Yeremia 29 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 29:1-32

Barua Kwa Watu Wa Uhamisho

129:1 2Nya 36:10; Yer 13:1729:1 Eze 39:25; Rum 10:20; Sef 3:20; Yer 46:27; Eze 37:21; Kum 30:3; Yer 30:3Haya ndiyo maneno ya ile barua ambayo nabii Yeremia aliituma kutoka Yerusalemu kwenda kwa wazee waliobaki miongoni mwa wale waliohamishwa, na kwa makuhani, manabii na watu wengine wote ambao Nebukadneza alikuwa amewachukua kwenda uhamishoni Babeli kutoka Yerusalemu. 229:2 2Fal 24:12; Yer 22:24-28; 2Fal 24:8(Hii ilikuwa ni baada ya Mfalme Yekonia29:2 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini. na malkia mamaye, maafisa wa mahakama, viongozi wa Yuda na wa Yerusalemu, mafundi na wahunzi kwenda uhamishoni kutoka Yerusalemu.) 3Barua ilikabidhiwa kwa Elasa mwana wa Shafani, na kwa Gemaria mwana wa Hilkia, ambao Sedekia mfalme wa Yuda aliwatuma kwa Mfalme Nebukadneza huko Babeli. Barua yenyewe ilisema:

429:4 Yer 24:5Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, awaambialo wale wote niliowapeleka kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli: 5“Jengeni nyumba na mstarehe, pandeni bustani na mle mazao yake. 629:6 Yer 30:19Oeni wake na mzae wana na binti, waozeni wana wenu wake, nanyi watoeni binti zenu waolewe, ili nao pia wazae wana na binti. Ongezekeni idadi yenu huko, wala msipungue. 729:7 Ebr 6:10; 1Tim 2:1-2; Rum 13:1-5; Es 3:8Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. Mwombeni Bwana kwa ajili ya mji huo, kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi.”

829:8 Yer 37:9; 23:21-27; 1Yn 4:1; Kum 13:1Naam, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Msikubali manabii na wabashiri walioko miongoni mwenu wawadanganye. Msisikilize ndoto ambazo mmewatia moyo kuota. 929:9 Mao 2:14; Eze 13:6; Yer 27:15; 23:21Wanawatabiria ninyi uongo kwa jina langu. Sikuwatuma,” asema Bwana.

1029:10 2Nya 36:21; Dan 9:2; Yer 16:14; 24:6; 32:42; 1Fal 8:56Hili ndilo asemalo Bwana: “Miaka sabini itakapotimia kwa ajili ya Babeli, nitakuja kwenu na kutimiza ahadi yangu ya rehema ya kuwarudisha mahali hapa. 1129:11 Za 40:5; Zek 8:15; Isa 55:12Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. 1229:12 Za 145:19; Isa 55:6; Dan 9:3; Hos 2:23; Sef 3:12; Zek 13:9Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. 1329:13 Mt 7:7; Kum 4:29; 2Nya 6:37; Yer 24:7Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana.

15Mnaweza mkasema, “Bwana ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,” 16lakini hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme aketiaye kiti cha enzi cha Daudi, na watu wa kwenu wote wanaobaki katika mji huu, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi uhamishoni. 1729:17 Yer 24:8-10; 27:8; Isa 5:4Naam, hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao, nami nitawafanya kuwa kama tini dhaifu zile ambazo ni mbovu sana zisizofaa kuliwa. 1829:18 Yer 15:4; Kum 28:25; Yer 42:18; Mao 2:18-19; Hes 5:27; Yer 18:16; Isa 28:22Nitawafukuza kwa upanga, kwa njaa na kwa tauni, nami nitawafanya kitu cha kuchukiza sana kwa falme zote za dunia, na kuwa kitu cha laana na cha kuogofya, cha dharau na kukemewa, miongoni mwa mataifa yote nitakakowafukuzia. 1929:19 Yer 6:19; 32:33; 25:4; 7:25Kwa kuwa hawakuyasikiliza maneno yangu,” asema Bwana, “maneno ambayo niliwatumia tena na tena kupitia watumishi wangu manabii. Wala ninyi watu wa uhamisho hamkusikiliza pia,” asema Bwana.

2029:20 Yer 24:5; Amo 3:6; Mik 4:10Kwa hiyo, sikieni neno la Bwana, enyi nyote mlio uhamishoni, niliowapeleka Babeli kutoka Yerusalemu. 2129:21 Yer 14:14Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya, na Sedekia mwana wa Maaseya, wanaowatabiria uongo kwa jina langu: “Nitawatia mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atawaua mbele ya macho yenu hasa. 2229:22 Dan 3:6; Isa 65:15Kwa ajili yao, watu wote wa uhamisho kutoka Yuda walioko Babeli watatumia laana hii: ‘Bwana na akutendee kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwachoma kwa moto.’ 2329:23 Yer 23:14; Ebr 4:13; Yer 13:27; Sef 3:4; Mwa 31:48; Yer 7:11Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya. Nami nayajua haya, na ni shahidi wa jambo hilo,” asema Bwana.

Ujumbe Kwa Shemaya

24Mwambie Shemaya Mnehelami, 2529:25 2Fal 25:18; Yer 21:1“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania, 2629:26 Kum 13:1-5; 1Sam 10:11; 2Fal 9:11; Yer 20:2; Yn 10:20; Hos 9:7Bwana amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya Bwana. Unapaswa kufunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii. 27Kwa nini basi hukumkemea Yeremia Mwanathothi, aliyejifanya kama nabii miongoni mwenu? 28Ametutumia ujumbe huu huku Babeli: Mtakuwako huko muda mrefu. Kwa hiyo jengeni nyumba mkakae; pandeni mashamba na mle mazao yake.’ ”

29Kuhani Sefania, hata hivyo, akamsomea nabii Yeremia ile barua. 30Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 3129:31 Yer 14:14; 28:15“Tuma ujumbe huu kwa watu wote walio uhamishoni: ‘Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, hata ingawa sikumtuma, naye amewafanya kuamini uongo, 3229:32 1Sam 2:30-33; Yer 28:16; Rum 2:8hili ndilo Bwana asemalo: Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asema Bwana, kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ”