Yeremia 46 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 46:1-28

Ujumbe Kuhusu Misri

146:1 Yer 25:15-38; 1:10Hili ni neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa:

246:2 2Fal 23:29; 2Nya 35:20; Mwa 2:14Kuhusu Misri:

Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

346:3 Isa 21:5; Yer 51:11-12; Isa 8:9-10; Yoe 3:9-10“Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo,

mtoke kwa ajili ya vita!

446:4 Eze 21:9-11; 2Nya 26:14; Neh 4:16; 1Sam 17:5, 38Fungieni farasi lijamu,

pandeni farasi!

Shikeni nafasi zenu

mkiwa mmevaa chapeo!

Isugueni mikuki yenu,

vaeni dirii vifuani!

546:5 Yer 48:44; Za 31:13; Yer 49:29; Ufu 6:15-17Je, ninaona nini?

Wametiwa hofu,

wanarudi nyuma,

askari wao wameshindwa.

Wanakimbia kwa haraka

pasipo kutazama nyuma,

tena kuna hofu kuu kila upande,”

asema Bwana.

646:6 Isa 30:16; Za 20:8; Dan 11:19; Mwa 2:14; 15:18Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia,

wala wenye nguvu hawawezi kutoroka.

Kaskazini, kando ya Mto Frati,

wanajikwaa na kuanguka.

746:7 Dan 11:22; Yer 47:2“Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili,

kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?

846:8 Dan 11:10; Eze 29:3, 9; 30:12; Amo 8:8Misri hujiinua kama Mto Naili,

kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi.

Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia,

nitaiangamiza miji na watu wake.’

946:9 Mwa 10:6; Yer 47:3; Isa 66:19; Eze 26:10Songeni mbele, enyi farasi!

Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi,

Endeleeni mbele, enyi mashujaa:

watu wa Kushi46:9 Kushi ni Naili ya Juu; sasa ni Sudan. na Putu46:9 Putu sasa ni Libya. wachukuao ngao,

watu wa Ludi46:9 Nchi iliyo Afrika ya Kaskazini, magharibi ya Mto Naili; sasa ni Libya. wavutao upinde.

1046:10 Eze 32:10; Mao 1:15; Hes 31:3; 2Fal 23:29-30; Law 3:9; Isa 34:6Lakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

siku ya kulipiza kisasi,

kisasi juu ya adui zake.

Upanga utakula hata utakapotosheka,

hadi utakapozima kiu yake kwa damu.

Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu

kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.

1146:11 Yer 8:22; Mwa 37:35; 2Fal 19:21; Isa 47:1; Yer 30:13“Panda hadi Gileadi ukapate zeri,

ee Bikira Binti wa Misri.

Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;

huwezi kupona.

1246:12 Isa 19:4; Nah 3:8-10Mataifa yatasikia juu ya aibu yako,

kilio chako kitaijaza dunia.

Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,

nao wataanguka chini pamoja.”

1346:13 Yer 43:10; Isa 19:1; Yer 27:7; Eze 32:11Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:

1446:14 Yer 43:8; Isa 19:13; 2Sam 2:26; Kum 32:42; Yer 24:8“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,

hubiri pia katika Memfisi46:14 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. na Tahpanhesi:46:14 Ni mji katika Misri.

‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,

kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’

1546:15 Yos 23:5; Isa 66:15-16Kwa nini mashujaa wako wamesombwa

na kupelekwa mbali?

Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana

atawasukuma awaangushe chini.

1646:16 Law 26:37; Isa 13:14; Yer 25:38Watajikwaa mara kwa mara,

wataangukiana wao kwa wao.

Watasema, ‘Amka, turudi

kwa watu wetu na nchi yetu,

mbali na upanga wa mtesi.’

1746:17 Isa 19:11-16; 1Fal 20:10-11Huko watatangaza,

‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,

amekosa wasaa wake.’

1846:18 Yer 48:15; Yos 19:22; 1Fal 18:42“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,

ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote,

“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,

kama Karmeli kando ya bahari.

1946:19 Yer 48:18; Isa 20:4; 19:13; Eze 29:10-12; 35:7Funga mizigo yako kwenda uhamishoni,

wewe ukaaye Misri,

kwa kuwa Memfisi utaangamizwa

na kuwa magofu pasipo mkazi.

2046:20 Isa 14:31; Hos 10:11; Yer 47:2“Misri ni mtamba mzuri,

lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini.

2146:21 2Fal 7:6; Ay 20:24; Za 18:18; Yer 18:17; Lk 15:27; Ay 18:20; Za 37:13Askari wake waliokodiwa katika safu zake

wako kama ndama walionenepeshwa.

Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,

hawataweza kuhimili vita,

kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,

wakati wao wa kuadhibiwa.

2246:22 Za 74:5Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia

kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,

watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,

kama watu wakatao miti.

2346:23 Isa 29:4; Amo 7:12; Za 74:5; Kum 28:42Wataufyeka msitu wake,”

asema Bwana,

“hata kama umesongamana kiasi gani.

Ni wengi kuliko nzige,

hawawezi kuhesabika.

2446:24 2Fal 24:7; Yer 1:15Binti wa Misri ataaibishwa,

atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”

2546:25 Eze 30:14; Nah 3:4; Yer 43:12; Isa 20:6; Eze 30:22; 2Fal 24:7Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,46:25 Thebesi kwa Kiebrania ni No (au No-Amoni), mji katika Misri. na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao. 2646:26 Yer 44:30; Isa 19:4; Eze 32:11; 29:11-16Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana.

2746:27 Yer 29:14; Isa 41:13; Yer 51:46; Isa 11:11; 43:5; 41:8; Yer 50:19“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,

usifadhaike, ee Israeli.

Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali,

uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.

Yakobo atakuwa tena na amani na salama,

wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.

2846:28 Kut 14:22; Hes 14:9; Yer 4:27; Isa 8:9-10Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,

kwa maana mimi niko pamoja nawe,”

asema Bwana.

“Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote

ambayo miongoni mwake nimekutawanya,

sitakuangamiza wewe kabisa.

Nitakurudi, lakini kwa haki tu,

wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”