Yeremia 26 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 26:1-24

Yeremia Atishiwa Kuuawa

126:1 2Fal 23:36Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwa Bwana: 226:2 Yer 19:14; Kut 23:14; Mdo 20:27; Kum 12:5; Yer 17:19; Mt 28:20; Kum 4:2“Hili ndilo Bwana asemalo: Simama katika ua wa nyumba ya Bwana na useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba ya Bwana. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno. 326:3 Kum 30:2; Isa 55:7; Yer 18:8; 2Nya 33:12-13; Yer 35:15; 36:7Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya. 426:4 Law 26:14; Yer 25:3; 1Fal 9:6; Yer 11:8Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu, 526:5 Mit 1:24; Isa 65:12; Yer 7:13; 25:4; 44:5nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza), 626:6 Yos 18:1; Amu 18:31; Kum 28:25; 2Fal 22:19ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ”

7Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba ya Bwana. 826:8 Mdo 6:12; 21:27; Law 24:15-16; Neh 9:26; Yer 11:21Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu Bwana alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe! 926:9 Law 26:32; Yer 9:11; Mdo 21:32Kwa nini unatoa unabii katika jina la Bwana kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba ya Bwana.

1026:10 Yer 34:19; Eze 22:27; Mwa 23:10Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya Bwana na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya Bwana. 1126:11 Yer 38:4; Kum 18:20; Mdo 6:11; Kum 18:20Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”

1226:12 Yer 1:18; Isa 6:8; Mdo 5:29; Amo 7:15; Mdo 4:18-20Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Bwana amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia. 1326:13 Yoe 2:12; Yer 7:5; 35:15; 11:4; 18:8Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu, na kumtii Bwana Mungu wenu. Ndipo Bwana atawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu. 1426:14 Yos 9:15; Yer 38:5Lakini kwa habari yangu mimi, niko mikononi mwenu, nifanyieni lolote mnaloona kuwa ni jema na la haki. 1526:15 Kum 19:10; Yer 1:17Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli Bwana amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”

1626:16 Mdo 23:9; 5:34-39; 23:29Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la Bwana, Mungu wetu.”

17Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele, wakaliambia kusanyiko lote la watu, 1826:18 Isa 2:3; 2Fal 25:9; Neh 4:2; Mik 1:4; Zek 8:3; Yer 17:3; 9:11“Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“ ‘Sayuni italimwa kama shamba,

Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,

na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu

kilichofunikwa na vichaka.’

1926:19 1Nya 3:13; Kut 32:14; Isa 37:14-20; 2Sam 24:16; Hab 2:10; 2Nya 32:24-26Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha Bwana na kuhitaji msaada wake? Je, Bwana hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”

2026:20 Yos 9:17(Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la Bwana. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia. 2126:21 Mwa 31:21; Mt 10:23; 1Fal 19:2-3; Yer 2:30; Mt 23:37Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumuua. Lakini Uria alipata habari, na kwa kuogopa akakimbilia Misri. 2226:22 Yer 36:12, 25; Mit 29:12Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria. 2326:23 2Fal 23:6; Ebr 11:37Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimuua kwa upanga, na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo.)

2426:24 2Fal 22:12; Yer 39:14Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shafani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 26:1-24

耶利米被捕

1犹大约西亚的儿子约雅敬执政初期,耶和华对耶利米说: 2“这是耶和华说的,‘你要站在我殿的院子里,把我吩咐你的话一字不漏地告诉从犹大各城前来敬拜的人。 3或许他们会听从我的话,改邪归正,那样我会施怜悯,取消原本用来惩治他们罪恶的灾祸。 4你要告诉他们,耶和华这样说,“如果你们不听从我的话,不遵行我赐给你们的律法, 5不听从我屡次派我的仆人——众先知传给你们的话, 6我必使这殿像示罗一样被毁,使耶路撒冷被万国咒诅。”’”

7祭司、先知和民众都听见了耶利米在耶和华的殿里说的这些话。 8耶利米传达完耶和华的话之后,祭司、先知和民众就抓住他,说:“你真该死! 9你为什么奉耶和华的名预言这殿必像示罗一样被毁,这城必要荒无人烟呢?”于是,他们在耶和华的殿里把耶利米围了起来。

10犹大的首领得知后,就离开王宫,上到耶和华的殿,坐在耶和华殿新门的入口。 11祭司和先知对官员和民众说:“这人该被处死!因为他预言这城要被毁,这是你们亲耳听到的。”

12耶利米对官员和民众说:“你们刚才听见的这些关于这殿和这城的预言都是耶和华差我说的。 13你们要改邪归正,听从你们上帝耶和华的话,这样耶和华必施怜悯,取消本来要降给你们的灾祸。 14至于我,我已落在你们手中,你们认为怎样好就怎样待我吧! 15不过,你们要知道,如果你们置我于死地,你们和这城及城中的居民必担当滥杀无辜的罪,因为确实是耶和华派我来告诉你们这些预言的。”

16官员和民众便对祭司和先知说:“这人不该被处死,因为他是奉我们上帝耶和华的名对我们说话。” 17有几个长老站起来对众人说: 18犹大希西迦执政期间,摩利沙弥迦犹大众人预言说,

“‘万军之耶和华说锡安必被夷为平地,

耶路撒冷必沦为废墟,

圣殿山要成为一片荒林。’

19“但犹大希西迦犹大众人并没有处死他。希西迦敬畏耶和华,求祂开恩,耶和华才施怜悯,没有把原本预备的灾祸降给他们。若处死这人,我们会大祸临头。”

20当时,基列·耶琳示玛雅的儿子乌利亚也奉耶和华的名预言这城和这地方将被毁,内容与耶利米说的一样。 21约雅敬王和他的王公大臣听见乌利亚的话,就想处死他。乌利亚得知后,吓得逃到埃及去了。 22约雅敬王便派亚革波的儿子以利拿单率随从去埃及捉拿他。 23他们把乌利亚埃及押到约雅敬王面前,王用刀杀了他,把尸首抛在平民的坟地中。 24然而,沙番的儿子亚希甘保护耶利米,他才没被交给民众处死。