Ujumbe Kuhusu Wafilisti
147:1 Zek 9:5-7; Sef 2:4-5; Amo 1:6; Mwa 10:14-19Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:
247:2 Isa 8:7; 14:31; 15:3Hili ndilo asemalo Bwana:
“Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,
yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.
Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake,
miji na wale waishio ndani yake.
Watu watapiga kelele;
wote waishio katika nchi wataomboleza
347:3 Yer 46:9; Eze 23:24; Yer 50:43; Eze 7:17; 21:7kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio,
kwa sauti ya magari ya adui
na mngurumo wa magurudumu yake.
Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,
mikono yao italegea.
447:4 Isa 23:1; Amo 1:9-10; Mwa 10:14-15; Yer 25:22; Yoe 3:4; Kum 2:23; Za 9:2-4Kwa maana siku imewadia
kuwaangamiza Wafilisti wote
na kuwakatilia mbali walionusurika wote
ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni.
Bwana anakaribia kuwaangamiza Wafilisti,
mabaki toka pwani za Kaftori.47:4 Kaftori ndio Krete.
547:5 Yer 41:5; Mik 1:16; Yer 25:20; Law 19:28Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza,
Ashkeloni atanyamazishwa.
Enyi mabaki kwenye tambarare,
mtajikatakata wenyewe mpaka lini?
647:6 Isa 34:5; Yer 12:12; Eze 21:3; Yer 48:10; 50:35“Mnalia, ‘Aa, upanga wa Bwana,
utaendelea mpaka lini ndipo upumzike?
Rudi ndani ya ala yako;
acha na utulie.’
747:7 Eze 25:15-17Lakini upanga utatuliaje
wakati Bwana ameuamuru,
wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni
pamoja na pwani yake?”