Yeremia 30 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 30:1-24

Kurudishwa Kwa Israeli

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 230:2 Isa 30:8; Yer 36:2“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Andika katika kitabu maneno yote niliyonena na wewe. 330:3 Yer 29:14; 16:15; Amo 9:14; Yer 24:6Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema Bwana.”

4Haya ndiyo maneno Bwana aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda: 530:5 Yer 6:25“Hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Vilio vya woga vinasikika:

hofu kuu, wala si amani.

630:6 Yer 4:31; Isa 29:22Ulizeni na mkaone:

Je, mwanaume aweza kuzaa watoto?

Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu

ameweka mikono yake tumboni

kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa,

kila uso ukigeuka rangi kabisa?

730:7 Isa 2:12; Amo 5:18; Yoe 2:11; Isa 22:5; Sef 1:15; Yer 23:3Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha!

Hakutakuwa na nyingine mfano wake.

Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo,

lakini ataokolewa kutoka hiyo.

830:8 Isa 9:4; Yer 25:14; Eze 34:27; Yer 27:7; Za 107:14“ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,

‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwao

na kuvipasua vifungo vyao;

wageni hawatawafanya tena watumwa.

930:9 Isa 55:3-4; 1Sam 13:14; Hos 1:11; 3:5; Yer 33:15; Eze 34:23-24Badala yake, watamtumikia Bwana, Mungu wao

na Daudi mfalme wao,

nitakayemwinua kwa ajili yao.

1030:10 Isa 41:10-13; 43:5; Yer 29:14; Isa 35:9; Yer 17:25; Isa 29:22; Eze 34:25-28“ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,

usifadhaike, ee Israeli,’

asema Bwana.

‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali,

wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.

Yakobo atakuwa tena na amani na usalama,

wala hakuna atakayemtia hofu.

1130:11 Law 26:44; Yer 4:27; 10:24; Hos 11:9; Amo 9:8; Yer 5:18; Isa 29:22; Eze 34:25-28Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’

asema Bwana.

‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote

ambamo miongoni mwao nimewatawanya,

sitawaangamiza ninyi kabisa.

Nitawaadhibu, lakini kwa haki.

Sitawaacha kabisa bila adhabu.’

1230:12 Yer 8:22; 15:18; Ay 6:4; Yer 10:19“Hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Kidonda chako hakina dawa,

jeraha lako haliponyeki.

1330:13 Nah 3:19; Amu 6:31; Yer 14:19; 8:22; 46:11Hakuna yeyote wa kukutetea shauri lako,

hakuna dawa ya kidonda chako,

wewe hutapona.

1430:14 Yer 22:20; Ay 13:24; 30:21; Yer 25:7; Mao 1:2Wale walioungana nawe wote wamekusahau,

hawajali chochote kukuhusu wewe.

Nimekupiga kama vile adui angelifanya,

na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya,

kwa sababu hatia yako ni kubwa mno

na dhambi zako ni nyingi sana.

1530:15 Yer 10:19; Mit 1:31Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako,

yale maumivu yako yasiyoponyeka?

Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyingi

nimekufanyia mambo haya.

1630:16 Kum 23:22; Yoe 3:4-8; Isa 29:8; Yer 10:25; Isa 14:2; Yer 49:2; 50:10“ ‘Lakini watu wote wakuangamizao wataangamizwa;

adui zako wote watakwenda uhamishoni.

Wale wote wakutekao nyara watatekwa nyara;

wote wakufanyao mateka nitawafanya mateka.

1730:17 Isa 6:12; Yer 33:24; Kut 15:26; Za 142:4Lakini nitakurudishia afya yako

na kuyaponya majeraha yako,’

asema Bwana,

‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa,

Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’

1830:18 Kum 30:3; Yer 32:44; Za 103:13; Eze 39:25; 36:10; Yer 31:23; Hes 24:5“Hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo,

na kuhurumia maskani yake.

Mji utajengwa tena juu ya magofu yake,

nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi.

1930:19 Neh 8:12; Mwa 15:5; Isa 51:3, 11; 60:9; Yer 31:4; Isa 35:10; 44:23; Zek 2:4Nyimbo za kushukuru zitatoka kwao

na sauti ya furaha.

Nitaiongeza idadi yao

wala hawatapungua,

nitawapa heshima

na hawatadharauliwa.

2030:20 Isa 54:13-14; Zek 8:5; Yer 31:17; Kut 23:22Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa

siku za zamani,

nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu;

nitawaadhibu wale wote wawaoneao.

2130:21 Yer 23:5-6; Hes 16:5; Kum 17:15Mmoja wao atakuwa kiongozi wao;

mtawala wao atainuka miongoni mwao.

Nitamleta karibu nami,

naye atanikaribia mimi,

kwa maana ni nani yule atakayejitolea

kuwa karibu nami?’

asema Bwana.

2230:22 Isa 19:25; Hos 2:23; Law 26:12‘Kwa hiyo ninyi mtakuwa watu wangu,

nami nitakuwa Mungu wenu.’ ”

2330:23 Yer 23:19; 25:32Tazama, tufani ya Bwana

italipuka kwa ghadhabu,

upepo wa kisulisuli uendao kasi

utashuka juu ya vichwa vya waovu.

2430:24 Yer 4:8; Mao 1:12; Yer 4:28; 23:19-20Hasira kali ya Bwana haitarudi nyuma

mpaka atakapotimiza makusudi yote ya moyo wake.

Siku zijazo

mtayaelewa haya.