Yeremia 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 23:1-40

Tawi La Haki

123:1 Eze 34:1-10; Zek 11:5-7, 15-17; Isa 56:11; Eze 34:31; Yer 10:21; 12:10; 25:36“Ole wao wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” asema Bwana. 223:2 Kut 32:34; Yer 21:12; Eze 34:8-10; Yn 10:8; Yer 10:21; 13:20Kwa hiyo hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asema Bwana. 323:3 Isa 11:10-12; Eze 34:11-16; Yer 32:37; 1Fal 8:48“Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia, nami nitawarudisha katika malisho yao, mahali ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao. 423:4 Mwa 48:15; Isa 31:4; Yer 46:26-28; Yn 6:39; Yer 30:10; 31:10Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asema Bwana.

523:5 2Fal 19:26; Eze 17:22; Mwa 18:19; Zek 6:12; Dan 9:24; Isa 4:2Bwana asema, “Siku zinakuja,

nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki,

Mfalme atakayetawala kwa hekima,

na kutenda lililo haki na sawa katika nchi.

623:6 Kut 23:21; Ezr 9:15; Zek 14:11; 1Kor 1:30; Law 25:18; Kum 32:8; Hos 2:8; Yer 33:16; Rum 3:21-22; Isa 42:6Katika siku zake, Yuda ataokolewa

na Israeli ataishi salama.

Hili ndilo jina atakaloitwa:

Bwana Haki Yetu.

723:7 Kum 15:15; Yer 16:14; 30:3“Hivyo basi, siku zinakuja, wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ 823:8 Eze 34:13; Isa 43:5-6; Yer 30:10; Eze 20:42; Amo 9:14-15bali watasema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asema Bwana. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”

Manabii Wasemao Uongo

923:9 Hab 3:16; Yer 20:8-9; 4:19; Ay 4:14Kuhusu manabii:

Moyo wangu umevunjika ndani yangu;

mifupa yangu yote inatetemeka.

Nimekuwa kama mtu aliyelewa,

kama mtu aliyelemewa na divai,

kwa sababu ya Bwana

na maneno yake matakatifu.

1023:10 Za 107:34; Yer 9:2, 10; 4:26; Hos 4:2-3; Kum 28:23-24; Yer 12:11Nchi imejaa wazinzi;

kwa sababu ya laana, nchi imekauka

na malisho yaliyoko nyikani yamekauka.

Mwenendo wa manabii ni mbaya

na mamlaka yao si ya haki.

1123:11 Yer 6:13; Sef 3:4; 2Fal 21:4; Yer 8:10; 7:10“Nabii na kuhani wote si wacha Mungu;

hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,”

asema Bwana.

1223:12 Ay 3:23; Za 35:6; Mit 4:19; Yer 11:23; Kum 32:35; Yer 13:16“Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi,

watafukuziwa mbali gizani

na huko wataanguka.

Nitaleta maafa juu yao

katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,”

asema Bwana.

1323:13 1Fal 18:18-22; Isa 9:16; 3:12; Eze 13:10“Miongoni mwa manabii wa Samaria

nililiona jambo la kuchukiza:

Walitabiri kwa Baali

na kuwapotosha Israeli watu wangu.

1423:14 Yer 5:30; Hos 6:10; Yer 29:23; Eze 13:22; Mt 11:24; Isa 1:9-10; Amo 4:11; Isa 5:18Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu

nimeona jambo baya sana:

Wanafanya uzinzi

na kuenenda katika uongo.

Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,

kwa ajili hiyo hakuna yeyote

anayeachana na uovu wake.

Wote wako kama Sodoma kwangu;

watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”

1523:15 Yer 8:14; 9:15; 8:10Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo kuhusu manabii:

“Nitawafanya wale chakula kichungu

na kunywa maji yaliyotiwa sumu,

kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu

kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.”

1623:16 Yer 27:9-14; Mt 7:15; Mit 19:27; Eze 13:3; Yer 14:14; 9:20Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Msisikilize wanachowatabiria manabii,

wanawajaza matumaini ya uongo.

Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,

hayatoki katika kinywa cha Bwana.

1723:17 Yer 13:10; 8:11; Amo 9:10; Mik 3:11; 1Fal 22:8; Yer 4:10; 5:12Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,

Bwana asema: Mtakuwa na amani.’

Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,

wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’

1823:18 1Fal 22:19; Rum 11:34Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Bwana

ili kuona au kusikia neno lake?

Ni nani aliyesikiliza

na kusikia neno lake?

1923:19 Isa 30:30; Yer 30:23; 25:32; Zek 7:14Tazama, dhoruba ya Bwana

itapasuka kwa ghadhabu,

kisulisuli kitazunguka na kuanguka

vichwani vya waovu.

2023:20 2Fal 23:26-27; Yer 30:24; 4:28Hasira ya Bwana haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.

Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi.

2123:21 Yer 14:14; 27:15Mimi sikuwatuma manabii hawa,

lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.

Mimi sikusema nao,

lakini wametabiri.

2223:22 2Fal 17:13; Kum 33:10; 2Fal 17:13; Yer 25:5; Amo 3:7Lakini kama wangesimama barazani mwangu,

wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,

nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya

na kutoka matendo yao maovu.”

2323:23 Za 139:1-10; 1Fal 20:23-28“Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”

Bwana asema,

“wala si Mungu aliyeko pia mbali?

2423:24 Ay 11:20; 1Fal 8:27; Ebr 4:13; Mwa 3:8; Ay 22:12-14; Mhu 12:14; Isa 28:15; 1Kor 4:5Je, mtu yeyote aweza kujificha

mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”

Bwana asema.

“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”

Bwana asema.

2523:25 Yer 14:14; 27:10; 29:8; Kum 13:1“Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ 2623:26 Isa 30:10; 1Tim 4:1-2; Eze 13:2; Yer 14:14Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe? 2723:27 Kum 13:13; Yer 29:8; Amu 3:7; 8:33-34; Mdo 13:8; Yer 2:23Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau jina langu kwa kumwabudu Baali. 2823:28 1Sam 3:17Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema Bwana. 2923:29 Za 39:3; 1Kor 3:13; 1Pet 4:10; Yer 5:14; Ebr 4:12“Je, neno langu si kama moto,” asema Bwana, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?

3023:30 Za 34:16; Kum 18:20; Yer 21:13; 14:15“Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asema Bwana. 31“Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘Bwana asema.’ 3223:32 Mao 2:14; Sef 3:4; Yer 7:8; 50:6; Ay 13:4; Eze 13:3; 22:28; Yer 14:14Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asema Bwana. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo,” asema Bwana.

Maneno Ya Uongo Na Manabii Wa Uongo

3323:33 2Fal 21:14; Yer 17:15; Mal 1:1“Wakati watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo wa Bwana ni nini?’ wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asema Bwana.’ 3423:34 Mao 2:14; Zek 13:3Nabii, kuhani, au mtu yeyote akisema, ‘Huu ndio mzigo wa Bwana,’ nitamwadhibu huyo na nyumba yake. 3523:35 Yer 33:3; 42:4Hivyo mnaambiana kila mmoja na mwenzake, au kwa mtu wa nyumba yao: ‘Bwana amejibu nini?’ au ‘Bwana amesema nini?’ 3623:36 Gal 1:7-8; 2Pet 3:16; Yos 3:10Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa Bwana,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu. 37Hivi ndivyo utakavyoendelea kumuuliza nabii: ‘Bwana amekujibu nini?’ au ‘Je, Bwana amesema nini?’ 38Ingawa unadai, ‘Huu ndio mzigo wa Bwana,’ hili ndilo Bwana asemalo: Ulitumia maneno, ‘Huu ndio mzigo wa Bwana,’ hata ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni mzigo wa Bwana.’ 3923:39 Yer 7:15Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutupa mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu. 4023:40 Yer 20:11; Eze 5:14-15Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu: yaani aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”