Yeremia 3 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 3:1-25

Israeli Asiye Mwaminifu

13:1 Kum 24:1-4; Lk 15:16, 24; Mwa 3; 17; 2Fal 16; 7; Yer 2:25; Eze 16:26; Hos 2:5, 12“Kama mtu akimpa talaka mkewe,

naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine,

je, huyo mume aweza kumrudia tena?

Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa?

Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi:

je, sasa utanirudia tena?”

asema Bwana.

23:2 Mwa 38:14; Eze 16:25; Kum 12:2; Hes 15:39; Isa 1:21“Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone.

Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe?

Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi,

ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani.

Umeinajisi nchi

kwa ukahaba wako na uovu wako.

33:3 Law 26:19; Kum 11:14; Amo 4; 7; Sef 3:5; Yer 5:25; 14:4; Yoe 1:10; Eze 16:30Kwa hiyo mvua imezuiliwa,

nazo mvua za vuli hazikunyesha.

Hata hivyo, una uso usio na haya kama wa kahaba;

unakataa kutahayari kwa aibu.

43:4 Kum 32:6; Hos 2:15; Za 89:26; Isa 63:16; Yer 31:9Je, wewe hujaniita hivi punde tu:

‘Baba yangu, rafiki yangu tangu ujana wangu,

53:5 Isa 57:19; Za 103:9je, utakasirika siku zote?

Je, ghadhabu yako itaendelea milele?’

Hivi ndivyo unavyozungumza,

lakini unafanya maovu yote uwezayo.”

Wito Kwa Ajili Ya Toba

63:6 Kum 12:2; Hos 4:13; Yer 2:20; 1Nya 3:14; Isa 24:16; Yer 31:22; Eze 20:28Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko. 73:7 Eze 16:46; 2Fal 17:13; Amo 4:8Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili. 83:8 Eze 16:47; 23:11; Yer 11:10; Kum 4:27Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa ajili ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi. 93:9 Law 17:7; Isa 1:21; 57:6; Yer 7:22Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti. 103:10 Yer 12:2; Eze 33:31; Hos 7:14; Isa 31:6; Amo 4:9; Hag 2:17; 2Fal 17:19Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema Bwana.

113:11 Eze 16:52; 23:11; Yer 2:19Bwana akaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu. 123:12 Isa 44:22; 2Fal 17:3-6; Kum 4:30; Za 86:15; Yer 31:21; Eze 14:6; 1Fal 3:26Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini:

“ ‘Rudi, Israeli usiye mwaminifu,’ asema Bwana,

‘sitakutazama tena kwa uso uliokunjamana,

kwa kuwa mimi ni mwenye huruma,’ asema Bwana,

‘Sitashika hasira yangu milele.

133:13 Law 26:40-44; Yer 31:18-20; Lk 15:18-21; 1Yn 1:9; Yer 2:2, 5; Kum 12:2; Yer 14; 20Ungama dhambi zako tu:

kwamba umemwasi Bwana Mungu wako,

umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni

chini ya kila mti unaotanda,

nawe hukunitii mimi,’ ”

asema Bwana.

143:14 Rum 11:5; Ay 22:23; Hos 2:19; Isa 54:5“Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema Bwana. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni. 153:15 Isa 31:4; Mdo 20:28; Efe 4:10; Mdo 13:22Kisha nitawapeni wachungaji wanipendezao moyo wangu, ambao watawaongoza kwa maarifa na ufahamu. 163:16 Isa 65:17; Yn 4:21-24; Hes 3:31; 1Nya 15:25Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano la Bwana,’ ” asema Bwana. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine. 173:17 Za 47:8; Eze 43:7; Za 22:23; 81:12; Yer 18:12; 17:12; 33:16Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha Bwana, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la Bwana. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. 183:18 Amo 9:15; Eze 37:19; Yer 16:15; Isa 11:13; Hos 1:11; Yer 30:3; 50:4; Kum 31:7; Kut 4:22Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi.

193:19 Kut 4:22; Isa 63:16; 2Sam 7:14; Za 106:24; Eze 20:6“Mimi mwenyewe nilisema,

“ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana

na kuwapa nchi nzuri,

urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’

Nilidhani mngeniita ‘Baba,’

na msingegeuka, mkaacha kunifuata.

20Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe,

vivyo hivyo mmekosa uaminifu kwangu pia, ee nyumba ya Israeli,”

asema Bwana.

213:21 Yer 31:18; Isa 57:11Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame,

kulia na kuomboleza kwa watu wa Israeli,

kwa sababu wamepotoka katika njia zao

na wamemsahau Bwana Mungu wao.

223:22 Hos 14:4; Ay 22:23; Isa 30:26; Hos 6:1; Yer 33:6; 2:19“Rudini, enyi watu msio waaminifu,

nami nitawaponya ukengeufu wenu.”

“Naam, tutakuja kwako,

kwa maana wewe ni Bwana Mungu wetu.

233:23 Yer 17:14; Za 3:8; Yer 2:20Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima

na milimani ni udanganyifu;

hakika katika Bwana, Mungu wetu,

uko wokovu wa Israeli.

243:24 Yer 11:13; Hos 9:10Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala

matunda ya kazi za baba zetu:

makundi yao ya kondoo na ngʼombe,

wana wao na binti zao.

253:25 Eze 6:9; Dan 9:7; Za 25:7; Yer 22:21; 31:19; Amu 10:10; 1Fal 8:47; Yer 14:20Sisi na tulale chini katika aibu yetu,

na fedheha yetu itufunike.

Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wetu,

sisi na mababa zetu;

tangu ujana wetu hadi leo

hatukumtii Bwana Mungu wetu.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

耶利米書 3:1-25

1耶和華說:「如果丈夫休掉妻子,

妻子離去另嫁別人,

前夫怎會再娶她呢?

那樣做豈不完全玷污了土地嗎?

你曾與許多情人苟合,

現在要歸向我嗎?

2「你舉目看看那些光禿的高山,

你在哪裡沒有被玷污過呢?

你坐在路旁等候情郎,

就像曠野的遊牧民,

你的淫亂惡行玷污了土地。

3因此,秋雨不降,

春雨不來。

你卻仍然不知羞恥,

一副娼妓的嘴臉。

4你不是剛對我說,

『我父啊!你從我年幼時就做我的摯友。

5難道你會永遠發怒、

懷恨到底嗎?』

你雖然這樣說,

卻仍大肆作惡。」

呼籲背信的以色列悔改

6約西亞王執政期間,耶和華對我說:「你看見背信的以色列所行的了嗎?她上到高山上、在綠樹下淫亂。 7我以為她淫亂之後會回到我身邊,她卻執迷不悟。她不貞的妹妹猶大也看見了這事。 8因為背信的以色列淫亂,我給她休書,把她休掉。她不貞的妹妹猶大卻不害怕,竟也去淫亂。 9以色列對淫亂不以為然,竟與石頭木頭苟合,玷污了土地。 10儘管如此,她不貞的妹妹猶大只是假裝歸向我,並不誠心。這是耶和華說的。」

11耶和華對我說:「背信的以色列比不貞的猶大罪過還輕。 12你去向北方宣告,

「『耶和華說,

背信的以色列啊,回轉吧!

我必不向你們發怒,

因為我充滿慈愛,

不會永遠懷怒。』

這是耶和華說的。

13『你必須要承認自己的罪,

承認背叛了你的上帝耶和華,

在綠樹下祭拜各種外邦的神明,

不聽從我的話。』

這是耶和華說的。

14「『背信的子民啊,回轉吧!

因為我是你們的主人3·14 「主人」或譯作「丈夫」。

我要從你們中間選些人帶回錫安

每座城邑選一人,每個宗族選二人。』

這是耶和華說的。

15「『我要賜給你們合我心意的牧人,讓他們用知識與智慧牧養你們。 16你們在地上繁衍昌盛的時候,人們不會再提及耶和華的約櫃,不會再把它放在心上,不會再想起它,不會再感到需要它,也不會再造一個。這是耶和華說的。 17那時,耶路撒冷必被稱為「耶和華的寶座」,萬國都要聚集在耶路撒冷尊崇耶和華的名,不再執迷不悟地作惡。 18那時,猶大人必與以色列人一同從北方來到我賜給你們祖先作基業的地方。

19「『我曾想,我多麼願意把你們當成我的兒女,

賜給你們萬國中最肥美的土地。

我原以為你們會叫我「父親」,

再不離我而去。

20然而,以色列家啊!

你們竟對我不忠,

就像不貞的妻子離開丈夫。

這是耶和華說的。』」

21從光禿的山頭傳來聲音,

以色列子民哭泣呼求的聲音,

因為他們走入歧途,

忘掉了他們的上帝耶和華。

22耶和華說:「背信的子民啊,

歸來吧!

我要醫治你們背信的病。」

他們說:「是的,我們要到你面前,

因為你是我們的上帝耶和華。

23在高山丘陵上狂歡、

拜偶像真是枉然,

唯有我們的上帝耶和華才能拯救以色列

24「從我們年幼時,那些可恥的神像就吞噬了我們祖先辛苦得來的牛羊和兒女。 25讓我們躺在自己的羞恥中,讓我們的恥辱遮蓋我們吧!因為我們和我們的祖先都得罪了我們的上帝耶和華,我們自幼至今一直沒有順服我們的上帝耶和華。」