Yeremia 18 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 18:1-23

Katika Nyumba Ya Mfinyanzi

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 2“Shuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” 3Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. 4Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kama vile ilivyoonekana vyema kwake yeye.

5Kisha neno la Bwana likanijia kusema: 618:6 Isa 29:16; 45:9; Rum 9:20-21; Mwa 2:7“Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” asema Bwana. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli. 718:7 Yer 1:10Ikiwa wakati wowote nikitangaza kuwa taifa au ufalme utangʼolewa, utaangushwa na kuangamizwa, 818:8 Kut 32:14; Eze 18:21; Yn 3:8-10; Dan 9:14; Amu 10:15-16; Za 25:11; Yer 26:13; 31:28; 42:10; Hos 11:8-9; Yoe 2:13ikiwa lile taifa nililolionya litatubia uovu wake, ndipo nitakapokuwa na huruma, wala sitawapiga kwa maafa niliyokuwa nimewakusudia. 918:9 Yer 1:10; 31:28Ikiwa wakati mwingine nitatangaza kuwa taifa ama utawala ujengwe na kuwekwa wakfu, 1018:10 Eze 33:18; 1Sam 2:29-30; 13:13; Yer 1:10ikiwa utafanya maovu mbele zangu na hukunitii, ndipo nitakapoghairi makusudio yangu mema niliyokuwa nimeyakusudia.

1118:11 2Fal 22:16; Yer 4:6; Kum 4:30; 2Fal 17:13; Isa 1:16-19; Ay 16:17; Yer 7:3“Basi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Tazama! Ninaandaa maafa kwa ajili yenu, nami ninabuni mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka njia zenu mbaya, kila mmoja wenu, tengenezeni njia zenu na matendo yenu.’ 1218:12 Isa 57:10; Yer 2:25; 3:17Lakini wao watajibu, ‘Hakuna faida. Tutaendelea na mipango yetu wenyewe, kila mmoja wetu atafuata ukaidi wa moyo wake mbaya.’ ”

1318:13 Isa 66:8; Yer 2:10; 5:30; 2Fal 19:21Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:

“Ulizia miongoni mwa mataifa:

Ni nani alishasikia jambo kama hili?

Jambo la kutisha sana limefanywa

na Bikira Israeli.

14Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutoweka

kwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote?

Je, maji yake baridi yatokayo katika vyanzo vilivyo mbali

yaliwahi kukoma kutiririka wakati wowote?

1518:15 Yer 51:18; Hos 11:12; Yer 6:16; Isa 57:14; 62:10; 17:10; 1:13; Eze 44:12Lakini watu wangu wamenisahau mimi,

wanafukizia uvumba sanamu zisizofaa kitu,

zilizowafanya wajikwae katika njia zao

na katika mapito ya zamani.

Zimewafanya wapite kwenye vichochoro

na kwenye barabara ambazo hazikujengwa.

1618:16 Eze 33:28-29; Yer 49:13; 42:18; Ay 16:4; 2Fal 19:21; Kum 28:37; Yer 25:9Nchi yao itaharibiwa,

itakuwa kitu cha kudharauliwa daima;

wote wapitao karibu nayo watashangaa

na kutikisa vichwa vyao.

1718:17 Ay 7:10; Yer 13:24; 2Nya 29:6; Yer 2:27Kama upepo utokao mashariki,

nitawatawanya mbele ya adui zao;

nitawapa kisogo wala sio uso,

katika siku ya maafa yao.”

1818:18 Yer 11:19; Hag 2:11; Yer 5:13; Za 64:2-8; Yer 9:3; 2:8; Mao 2:7; Ay 5:13Wakasema, “Njooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.”

19Nisikilize, Ee Bwana,

sikia wanayosema washtaki wangu!

2018:20 Mwa 20:7; Kum 9:19; Za 119:85; 35:7; 109:23; Mwa 44:4; Yer 14:7-9Je, mema yalipwe kwa mabaya?

Lakini wao wamenichimbia shimo.

Kumbuka kwamba nilisimama mbele yako

na kunena mema kwa ajili yao,

ili wewe ugeuze hasira yako kali mbali nao.

2118:21 Yer 11:22; 14:16; 1Sam 15:33; Mao 5:3; Za 63:10; Isa 47:9; 9:17Kwa hiyo uwaache watoto wao waone njaa;

uwaache wauawe kwa makali ya upanga.

Wake zao wasiwe na watoto, na wawe wajane;

waume wao wauawe,

nao vijana wao waume

wachinjwe kwa upanga vitani.

2218:22 Yer 6:26; Za 35:15; Yer 5:26; Za 119:85; Yer 20:10Kilio na kisikike kutoka kwenye nyumba zao

ghafula uwaletapo adui dhidi yao,

kwa kuwa wamechimba shimo ili kunikamata

na wameitegea miguu yangu mitego.

2318:23 Yer 11:21; 37:15; Neh 4:5; Za 109:14; 59:5; Yer 10:24Lakini unajua, Ee Bwana,

hila zao zote za kuniua.

Usiyasamehe makosa yao

wala usifute dhambi zao

mbele za macho yako.

Wao na waangamizwe mbele zako;

uwashughulikie wakati wa hasira yako.