Yeremia 42 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 42:1-22

Yeremia Ashauri Walionusurika Wasihame Yuda

142:1 Yer 40:13; 6:13; 41:11; 44:12Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea, na Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia 242:2 Mwa 20:7; Yak 5:16; Law 26:22; Mdo 8:24; Yer 36:7Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombe Bwana Mungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa tumesalia wachache tu. 342:3 Ezr 8:21; Za 86:11; Mit 3:6; Yer 15:11Omba ili Bwana Mungu wako atuambie twende wapi na tufanye nini.”

442:4 Kut 8:29; 1Sam 12:23; Hes 22:18; 1Fal 22:14; 1Sam 3:17Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba Bwana Mungu wenu kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho Bwana, wala sitawaficha chochote.”

542:5 Kum 4:26; 1Fal 22:16; Za 119:160; Rum 3:4; Yn 8:26; Mwa 31:48; Isa 1:2; Rum 1:9; Ufu 1:5Kisha wakamwambia Yeremia, “Bwana na awe shahidi wa kweli na mwaminifu kati yetu kama hatutafanya sawasawa na kila kitu Bwana Mungu wako atakachokutuma utuambie. 642:6 Kum 5:29; 6:3; Yer 7:23; 43:4; Mhu 3:2; Dan 11:4; 2Nya 34:24; Eze 36:36Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii Bwana Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii Bwana Mungu wetu.”

7Baada ya siku kumi, neno la Bwana likamjia Yeremia. 842:8 Ebr 8:11; Lk 7:28; Mk 9:35; Yer 4:16Kwa hiyo akawaita pamoja Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye na watu wote kuanzia mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana. 9Akawaambia, “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kuwasilisha maombi yenu: 1042:10 Yer 24:6; Kum 30:6; Yer 31:28; 43:4; Mhu 3:2; Dan 11:4; 2Nya 34:24; Eze 36; 36‘Kama mkikaa katika nchi hii, nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa, kwani ninahuzunishwa na maafa niliyowapiga nayo. 1142:11 Eze 30:18; Hes 14:9; Yer 27:11; Ebr 7:25; Rum 8:31; Mit 20:22; 1Sam 15:24Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asema Bwana, kwa kuwa niko pamoja nanyi, nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mikononi mwake. 1242:12 Mwa 31:3; Neh 1:9; Za 106:45-46; Kut 3:21; 2Sam 24:14; 2Kor 1:3Nitawaonea huruma ili naye awe na huruma nanyi na kuwarudisha katika nchi yenu.’

1342:13 Kum 11:28; Yer 44:16“Hata hivyo, kama mkisema, ‘Hatutakaa katika nchi hii,’ hivyo mkaacha kumtii Bwana Mungu wenu, 1442:14 Kum 17:16; Isa 30:2; 65:13; Hes 11:4-5; Ay 6:20; Mt 24:31; 4:2-4; Mit 10:3nanyi kama mkisema, ‘Hapana, tutakwenda kuishi Misri, mahali ambapo hatutaona vita au kusikia sauti ya tarumbeta au kuwa na njaa ya chakula,’ 15basi sikieni neno la Bwana, enyi mabaki ya Yuda. Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Ikiwa mmekusudia kwenda Misri na kufanya makazi huko, 1642:16 Law 26:33; Eze 14:17; 11:8; Yer 41:18; Mwa 41:55; 2:17; Ay 21:20; Eze 3:16; 18:4basi ule upanga mnaouogopa utawapata huko, na njaa mnayoihofia itawafuata huko Misri, nanyi mtafia huko. 1742:17 Yer 21:7; 44:13; 24:10Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’ 1842:18 Kum 29:18-20; 2Nya 12:7; 36:19; Yer 29:18; 39:1-9; 25:18; Hes 5:27; Za 44:13Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama vile hasira yangu na ghadhabu yangu ilivyomwagwa juu ya wale walioishi Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu mtakapokwenda Misri. Mtakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha kulaumia na cha kushutumia, nanyi kamwe hamtaona mahali hapa tena.’

1942:19 Kum 17:16; Isa 30:7; Yer 40:15; 43:2“Enyi mabaki ya Yuda, Bwana amewaambia, ‘Msiende Misri.’ Hakikisheni jambo hili: Ninawaonya leo 2042:20 Eze 14:7-8kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwa Bwana Mungu wenu na kusema, ‘Mwombe Bwana Mungu wetu kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’ 2142:21 Zek 7:11-12; Yer 40:3; Eze 2:7; 12:2; Kut 24:7Nimewaambieni leo, lakini bado ninyi hamtaki kumtii Bwana Mungu wenu katika yote aliyonituma niwaambie. 2242:22 Yer 24:10; Eze 6:11; Isa 1:28; Yer 15:2; Hos 6:9Basi sasa, hakikisheni jambo hili: Mtakufa kwa upanga, njaa na tauni mahali ambapo mnataka kwenda kuishi.”