9:12; Yer 9:8; Mik 7:2“Miongoni mwa watu wangu wamo walio waovu

wanaovizia kama watu wanaotega ndege,

na kama wale wanaoweka mitego

kuwakamata watu.

27Kama vitundu vilivyojaa ndege,

nyumba zao zimejaa udanganyifu;

wamekuwa matajiri na wenye nguvu,

285:28 Kum 32:15; Zek 7:10; Kut 22:21-24; Amo 5:12; Za 73:12; 82:3wamenenepa na kunawiri.

Matendo yao maovu hayana kikomo;

hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda,

hawatetei haki za maskini.

29Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”

asema Bwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

juu ya taifa kama hili?

305:30 Yer 18:13; Hos 6:10; Yer 23:14“Jambo la kutisha na kushtusha

limetokea katika nchi hii:

315:31 Eze 13:6; Isa 30:10; Mik 2:11; Mao 4:13; Hos 9:5Manabii wanatabiri uongo,

makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe,

nao watu wangu wanapenda hivyo.

Lakini mtafanya nini mwisho wake?

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

耶利米书 5:1-31

耶路撒冷的罪

1耶和华说:

“你们在耶路撒冷街头四处看看,

在广场找找,

如果你们能找到一个公正诚实的人,

我就赦免这城。

2虽然他们凭永活的耶和华起誓,

却口是心非。”

3耶和华啊,你关注的不是诚实吗?

你责打他们,他们不感到疼痛;

你严惩他们,他们仍不受教。

他们拒不悔改,

脸比石头还硬。

4我想:“他们贫穷、愚昧,

不明白耶和华的道,

也不知道他们上帝的法令。

5我要找他们的首领说话,

因为这些首领明白耶和华的道,

知道他们上帝的法令。”

然而,他们却一致折断轭,

挣开绳索。

6因此,林中的狮子必袭击他们,

荒野的豺狼必残害他们,

豹子也蹲伏在他们的城外,

伺机撕裂出城的人,

因为他们罪大恶极,屡屡叛道。

7耶和华说:

耶路撒冷啊,我怎能赦免你呢?

你的儿女背弃我,

凭假神起誓。

我供应他们的一切需要,

他们却纵情淫乱,

涌向娼妓的家。

8他们像吃得肥壮、发情的公马,

个个垂涎邻居的妻子。

9我怎能不惩罚他们呢?

我怎能不亲自报应这样的国民呢?

这是耶和华说的。

10你们要上去毁坏她的葡萄园,

但不可彻底毁坏。

要砍掉枝子,

因为那些枝子不属于耶和华。

11以色列家和犹大家全然背叛我。

这是耶和华说的。

12“他们毁谤耶和华说,

‘祂不会管的,灾祸不会临到我们,

我们必不会遇见刀剑和饥荒。

13先知不过是一阵风,

他们的话并非来自上帝,

他们预言的灾祸必降临到自己身上。’”

14因此,万军之上帝耶和华对我说:

“因为他们说了这话,

我要使我的话在你口中成为火,

使他们像柴一样被烧毁。

15以色列家啊,我要使一个国家,

一个历久不衰的古国从远方来攻击你们,

你们不明白他们的语言,

也听不懂他们说的话。

这是耶和华说的。

16他们都是勇士,

他们的箭袋像敞开的坟墓。

17他们必吞噬你们的庄稼和粮食,

吞噬你们的儿女,

吞噬你们的牛羊,

吞噬你们的葡萄和无花果,

用刀剑摧毁你们所依靠的坚城。”

18耶和华说:“即使在那时,我也不会彻底毁灭你们。 19耶利米啊,如果有人问,‘为什么我们的上帝耶和华这样待我们?’你可以对他们说,‘你们怎样背弃耶和华,在自己的土地上供奉外族的神明,也要怎样在异地他乡服侍外族人。’

20“要向雅各家宣告,

犹大传讲,

21‘听着,你们这群愚昧无知的人啊,

你们视而不见,

听而不闻。

22难道你们不该敬畏我吗?

这是耶和华说的。

难道你们在我面前不该颤抖吗?

我以沙石为海的界限,

使水永远不能越过它。

汹涌的波涛不能逾越,

澎湃的海浪不能漫过。

23但你们这些人心里顽固,

悖逆成性。

你们离我而去。

24你们心中从不说,

我们要敬畏我们的上帝耶和华,

祂按时降下秋雨和春雨,

让我们按时收割。

25你们的罪过使你们不再风调雨顺,

你们的罪恶使你们失去祝福。’

26我的子民中有恶人,

他们像捕鸟人一样埋伏等候,

设下网罗陷害人。

27他们的家里充满了诡诈,

就像笼子装满了鸟。

他们变得有财有势,

28吃得肥胖红润,坏事做尽,

不秉公审判,不为孤儿申冤,

不为穷人主持公道。”

29耶和华说:“我怎能坐视不理呢?

我怎能不惩罚这样的国家呢?

30这地方发生了一件令人震惊、恐惧的事,

31就是先知说假预言,

祭司滥用权力,

我的子民却以此为乐。

但当最后的结局来临时,

他们还能做什么呢?