Yeremia 32 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 32:1-44

Yeremia Anunua Shamba

132:1 2Fal 25:1; Yer 25:1; 39:1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana, katika mwaka wa kumi wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Nebukadneza. 232:2 Neh 3:25; Yer 37:21; Mt 5:12; Za 88:8Wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka mji wa Yerusalemu, naye nabii Yeremia alikuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi katika jumba la kifalme la Yuda.

332:3 Yer 26:8-9; 21; 4; 34:2-4Basi Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga huko akisema, “Kwa nini unatabiri hivyo? Wewe unasema, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteka. 432:4 Yer 21:7; 52:9; 44:30; 34:21; 38:18, 23; 39:5-7Sedekia mfalme wa Yuda hataweza kuponyoka mikononi mwa Wakaldayo, lakini kwa hakika atatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atazungumza naye ana kwa ana na kumwona kwa macho yake mwenyewe. 532:5 Yer 39:7; Eze 12:13; Mao 1:14; Mit 21:30; Yer 21:4; 2Fal 25:7Atamchukua Sedekia hadi Babeli, mahali atakapoishi mpaka nitakapomshughulikia, asema Bwana. Kama utapigana dhidi ya Wakaldayo, hutashinda.’ ”

6Yeremia akasema, “Neno la Bwana lilinijia kusema: 732:7 Law 25:24-32; Rut 4:3-4; Mt 27:10; Yos 21:18Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako atakuja kwako na kusema, ‘Nunua shamba langu huko Anathothi, kwa sababu wewe kama jamaa ya karibu ni haki na wajibu wako kulinunua.’

8“Kisha, kama Bwana alivyosema, binamu yangu Hanameli alinijia katika ua wa walinzi na kusema: ‘Nunua shamba langu lililoko Anathothi katika nchi ya Benyamini. Kwa kuwa ni haki yako kulikomboa na kulimiliki, jinunulie.’

“Nilijua kwamba hili lilikuwa neno la Bwana. 932:9 Mwa 23:16; Yer 37:12Hivyo nikalinunua shamba hilo lililoko Anathothi kutoka kwa binamu yangu Hanameli, nami nikampimia shekeli kumi na saba32:9 Shekeli 17 za fedha ni sawa na gramu 200. za fedha. 1032:10 Rut 4:9; Isa 8:2; Mwa 23:20Nikatia sahihi na kuweka muhuri hati ya kumiliki, nikaweka mashahidi, na kupima ile fedha kwenye mizani. 11Nikachukua ile hati ya kununulia, nakala iliyotiwa muhuri yenye makubaliano na masharti, pia pamoja na ile nakala isiyo na muhuri, 1232:12 Yer 36:4; 43:3-6; 51:59nami nikampa Baruku mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, hati hii mbele ya binamu yangu Hanameli, na mbele ya mashahidi waliokuwa wameweka sahihi kwenye hati hii na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ua wa walinzi.

13“Nilimpa Baruku maelezo haya mbele yao: 1432:14 Isa 8:16‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Chukua hati hizi, yaani nakala zote zenye muhuri na zisizo na muhuri za hati ya kununulia, na uziweke kwenye gudulia la udongo wa mfinyanzi ili zidumu kwa muda mrefu. 1532:15 Eze 28:26; Amo 9:14-15; Yer 30:18; Isa 44:26Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nyumba, mashamba na mashamba ya mizabibu yatanunuliwa tena katika nchi hii.’

16“Baada ya kumkabidhi Baruku mwana wa Neria hii hati ya kununulia, nilimwomba Bwana:

1732:17 Kum 9:29; Kut 20:5; Za 102:25; 2Fal 3:18; Mwa 32:9-12; Mt 19:26; 2Fal 19:15“Ee Bwana Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza. 1832:18 Kum 5:9-10; Eze 20:5; Kut 20:6; Za 109:14; Yer 10:16; Za 79:12Wewe huonyesha upendo kwa maelfu, lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni Bwana Mwenye Nguvu Zote, 1932:19 Isa 28:29; Ay 34:11, 21; Mit 5:21; Dan 2:20; Mt 16:27; Ay 12:13; 14:16makusudi yako ni makuu, na matendo yako ni yenye uwezo. Macho yako yanaona njia zote za wanadamu, nawe humlipa kila mmoja kulingana na mwenendo wake, na kama yanavyostahili matendo yake. 2032:20 Kut 9:16; Isa 63:12; Kut 3:20; Ay 9:10; Isa 55:13; Yer 13:11Ulitenda ishara za miujiza na maajabu huko Misri, na umeyaendeleza mpaka leo, katika Israeli na miongoni mwa wanadamu wote, nawe umejulikana na kufahamika hivyo mpaka leo. 2132:21 1Nya 17:21; Kut 6:6; Kum 26:8; 2Sam 7:23; Dan 9:15; Yer 6:12; Kum 5:15Uliwatoa watu wako Israeli kutoka Misri kwa ishara na maajabu, kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa na kwa matisho makuu. 2232:22 Kut 3:8; Eze 20:6Uliwapa nchi hii uliyokuwa umeapa kuwapa baba zao, nchi inayotiririka maziwa na asali. 2332:23 Za 78:54-55; Neh 9:26; Dan 9:10-14; Kum 28:64; Za 44:2; Kut 16:28; Yer 11:8Waliingia na kuimiliki, lakini hawakukutii wala kuifuata sheria yako. Hawakufanya kile ulichowaamuru kufanya. Hivyo ukaleta maafa haya yote juu yao.

2432:24 Yer 14:12; Yos 23:15; Kum 4:25-26; 2Sam 20:15; Yer 6:6; Kum 28:2“Tazama jinsi tumezungukwa na jeshi ili kuuteka mji huu. Kwa sababu ya upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo ambao wanaushambulia. Ulilosema limetokea kama vile unavyoona sasa. 25Ingawa mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo, wewe, Ee Bwana Mwenyezi, uliniambia, ‘Nunua shamba kwa fedha, na jambo hilo lishuhudiwe.’ ”

26Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 2732:27 Hes 16:22; Mwa 18:14; 2Fal 3:18“Mimi ndimi Bwana, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza? 2832:28 2Nya 36:17; Yer 21:10Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa Wakaldayo, na mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ambaye atauteka. 2932:29 Yer 19:13; 52:13; 44:18; 7:9Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine.

3032:30 Za 25:7; Yer 22:21; 8:19; 25:7“Watu wa Israeli na wa Yuda hawakufanya kitu kingine ila uovu mbele zangu tangu ujana wao. Naam, watu wa Israeli hawakufanya kitu kingine ila kunikasirisha kwa kazi ambazo mikono yao imetengeneza, asema Bwana. 3132:31 2Fal 23:27; 24:3; Sef 3:1; Mt 23:37; 2Fal 21:4-5; 1Fal 11:7-8Tangu siku ulipojengwa hadi sasa, mji huu umenikasirisha na kunighadhibisha kiasi kwamba ni lazima niuondoe machoni pangu. 3232:32 Isa 1:4-6; Dan 9:8; 1Fal 14:9; Yer 2:26; 44:9Watu wa Israeli na wa Yuda wamenikasirisha kwa uovu wote waliofanya: wao, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao, watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. 3332:33 1Fal 14:9; Za 14:3; Kum 4:5; Isa 28:9; Yer 7:13, 28; 2:27; Eze 8:16; Zek 7:11Walinigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao. Ingawa niliwafundisha tena na tena, hawakupenda kusikiliza wala kuitikia adhabu. 3432:34 Yer 7:30; Eze 8:3-16Waliweka miungu yao ya kuchukiza sana katika nyumba iitwayo kwa Jina langu na kuinajisi. 3532:35 Law 18:21; Yer 7:31; 2Fal 23:10; Yer 19:5; 25:7Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu kwa ajili ya Baali katika Bonde la Ben-Hinomu, ambapo walitoa wana wao na binti zao kafara kwa Moleki, ingawa kamwe sikuamuru, wala halikuingia akilini mwangu, kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.

36“Mnasema kuhusu mji huu, ‘Kwa upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli,’ lakini hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo: 3732:37 Isa 11:12; Yer 23:3-6; Law 25:18; Kum 30:3; Eze 34:28; 39:26; Yer 21:5Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama. 3832:38 Yer 24:7; 2Kor 6:16Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. 3932:39 Eze 11:19; Yn 17:21; 2Nya 30:12; Mdo 4:32; Kum 6:24; 10:16; Za 86:11Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao. 4032:40 Mwa 9:16; Isa 55:3; Yer 24; 7; Isa 42:6; Kum 4:10Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kamwe wasigeukie mbali nami. 4132:41 Kum 28:3-12; Yer 24:6; Kum 30; 9; Amo 9:15; Yer 31:28; Isa 62:4; Mik 7:18Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote.

4232:42 Yer 29:10; 31:28; Mao 3:38“Hili ndilo asemalo Bwana: Kama nilivyoleta maafa haya makubwa kwa watu hawa, ndivyo nitakavyowapa mafanikio niliyowaahidi. 43Kwa mara nyingine tena mashamba yatanunuliwa katika nchi hii ambayo mlisema, ‘Imekuwa ukiwa, isiyofaa, isiyo na watu wala wanyama, kwa sababu imetiwa mikononi mwa Wakaldayo.’ 4432:44 Yer 17:26; Ezr 9:9; Yer 33:7, 11, 26; Rut 4:9; Isa 8:2; Za 14:7Mashamba yatanunuliwa kwa fedha, na hati zitatiwa sahihi, zitatiwa muhuri na kushuhudiwa katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, katika miji ya Yuda na katika miji ya nchi ya vilima, sehemu za magharibi katika miji ya tambarare na katika Negebu, kwa sababu nitarudisha tena mafanikio yao,32:44 Au: nitawarudisha tena kutoka utumwani. asema Bwana.”