Yeremia 43 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 43:1-13

Yeremia Apelekwa Misri

143:1 Yer 26:8; 42:9-22Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya Bwana Mungu wao, yaani kila kitu Bwana alichokuwa amemtuma kuwaambia, 243:2 Yer 40:16; 42:1-2; 41:16; Za 12:4; 2The 2:10-12; Neh 9:29; 1Kor 4:18-21; Mwa 19:14; 2Kor 11:31; Kum 13:3; Kut 24:7; Eze 37:18Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! Bwana Mungu wetu hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ 343:3 Yer 38:4; 52:30; 32:12; 41:18Lakini Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu ili ututie mikononi mwa Wakaldayo, ili watuue au watuchukue uhamishoni Babeli.”

443:4 2Nya 25:16; Yer 42:5-6, 10; 41:16Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya Bwana ya kukaa katika nchi ya Yuda. 543:5 Yer 40:12Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa. 643:6 Yer 6:12; 32:12Pia wakawaongoza wanaume wote, wanawake na watoto, na binti za mfalme ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha na Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, na nabii Yeremia, na Baruku mwana wa Neria. 743:7 2Fal 25:26; Yer 2:16; 46:14; Eze 30:18Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii Bwana, wakaenda mpaka Tahpanhesi.

843:8 Za 139:7; Yer 2:16Huko Tahpanhesi neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 943:9 Mwa 31:45-53; Yos 4:1-7; 1Fal 18:31-32; Mwa 47:14“Wayahudi wakiwa wanaona, chukua baadhi ya mawe makubwa na kuyazika katika udongo wa mfinyanzi katika njia iliyojengwa kwa matofali katika ingilio la jumba la kifalme la Farao huko Tahpanhesi. 1043:10 Dan 2:21; Isa 44:22; Eze 29:18-20; Yer 25:9; 27:6; 46:13; 49:38; Za 18; 11Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema yake ya ufalme juu yake. 1143:11 Yer 46:13-26; Zek 11:9; Eze 32:11; 2Tim 1:7; Eze 29:19-20; Mit 11:19; Rum 6:23; Za 49:14Atakuja na kuishambulia Misri, akiwaua wale waliokusudiwa kuuawa, awateke mateka wale waliokusudiwa kutekwa, na upanga kwa wale waliokusudiwa upanga. 1243:12 Kut 12:12; Zek 13:2; Za 109:18-19; 104:2; Yos 7:15; 1Fal 16:32; Isa 2:18; Yer 46:25; Eze 30:13; Dan 11:8Atachoma moto mahekalu yao ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama vile mchungaji ajizungushiavyo vazi lake ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo bila kudhurika. 13Humo ndani ya hekalu la jua43:13 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). nchini ya Misri atabomoa nguzo za ibada, na kuteketeza kwa moto mahekalu ya miungu wa Misri.’ ”