Yeremia 41 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 41:1-18

141:1 Yer 40:8; Lk 22:21; Za 41:9Katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme na pia alikuwa mmoja wa maafisa wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa. Walipokuwa wakila pamoja huko, 241:2 Za 41:9; Yer 40:5; 2Sam 3:27; Rum 3:15; Yos 11:10; Ebr 11:37; 2Sam 20:9-10; Yer 40:8Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga, wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi. 3Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari wa Kikaldayo waliokuwa huko.

4Siku moja baada ya kuuawa kwa siri kwa Gedalia, kabla mtu yeyote hajafahamu jambo hilo, 541:5 Law 19:27; Yer 48:37; Mwa 12:6; 1Fal 16:24; 3:2; Isa 15:2; Yer 47:5; Hes 16:40; Amu 9:1-57; Mk 14:63watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya Bwana. 641:6 2Sam 5:16; Ufu 20:10; Hos 7:11; Za 5:9Ishmaeli mwana wa Nethania akaondoka Mispa ili kwenda kuwalaki, huku akilia alipokuwa akienda. Alipokutana nao, akasema, “Karibuni kwa Gedalia mwana wa Ahikamu.” 741:7 Mwa 27:24; 2Fal 10:14Walipoingia mjini, Ishmaeli mwana wa Nethania na wale watu waliokuwa pamoja naye wakawachinja na kuwatupa ndani ya kisima. 841:8 Isa 45:3Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine. 941:9 1Fal 15:22; 2Nya 16:6; Amu 6:2; Yos 10:16-18Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti.

1041:10 Yer 40:7, 12-14; Neh 2:10, 19Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao: walikuwa binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni.

1141:11 Yer 40:8-13Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye waliposikia juu ya uhalifu wote ambao Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa ameufanya, 1241:12 2Sam 2:13; Yn 9:7; Kut 14:14; Yn 18:36; Yos 9:3waliwachukua watu wao wote kwenda kupigana na Ishmaeli mwana wa Nethania. Wakakutana naye karibu na bwawa kubwa huko Gibeoni. 13Ikawa watu wote waliokuwa na Ishmaeli walipomwona Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa pamoja naye, wakafurahi. 14Watu wote ambao Ishmaeli alikuwa amewachukua mateka huko Mispa wakageuka na kumfuata Yohanani mwana wa Karea. 1541:15 Yos 21:30; Mit 28; 17; 1Sam 30:17Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na watu wake wanane wakamtoroka Yohanani na kukimbilia kwa Waamoni.

Kukimbilia Misri

1641:16 Yer 42:1; 43:2-4; Eze 7:16; 14:22; Sef 2:9Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu: walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni. 1741:17 2Sam 19:37; Yer 42:14; Mwa 35:19; Mik 5:2Kisha wakaenda mbele na kutua Geruth-Kimhamu karibu na Bethlehemu wakiwa njiani kwenda Misri 1841:18 Hes 14:9; Lk 12:4-5; Yer 40:5; Isa 5:12; Yer 42:16; 2Fal 25:22ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye alikuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

耶利米书 41:1-18

基大利被杀

1七月,犹大王室宗亲、大臣以利沙玛的孙子、尼探雅的儿子以实玛利,带着十个人去米斯巴亚希甘的儿子基大利。趁在米斯巴一同吃饭的时候, 2尼探雅的儿子以实玛利和同来的十个人起来,拔刀刺杀了巴比伦王委任管理犹大沙番的孙子、亚希甘的儿子基大利3还杀了所有在米斯巴基大利在一起的犹大人和那里的迦勒底士兵。

4第二天,基大利被杀的事仍无人知道。 5当天,从示剑示罗撒玛利亚来了八十个人,他们剃了胡须,撕裂衣服,割破身体,手里拿着素祭和乳香要去耶和华的殿。 6尼探雅的儿子以实玛利就从米斯巴出来迎接他们,边走边哭,见面后邀请他们去见亚希甘的儿子基大利7到了城中,尼探雅的儿子以实玛利和部下便屠杀他们,弃尸于蓄水池中。 8其中有十个人对以实玛利说:“请不要杀我们,我们在田野里藏了许多大麦、小麦、油和蜜。”他就没有杀他们。 9尼探雅的儿子以实玛利抛尸的地方是个很大的蓄水池,是从前亚撒王为抵御以色列巴沙而修建的。尼探雅的儿子以实玛利用被杀者的尸体填满了蓄水池。 10以实玛利还掳去了留在米斯巴的公主和其他人。护卫长尼布撒拉旦曾委任亚希甘的儿子基大利管理这些人。尼探雅的儿子以实玛利带着俘虏前往亚扪人那里。

11加利亚的儿子约哈难和其他将领听说尼探雅的儿子以实玛利的一切恶行后, 12便率领部下去攻打他,在基遍的大水池边追上了他。 13-14以实玛利米斯巴掳走的人看见加利亚的儿子约哈难和众将领,喜出望外,都转身投奔约哈难15尼探雅的儿子以实玛利带着八个人逃脱约哈难的追击,前往亚扪16加利亚的儿子约哈难和众将领从基遍救回了那些幸存的士兵、妇孺和宫廷侍臣,他们都是尼探雅的儿子以实玛利杀了亚希甘的儿子基大利之后从米斯巴掳走的。 17他们启程前往埃及,途中在伯利恒附近的基罗特金罕住下。 18他们是害怕迦勒底人才逃往埃及的,因为尼探雅的儿子以实玛利杀了巴比伦王委任管理犹大亚希甘的儿子基大利