Yeremia 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 24:1-10

Vikapu Viwili Vya Tini

124:1 2Fal 24:16; 2Nya 36:9; Kut 23:19; Kum 26:2; Amo 8:1-2Baada ya Yekonia24:1 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini. mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli, Bwana akanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la Bwana. 224:2 Wim 2:13; Isa 5:4Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama zile za mavuno ya kwanza. Kikapu cha pili kilikuwa na tini dhaifu sana, mbovu mno zisizofaa kuliwa.

324:3 Yer 1:11; Amo 8:1-2Kisha Bwana akaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?”

Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu ni mbovu mno zisizofaa kuliwa.”

4Kisha neno la Bwana likanijia: 524:5 Yer 29:4, 20“Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo. 624:6 Kum 30:3; Eze 11:17; Yer 42:10; 30:9; Amo 9:14-15Macho yangu yatakuwa juu yao kwa ajili ya kuwapatia mema, nami nitawarudisha tena katika nchi hii. Nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa, 724:7 Law 26:12; Ebr 8:10; Yer 32:40; 2Nya 6:37; Eze 11:19; Isa 11:9; 51:18; Zek 2:11nitawapa moyo wa kunifahamu mimi, kwamba mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.

824:8 Yer 29:17; 39:6-9; 44:26; 46:14; 32:4-5; 44:30“ ‘Lakini kama zilivyo zile tini dhaifu, ambazo ni mbovu mno zisizofaa kuliwa,’ asema Bwana, ‘ndivyo nitakavyomtendea Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na mabaki wengine kutoka Yerusalemu, wawe wamebaki katika nchi hii, au wanaishi Misri. 924:9 Yer 25:18; 34:17; Kum 28:25; 2Fal 22:19; Yer 29:18; Dan 9:7; Yer 15:4Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, popote nitakapowafukuzia. 1024:10 Isa 51:19; Ufu 6:8; Yer 27:8; 9:16; 15:2; Kum 28:21Nitautuma upanga, njaa na tauni dhidi yao hadi wawe wameangamia kutoka nchi niliyowapa wao na baba zao.’ ”