Yeremia 49 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 49:1-39

Ujumbe Kuhusu Amoni

149:1 Amo 1:13; Mwa 19:38; 1Sam 11:1-11; 2Sam 10:1-9; Law 18:21; Mwa 30:11Kuhusu Waamoni:

Hili ndilo asemalo Bwana:

“Je, Israeli hana wana?

Je, hana warithi?

Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi?

Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake?

249:2 Yer 4:19; Kum 3:11; Isa 1:2; Eze 25:2-11; Kum 13:16; Yer 30:16; Eze 21:28-32Lakini siku zinakuja,”

asema Bwana,

“nitakapopiga kelele ya vita

dhidi ya Raba mji wa Waamoni;

utakuwa kilima cha magofu,

navyo vijiji vinavyouzunguka

vitateketezwa kwa moto.

Kisha Israeli atawafukuza

wale waliomfukuza,”

asema Bwana.

349:3 Mwa 12:8; Yos 8:28; 13:26; Mwa 37:34“Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa!

Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba!

Vaeni nguo za gunia na kuomboleza,

kimbieni hapa na pale ndani ya kuta,

kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni,

yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.

449:4 Yer 21:13; 9:23; 1Tim 6:17; Yer 3:6Kwa nini unajivunia mabonde yako,

kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana?

Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema,

‘Ni nani atakayenishambulia?’

549:5 Yer 44:14Nitaleta hofu kuu juu yako

kutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

“Kila mmoja wenu ataondolewa,

wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi.

649:6 Yer 12:14-17; 48:47“Lakini hatimaye,

nitarudisha mateka wa Waamoni,”

asema Bwana.

Ujumbe Kuhusu Edomu

749:7 Ay 5:12-14; Za 83:6; Eze 25:12; Mwa 36:11-15, 34; 25:30Kuhusu Edomu:

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Je, hakuna tena hekima katika Temani?

Je, shauri limewapotea wenye busara?

Je, hekima yao imechakaa?

849:8 Mwa 10:7; Yer 25:23; Isa 2:19; Amu 6:2; Mwa 25:3Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,

wewe uishiye Dedani,

kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau

wakati nitakapomwadhibu.

9Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,

wasingebakiza zabibu chache?

Kama wezi wangekujia usiku,

je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?

1049:10 Eze 35:4; Isa 17:14; Mao 1:18; Mwa 3:8; Isa 34:10-12; Yer 11:23Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,

nitayafunua maficho yake,

ili asiweze kujificha.

Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,

naye hatakuwepo tena.

1149:11 Hos 14:3; Mit 23:10-11; Kum 10:18; Yak 1:27Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.

Wajane wako pia

wanaweza kunitumaini mimi.”

1249:12 Isa 51:23; Mt 20:22; Mit 11:31; Yer 25:28-29; 25:15Hili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe. 1349:13 Mwa 22:16; 36:33; Isa 34:6; Yer 42:18; Eze 35:9; Yer 42:18Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema Bwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”

14Nimesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:

Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,

“Jikusanyeni ili kuushambulia!

Inukeni kwa ajili ya vita!”

15“Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,

aliyedharauliwa miongoni mwa watu.

1649:16 Ay 39:27-28; Amo 9:2; Eze 35:13; Oba 1:12Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako

vimekudanganya,

wewe unayeishi katika majabali ya miamba,

wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.

Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,

nitakushusha chini kutoka huko,”

asema Bwana.

1749:17 Kum 29:22; Yer 50:13; Eze 35:7“Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;

wote wapitao karibu

watashangaa na kuzomea

kwa sababu ya majeraha yake yote.

1849:18 Mwa 19:24; Kum 29:23; Amo 4:11; Isa 34:10; Yer 23:14Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,

pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”

asema Bwana,

“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.

Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.

1949:19 Yer 12:5; Ay 9:19; Yer 50:44; Za 89:6-8; 1Sam 17:34; Kut 8:10; 2Nya 20:6“Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani

kuja kwenye nchi ya malisho mengi,

ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.

Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?

Ni nani aliye kama mimi,

na ni nani awezaye kunipinga?

Tena ni mchungaji yupi awezaye

kusimama kinyume nami?”

2049:20 Isa 14:27; Yer 50:45; Mao 1:10; Mal 1:3-4; Isa 34:5; Mwa 36:11Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Edomu,

kile alichokusudia dhidi ya wale waishio Temani:

Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;

yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.

2149:21 Za 114:7; Eze 31:16; Yer 51:29; Eze 26:18; Yer 50:46; Eze 26:15; 27:28Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.

Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu.49:21 Kwa Kiebrania ni Bahari ya Mafunjo.

2249:22 Kum 28:49; Hab 1:8; Isa 13:8; Yer 48:40-41; 4:13; Hos 8:1; Nah 3:13; Mwa 36:33Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,

akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.

Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu

itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

Ujumbe Kuhusu Dameski

2349:23 2Fal 14:28; Mdo 9:2; 1Fal 8:65; Eze 47:16; 2Fal 18:34; Mwa 49:4; Isa 57:20Kuhusu Dameski:

“Hamathi na Arpadi imetahayarika,

kwa kuwa wamesikia habari mbaya.

Wamevunjika moyo na wametaabika

kama bahari iliyochafuka.

2449:24 Yer 13:21Dameski amedhoofika,

amegeuka na kukimbia,

hofu ya ghafula imemkamata sana;

amepatwa na uchungu na maumivu,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

25Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa,

mji ambao ninaupenda?

2649:26 Isa 17:12-14; Yer 50:30; Isa 9:17; 13:18Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;

askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

2749:27 Eze 39:6; Amo 1:4; 1Fal 15:18; Yer 21:14; 43:12; Eze 39:6; Mwa 14:15“Nitatia moto kuta za Dameski;

utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.”

Ujumbe Kuhusu Kedari Na Hazori

2849:28 Mwa 25:13; Amu 6:3; Isa 21:13; Yer 10:22; Yos 11:1Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia:

Hili ndilo asemalo Bwana:

“Inuka, ushambulie Kedari

na kuwaangamiza watu wa mashariki.

2949:29 Yer 6:25; 46:5; Za 120:5Hema zao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa;

vibanda vyao vitatwaliwa

pamoja na mali zao zote na ngamia zao.

Watu watawapigia kelele,

‘Hofu kuu iko kila upande!’

3049:30 Amu 6:2; Yos 11:1; Yer 10:22“Kimbieni haraka!

Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,”

asema Bwana.

“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu;

amebuni hila dhidi yenu.

3149:31 Eze 38:11; Hes 23:9; Mik 7:14“Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,

linaloishi kwa kujiamini,”

asema Bwana,

“taifa lisilo na malango wala makomeo;

watu wake huishi peke yao.

3249:32 Yer 9:26; 25:22; Amu 6:5; Yer 13:24Ngamia wao watakuwa nyara,

nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.

Wale walio maeneo ya mbali

nitawatawanya pande zote,

nami nitaleta maafa juu yao

kutoka kila upande,”

asema Bwana.

3349:33 Yer 10:22; 48:9; Isa 13:22; Hos 11:1“Hazori itakuwa makao ya mbweha,

mahali pa ukiwa milele.

Hakuna yeyote atakayeishi humo;

hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”

Ujumbe Kuhusu Elamu

3449:34 Mwa 10:22; 2Fal 24:18Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda:

3549:35 Za 37:15; Ezr 4:9; Dan 8:2; Isa 22:6Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,

ulio tegemeo la nguvu zao.

3649:36 Dan 11:4Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu

toka pande nne za mbingu,

nitawatawanya katika hizo pande nne,

wala hapatakuwa na taifa

ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa

hawatakwenda.

3749:37 Yer 44:2; 30:24; 9:16; Eze 32:24Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,

mbele yao wale wanaotafuta uhai wao;

nitaleta maafa juu yao,

naam, hasira yangu kali,”

asema Bwana.

“Nitawafuatia kwa upanga

mpaka nitakapowamaliza.

38Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu

na kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,”

asema Bwana.

3949:39 Yer 48:47“Lakini nitarudisha mateka wa Elamu

katika siku zijazo,”

asema Bwana.