Yeremia 2 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 2:1-37

Israeli Amwacha Mungu

12:1 Isa 38:4; Eze 1:3Neno la Bwana lilinijia kusema, 22:2 Za 71:17; Eze 16:8; Kut 13:21; Hos 2:15; Ufu 2:4; Isa 54:4; Yer 3:4; Kum 1:29“Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu:

“ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako,

jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi

na kunifuata katika jangwa lile lote,

katika nchi isiyopandwa mbegu.

32:3 Kut 19:6; Yak 1:18; Kum 7:6; Law 23:9-14; Yer 10:25; Ufu 14:4; Yer 30:16; 50:7Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana,

kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake;

wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia,

nayo maafa yaliwakumba,’ ”

asema Bwana.

4Sikia neno la Bwana, ee nyumba ya Yakobo,

nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.

52:5 2Fal 17:15; Rum 1:21; Isa 44:9; Kum 32:21; 1Sam 12:21; Za 31:9Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu,

hata wakatangatanga mbali nami hivyo?

Walifuata sanamu zisizofaa,

nao wenyewe wakawa hawafai.

62:6 Hos 13:4; Kum 18:5; 32:10; Kut 6:6; Yer 51:43Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana,

aliyetupandisha kutoka Misri

na kutuongoza kupitia nyika kame,

kupitia nchi ya majangwa na mabonde,

nchi ya ukame na giza,

nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake

wala hakuna mtu aishiye humo?’

72:7 Hes 13:27; Kum 11:10-12; Za 106:34-39; Kum 8:7-9; Yer 7:30; 16:18; Eze 36:17Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu

ili mpate kula matunda yake

na utajiri wa mazao yake.

Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu,

na kuufanya urithi wangu chukizo.

82:8 2Sam 2:12; Rum 2:20; 1Fal 18:22; Yer 23:13; Isa 40:19; Yer 4:22; 3:15; 9:14Makuhani hawakuuliza,

‘Yuko wapi Bwana?’

Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi;

viongozi waliasi dhidi yangu.

Manabii walitabiri kwa jina la Baali,

wakifuata sanamu zisizofaa.

92:9 Isa 3:13; Mik 6:2; Eze 20:35-36; Yer 25:31“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,”

asema Bwana.

“Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.

102:10 Mwa 10:4; 25:13Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu2:10 Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania. nawe uangalie,

tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini,

uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.

112:11 Gal 4:8; Isa 37:19; Za 106:20; Rum 1:23; Kum 4:5-9; 1Sam 4:21; Yer 16:20Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote?

(Hata ingawa hao si miungu kamwe.)

Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao

kwa sanamu zisizofaa kitu.

12Shangaeni katika hili, ee mbingu,

nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”

asema Bwana.

132:13 Za 36:9; Yn 4:14; Yer 17:13; Kum 31:16; Isa 65:11; 12:3“Watu wangu wametenda dhambi mbili:

Wameniacha mimi,

niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,

nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,

visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.

142:14 Kut 4:22; Yer 31:9Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa?

Kwa nini basi amekuwa mateka?

152:15 Yer 4:7; 50:17; 2Fal 25:9; Law 26:43Simba wamenguruma;

wamemngurumia.

Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;

miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu.

162:16 Isa 19:13; Yer 43:7-9Pia watu wa Memfisi2:16 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. na Tahpanhesi2:16 Tahpanhesi ni mji katika nchi ya Misri.

wamevunja taji ya kichwa chako.

172:17 Yer 4:18; Isa 1:28; Yer 17:13; 19:4Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe

kwa kumwacha Bwana, Mungu wako

alipowaongoza njiani?

182:18 Isa 30:2; Hos 13:3; Eze 17:15; 2Fal 16:7; Hos 5:13; 7:11; Isa 7:20Sasa kwa nini uende Misri

kunywa maji ya Shihori?2:18 Kijito kinachoelekeza maji katika Mto Naili.

Nawe kwa nini kwenda Ashuru

kunywa maji ya Mto Frati?

192:19 Hos 14:4; Isa 59:12; Yer 14:7; Kut 19:5; Ay 20:14; Amo 8:10; Yer 3:11; 19:4Uovu wako utakuadhibu;

kurudi nyuma kwako kutakukemea.

Basi kumbuka, utambue

jinsi lilivyo ovu na chungu kwako

unapomwacha Bwana Mungu wako

na kutokuwa na hofu yangu,”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

202:20 Law 26:13; Yer 3:23; Kum 12:2; Yer 5:5; Ay 21:14; Isa 57:7; Eze 16:15; Isa 1:12“Zamani nilivunja nira yako

na kukatilia mbali vifungo vyako;

ukasema, ‘Sitakutumikia!’

Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu

na chini ya kila mti uliotanda matawi yake

ulijilaza kama kahaba.

212:21 Kut 15:17; Za 80:8; Mk 12:1; Isa 5:4Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana,

mkamilifu na wa mbegu nzuri.

Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami,

ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu?

222:22 Za 51:2; Ay 9:30; Mao 1:8, 17; Yer 17:1Hata ujisafishe kwa magadi

na kutumia sabuni nyingi,

bado doa la hatia yako liko mbele zangu,”

asema Bwana Mwenyezi.

232:23 Yer 23:27; Mwa 3:12-13; Rum 3:19; 2Fal 23:10; Yer 31:22; Mit 30:12; Yer 9:14“Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi,

sijawafuata Mabaali’?

Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni;

fikiri uliyoyafanya.

Wewe ni ngamia jike mwenye mbio

ukikimbia hapa na pale,

242:24 Mwa 16:12; Yer 14:6; Ay 39:6punda-mwitu aliyezoea jangwa,

anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa:

katika wakati wake wa kuhitaji mbegu

ni nani awezaye kumzuia?

Madume yoyote yanayomfuatilia

hayana haja ya kujichosha;

wakati wa kupandwa kwake watampata tu.

252:25 Isa 57:10; Kum 32:16; Yer 3:13; 14:10Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu,

na koo lako liwe limekauka.

Lakini ulisema, ‘Haina maana!

Ninaipenda miungu ya kigeni,

nami lazima niifuatie.’

26“Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa,

hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa:

wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao,

makuhani wao na manabii wao.

272:27 Yer 32:33; Eze 7:22; Isa 26:16; Yer 10:8; 9:3; 1Fal 14:9; 2Nya 29:9Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’

nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’

Wamenipa visogo vyao

wala hawakunigeuzia nyuso zao;

lakini wakiwa katika taabu, wanasema,

‘Njoo utuokoe!’

282:28 Isa 45:20; Kum 32:37; 2Fal 17:29; Isa 40:19Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea?

Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa

wakati mko katika taabu!

Kwa maana mna miungu mingi

kama mlivyo na miji, ee Yuda.

292:29 Dan 9:11; Mik 3:11; Yer 6:13; Mik 7:2“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu?

Ninyi nyote mmeniasi,”

asema Bwana.

302:30 Neh 9:26; 2Nya 36:16; Mdo 7:52; 1The 2:15; Yer 11:21; Law 26:23“Nimeadhibu watu wako bure tu,

hawakujirekebisha.

Upanga wako umewala manabii wako

kama simba mwenye njaa.

312:31 Isa 45:19; Ay 21:14“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana:

“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli

au nchi ya giza kuu?

Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,

hatutarudi kwako tena’?

32Je, mwanamwali husahau vito vyake,

au bibi arusi mapambo yake ya arusi?

Lakini watu wangu wamenisahau mimi,

tena kwa siku zisizo na hesabu.

33Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!

Hata wale wanawake wabaya kuliko wote

wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.

342:34 Yer 19:4; Mit 6:17; Kut 22:2; 2Fal 21:16Katika nguo zako watu huona

damu ya uhai ya maskini wasio na hatia,

ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.

Lakini katika haya yote

352:35 Mit 28:13; Eze 17:20; 2Sam 12:13; 1Yn 1:8-10; Mit 30:12; Isa 66:16; Yer 25:31unasema, ‘Sina hatia;

Mungu hajanikasirikia.’

Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema,

‘Mimi sijatenda dhambi.’

362:36 Yer 31:22; Hos 5:13; Za 108:12; Isa 30:2-7; Yer 37:7Kwa nini unatangatanga sana,

kubadili njia zako?

Utakatishwa tamaa na Misri

kama ulivyokatishwa na Ashuru.

372:37 2Sam 13:19; Yer 37:7Pia utaondoka mahali hapo

ukiwa umeweka mikono kichwani,

kwa kuwa Bwana amewakataa wale unaowatumainia;

hutasaidiwa nao.

New International Version

Jeremiah 2:1-37

Israel Forsakes God

1The word of the Lord came to me: 2“Go and proclaim in the hearing of Jerusalem:

“This is what the Lord says:

“ ‘I remember the devotion of your youth,

how as a bride you loved me

and followed me through the wilderness,

through a land not sown.

3Israel was holy to the Lord,

the firstfruits of his harvest;

all who devoured her were held guilty,

and disaster overtook them,’ ”

declares the Lord.

4Hear the word of the Lord, you descendants of Jacob,

all you clans of Israel.

5This is what the Lord says:

“What fault did your ancestors find in me,

that they strayed so far from me?

They followed worthless idols

and became worthless themselves.

6They did not ask, ‘Where is the Lord,

who brought us up out of Egypt

and led us through the barren wilderness,

through a land of deserts and ravines,

a land of drought and utter darkness,

a land where no one travels and no one lives?’

7I brought you into a fertile land

to eat its fruit and rich produce.

But you came and defiled my land

and made my inheritance detestable.

8The priests did not ask,

‘Where is the Lord?’

Those who deal with the law did not know me;

the leaders rebelled against me.

The prophets prophesied by Baal,

following worthless idols.

9“Therefore I bring charges against you again,”

declares the Lord.

“And I will bring charges against your children’s children.

10Cross over to the coasts of Cyprus and look,

send to Kedar2:10 In the Syro-Arabian desert and observe closely;

see if there has ever been anything like this:

11Has a nation ever changed its gods?

(Yet they are not gods at all.)

But my people have exchanged their glorious God

for worthless idols.

12Be appalled at this, you heavens,

and shudder with great horror,”

declares the Lord.

13“My people have committed two sins:

They have forsaken me,

the spring of living water,

and have dug their own cisterns,

broken cisterns that cannot hold water.

14Is Israel a servant, a slave by birth?

Why then has he become plunder?

15Lions have roared;

they have growled at him.

They have laid waste his land;

his towns are burned and deserted.

16Also, the men of Memphis and Tahpanhes

have cracked your skull.

17Have you not brought this on yourselves

by forsaking the Lord your God

when he led you in the way?

18Now why go to Egypt

to drink water from the Nile2:18 Hebrew Shihor; that is, a branch of the Nile?

And why go to Assyria

to drink water from the Euphrates?

19Your wickedness will punish you;

your backsliding will rebuke you.

Consider then and realize

how evil and bitter it is for you

when you forsake the Lord your God

and have no awe of me,”

declares the Lord, the Lord Almighty.

20“Long ago you broke off your yoke

and tore off your bonds;

you said, ‘I will not serve you!’

Indeed, on every high hill

and under every spreading tree

you lay down as a prostitute.

21I had planted you like a choice vine

of sound and reliable stock.

How then did you turn against me

into a corrupt, wild vine?

22Although you wash yourself with soap

and use an abundance of cleansing powder,

the stain of your guilt is still before me,”

declares the Sovereign Lord.

23“How can you say, ‘I am not defiled;

I have not run after the Baals’?

See how you behaved in the valley;

consider what you have done.

You are a swift she-camel

running here and there,

24a wild donkey accustomed to the desert,

sniffing the wind in her craving—

in her heat who can restrain her?

Any males that pursue her need not tire themselves;

at mating time they will find her.

25Do not run until your feet are bare

and your throat is dry.

But you said, ‘It’s no use!

I love foreign gods,

and I must go after them.’

26“As a thief is disgraced when he is caught,

so the people of Israel are disgraced—

they, their kings and their officials,

their priests and their prophets.

27They say to wood, ‘You are my father,’

and to stone, ‘You gave me birth.’

They have turned their backs to me

and not their faces;

yet when they are in trouble, they say,

‘Come and save us!’

28Where then are the gods you made for yourselves?

Let them come if they can save you

when you are in trouble!

For you, Judah, have as many gods

as you have towns.

29“Why do you bring charges against me?

You have all rebelled against me,”

declares the Lord.

30“In vain I punished your people;

they did not respond to correction.

Your sword has devoured your prophets

like a ravenous lion.

31“You of this generation, consider the word of the Lord:

“Have I been a desert to Israel

or a land of great darkness?

Why do my people say, ‘We are free to roam;

we will come to you no more’?

32Does a young woman forget her jewelry,

a bride her wedding ornaments?

Yet my people have forgotten me,

days without number.

33How skilled you are at pursuing love!

Even the worst of women can learn from your ways.

34On your clothes is found

the lifeblood of the innocent poor,

though you did not catch them breaking in.

Yet in spite of all this

35you say, ‘I am innocent;

he is not angry with me.’

But I will pass judgment on you

because you say, ‘I have not sinned.’

36Why do you go about so much,

changing your ways?

You will be disappointed by Egypt

as you were by Assyria.

37You will also leave that place

with your hands on your head,

for the Lord has rejected those you trust;

you will not be helped by them.