Yeremia 20 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 20:1-18

Yeremia Ateswa Na Pashuri

120:1 1Nya 24:14; 2Fal 25:18; Lk 22:52Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu la Bwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya, 220:2 Kum 25:2-3; 2Kor 11:24; Ay 13:27; Zek 14:10; Ay 29:7; Yer 15:15; 37:15; 29:26; Mdo 16:24; Ebr 11:36akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa kwenye mkatale katika Lango la Juu la Benyamini huko Hekaluni la Bwana. 3Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwana hakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.20:3 Magor-Misabibu maana yake hapa ni Vitisho pande zote. 420:4 Ay 18:11; Yer 29:21; 25:9; 52:27; 39:9; 21:10; 13:19Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, na kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga. 520:5 2Fal 25:15; Yer 17:3; 3:24; 2Fal 20:17Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli. 620:6 Yer 14:15; Mao 2:14; Yer 28:15Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”

Malalamiko Ya Yeremia

720:7 Kut 5:23; 22:16; Isa 8:11; 1Kor 9:16; Ay 12:4Ee Bwana, umenidanganya,

nami nikadanganyika;

wewe una nguvu kuniliko,

nawe umenishinda.

Ninadharauliwa mchana kutwa,

kila mmoja ananidhihaki.

820:8 Yer 28:8; 2Nya 36:16; Yer 6:7-10Kila ninenapo, ninapiga kelele

nikitangaza ukatili na uharibifu.

Kwa hiyo neno la Bwana limeniletea matukano

na mashutumu mchana kutwa.

920:9 Za 39:3; Yer 4:19; Amo 3:8; Mdo 4:20; 18:5; Yer 44:16Lakini kama nikisema, “Sitamtaja

wala kusema tena kwa jina lake,”

neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,

moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.

Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;

kweli, siwezi kujizuia.

1020:10 Yer 6:25; Neh 6:6-13; Ay 19:14; Lk 11:54; Za 57:4Ninasikia minongʼono mingi,

“Hofu iko pande zote!

Mshtakini! Twendeni tumshtaki!”

Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,

wakisema,

“Labda atadanganyika;

kisha tutamshinda

na kulipiza kisasi juu yake.”

1120:11 Rum 8:31; Yer 15:15; 17:18; 23:40; 7:19; Za 129:2Lakini Bwana yu pamoja nami

kama shujaa mwenye nguvu;

hivyo washtaki wangu watajikwaa

na kamwe hawatashinda.

Watashindwa, nao wataaibika kabisa;

kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

1220:12 Yer 17:10; Za 54:7; Rum 12:19; Za 62:8; Yer 11:20; Za 7:9; Kum 32:35Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

wewe umjaribuye mwenye haki

na kupima moyo na nia,

hebu nione ukilipiza kisasi juu yao,

kwa maana kwako

nimeliweka shauri langu.

1320:13 Za 35:10; Yak 2:5-6; Isa 12:6; Za 34:6; 97:10Mwimbieni Bwana!

Mpeni Bwana sifa!

Yeye huokoa uhai wa mhitaji

kutoka mikononi mwa waovu.

1420:14 Yer 15:10; Ay 3:8, 16Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

Nayo isibarikiwe ile siku

mama yangu aliyonizaa!

15Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

“Mtoto amezaliwa kwako,

tena mtoto wa kiume!”

1620:16 Mwa 19:25; Yer 18:22; 6:26Mtu huyo na awe kama miji ile

ambayo Bwana Mungu

aliiangamiza bila huruma.

Yeye na asikie maombolezo asubuhi

na kilio cha vita adhuhuri.

1720:17 Ay 3:10-16; 10:18-19Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

nalo tumbo lake la uzazi

lingebaki kuwa kubwa daima.

1820:18 1Fal 19:4; Za 102:3; Ay 3:20; 3:10-11; Mhu 4:2; Mwa 3:17; Ay 5:7; Za 90:9Kwa nini basi nilitoka tumboni

ili kuona taabu na huzuni,

na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

耶利米书 20:1-18

耶利米受迫害

1音麦的儿子巴施户珥祭司在耶和华的殿中做总管。他听见耶利米预言这些事, 2便叫人殴打耶利米先知,用枷锁把他锁在耶和华殿的便雅悯上门处。 3第二天,他打开枷锁释放了耶利米耶利米对他说:“耶和华不再叫你巴施户珥,要叫你玛歌珥·米撒毕20:3 “玛歌珥·米撒毕”意思是“四面有恐怖”。4因为耶和华说,‘我要使你和你的朋友都惊慌失措,让你亲眼看见你的朋友死在敌人刀下。我要把犹大人都交在巴比伦王手中,使他们或被掳到巴比伦或死于刀下。 5我要把这城里所有的财富、出产、珍宝,甚至犹大列王的宝物都交给敌人,带到巴比伦作战利品。 6巴施户珥和你所有的家人,以及听你说假预言的朋友都要被掳到巴比伦,死在那里,葬在那里。’”

耶利米的抱怨

7耶和华啊,

你欺骗我,我被你骗了。

你制服我,胜过我。

如今,我终日被嘲笑,人人戏弄我。

8我每次说预言,都大声疾呼:

“暴力和毁灭要来了!”

我因传讲耶和华的话而终日遭受侮辱和讥笑。

9有时我打算不再提起耶和华,

不再奉祂的名宣讲,

但祂的话如一团火在我心中燃烧,

憋在我骨头里,

我无法隐忍,不得不说。

10我听见许多人窃窃私语,

恐怖四下弥漫。

他们说:“我们告发他!告发他!”

我的好友都盼着我灭亡,说:

“或许他会受骗,

那样我们便能打倒他,

一泄心头之恨。”

11但耶和华与我同在,

祂像勇猛的战士。

所以迫害我的人必一败涂地,

他们因失败而羞愧难当,留下永远的耻辱。

12考验义人、洞悉人心的万军之耶和华啊,

求你让我看见你报应他们,

因为我已向你禀明案情。

13你们要歌颂耶和华!

要赞美耶和华!

因为祂从恶人手中救出穷人。

14愿我出生的那天受咒诅!

愿我母亲生我的那天不蒙祝福!

15愿那告诉我父亲喜得贵子、

使他欢喜的人受咒诅!

16愿那人像被耶和华无情毁灭的城!

愿他早晨听见哀鸣,

中午听见战争的呐喊,

17因为他没有把我杀死在母腹中,

没有使母腹成为我的坟墓,

让我永远留在里面。

18为什么我要从母胎出来,

经历患难和痛苦,

在羞辱中度过一生呢?