Yeremia 25 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 25:1-38

Miaka Sabini Ya Kuwa Mateka

125:1 2Fal 24:2; Yer 46:2Neno likamjia Yeremia kuhusu watu wote wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. 225:2 Yer 18:11Hivyo nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wale wote waishio Yerusalemu: 325:3 1Nya 3:14; Yer 11:7; 26:5; 7:26; Isa 65:12Kwa miaka ishirini na mitatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, hadi siku hii ya leo, neno la Bwana limekuwa likinijia, nami nimesema nanyi mara kwa mara, lakini hamkusikiliza.

425:4 Yer 6:17; 29:19; 7:25-26Ingawa Bwana amewatuma watumishi wake wote hao manabii kwenu mara kwa mara, hamkusikiliza wala hamkujali. 5Walisema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya na matendo yake maovu, ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayo Bwana aliwapa ninyi na baba zenu milele. 625:6 Kut 20:3; Kum 8:19Msiifuate miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Msinikasirishe kwa vitu ambavyo mmevitengeneza kwa mikono yenu.”

725:7 Kum 32:21; 2Fal 17:20; Yer 7:19“Lakini ninyi hamkunisikiliza mimi, tena mkanikasirisha kwa vitu mlivyovitengeneza kwa mikono yenu, nanyi mmejiletea madhara juu yenu wenyewe,” asema Bwana.

8Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu, 925:9 Isa 13:3-5; 14:31; 41:2; 2Nya 29:8; Yer 18:16; Hes 21:2; Eze 12:20nitayaita mataifa yote ya kaskazini na mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli,” asema Bwana. “Nitawaleta waishambulie nchi hii na wakazi wake wote, na dhidi ya mataifa yote yanayowazunguka. Nitawaangamiza kabisa na kuwafanya kitu cha kuchukiwa na kudharauliwa, na kuwa magofu daima. 1025:10 Isa 24:8; Eze 26:13; Yer 7:34; Mhu 12:3-4; Mao 5:15; Ufu 18:22-23; 15:5Nitawaondolea sauti ya shangwe na furaha, sauti ya bibi na bwana arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na mwanga wa taa. 1125:11 Law 26:31-32; Yer 12:11-12; 28:14; 4:26-27; 2Nya 36:21Nchi hii yote itakuwa ukiwa na isiyofaa kitu, nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.”

1225:12 Yer 27:7; 29:10; Isa 13:19-22; 14:22-23; Mwa 10:10; Za 137:8“Lakini miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asema Bwana. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele. 1325:13 Isa 30:8Nitaleta juu ya nchi hiyo mambo yote niliyosema dhidi yake, yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki, na kutolewa unabii na Yeremia dhidi ya mataifa yote. 1425:14 Isa 14:6; Yer 50:19; 51:27-28; Ay 21:19; Yer 27:7Wao wenyewe watakuwa watumwa wa mataifa mengi na wafalme wakuu. Nitawalipizia sawasawa na matendo yao na kazi ya mikono yao.”

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Mungu

1525:15 Za 75:8; Ufu 14:10; Ay 21:20; Isa 51:17; Yer 49:12; Mao 4:21; Eze 23:31Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao. 1625:16 Za 60:3; Nah 3:11; Yer 51:7Watakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.”

1725:17 Yer 1:10; 27:3Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa: 1825:18 Yer 24; 9; Mwa 19:13; Yer 44:22; 13:13; Ay 12:19; 2Nya 29:8Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo; 1925:19 2Fal 18:21; Isa 20:3; Eze 29:2; Yer 44:30pia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote, 2025:20 Mwa 10:23; Yer 47:5; Amo 1:7-8; Yos 13:3; Sef 2:4-7; Mwa 10:19pia wageni wote walioko huko; wafalme wote wa nchi ya Usi; wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi); 2125:21 Mwa 19:38; Yer 27:3; Mwa 25:30; Kum 23:6Edomu, Moabu na Amoni; 2225:22 Mwa 10:15; Yer 47:4; Dan 11:18; Isa 11:11; Yos 19:29; Isa 48:20; Yer 31:10wafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ngʼambo ya bahari; 2325:23 Mwa 25:3, 15; 22:21; Yer 9:26; 49:32Dedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali; 2425:24 2Nya 9:14; Yer 50:37wafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa; 2525:25 Mwa 25:2; 10:22; Isa 21:2wafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi; 2625:26 Yer 51:41; 50:3-9; Isa 23:17na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki25:26 Sheshaki ni Babeli kwa fumbo. atakunywa pia.

2725:27 Isa 29:9; Nah 3:18; Hab 2:16; Eze 14:17; 21:4; Yer 51:57; Eze 23:32-34“Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’ 28Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe! 2925:29 Mit 11:31; 1Pet 4:17; Isa 10:12; 2Sam 5:7; Eze 38:21; Yer 13:12-14; Isa 34:2Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’

3025:30 Isa 42:13; 16:10; Yoe 3:16; Za 46:6; Isa 63:3; Ufu 14:19-20“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:

“ ‘Bwana atanguruma kutoka juu;

atatoa sauti ya ngurumo

kutoka makao yake matakatifu

na kunguruma kwa nguvu sana

dhidi ya nchi yake.

Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,

atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.

3125:31 Hos 4:1; Mik 6:2; Yer 23:19; 1Sam 12:7; Yer 2:9, 35; Eze 36:5; Yer 15:9Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,

kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa;

ataleta hukumu juu ya wanadamu wote

na kuwaua waovu wote,’ ”

asema Bwana.

3225:32 Isa 34:2; Yer 23:19; Isa 30:25; Kum 28:49Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama! Maafa yanaenea

kutoka taifa moja hadi jingine;

tufani kubwa inainuka

kutoka miisho ya dunia.”

3325:33 Eze 39:17-20; Isa 66:16; Yer 16:4; Isa 34:2-8; Yer 8:2; Za 79:3Wakati huo, hao waliouawa na Bwana watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi.

3425:34 Yer 6:26; Za 44:22; Zek 11:4-7; Yer 2:8; Zek 10:3; Isa 34:6; Yer 50:27Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,

mgaagae mavumbini,

ninyi viongozi wa kundi.

Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;

mtaanguka na kuvunjavunjwa

kama vyombo vizuri vya udongo.

3525:35 Ay 11:20Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia,

viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea.

3625:36 Yer 6:26; 23:1; Zek 11:3Sikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi,

kwa maana Bwana anayaharibu malisho yao.

37Makao yao ya amani yataharibiwa

kwa sababu ya hasira kali ya Bwana.

3825:38 Ay 10:16; Yer 4:7; 44:22; 4:26; 46:16; 50:16; Kut 15:7Kama simba ataacha pango lake,

nchi yao itakuwa ukiwa

kwa sababu ya upanga wa mdhalimu,

na kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.