Yeremia 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 17:1-27

Dhambi Ya Yuda Na Adhabu Yake

117:1 Ay 19:24; 2Kor 3:3; Mit 3:3; Kum 6:6; Kut 27:2“Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma,

imeandikwa kwa ncha ya almasi,

kwenye vibao vya mioyo yao

na kwenye pembe za madhabahu zao.

217:2 2Nya 24:18; 2Fal 16:4; Yer 2:20Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao

na nguzo za Ashera,17:2 Ashera ni mungu mke aliyekuwa anaabudiwa na Wakanaani.

kandokando ya miti iliyotanda

na juu ya vilima virefu.

317:3 2Fal 24:13; Yer 15:13; Mik 3:12; Yer 26:18Mlima wangu katika nchi pamoja na utajiri

na hazina zako zote nitazitoa ziwe nyara,

pamoja na mahali pako pa juu pa kuabudia miungu

kwa sababu ya dhambi katika nchi yako yote.

417:4 Mao 5:2; Yer 12:7; 16:13; 22:28; 7:20; 15:14; Kum 28:48Kwa kosa lako mwenyewe utaupoteza

urithi niliokupa.

Nitakufanya mtumwa wa adui zako

katika nchi usiyoijua,

kwa kuwa umeiwasha hasira yangu,

nayo itawaka milele.”

517:5 Za 108:12; Isa 30:1-3; 2:22; 2Kor 1:9Hili ndilo asemalo Bwana:

“Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu,

ategemeaye mwenye mwili

kwa ajili ya nguvu zake,

ambaye moyo wake

umemwacha Bwana.

617:6 Kum 29:23; Za 107:34; Ay 20:17; 20:17; 30:3; 39:6; Yer 48:9Atakuwa kama kichaka cha jangwani;

hataona mafanikio yatakapokuja.

Ataishi katika sehemu zisizo na maji,

katika nchi ya chumvi ambapo

hakuna yeyote aishiye humo.

717:7 Mit 16:20; Za 146:5; 34:8; 40:4; Yer 39:18“Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika Bwana,

ambaye matumaini yake ni katika Bwana.

817:8 Yer 14:1-6; Eze 47:12; Ay 14:9; Za 92:12-14; Eze 19:10Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji

uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.

Hauogopi wakati wa joto ujapo;

majani yake ni mabichi daima.

Hauna hofu katika mwaka wa ukame

na hautaacha kuzaa matunda.”

917:9 Mhu 9:3; Mt 13:15; Mk 7:21-22Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote,

ni mwovu kupita kiasi.

Ni nani awezaye kuujua?

1017:10 Yos 22:22; Mit 17:3; Ufu 2:23; Eze 11:5; Rum 8:27; Za 62:12; Yer 32:19; Rum 2:6“Mimi Bwana huchunguza moyo

na kuzijaribu nia,

ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake,

kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”

1117:11 Lk 12:20Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga,

ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki.

Maisha yake yafikapo katikati, siku zitamwacha,

na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.

1217:12 Yer 3:17Kiti cha enzi kilichotukuzwa, kilichoinuliwa tangu mwanzo,

ndiyo sehemu yetu ya mahali patakatifu.

1317:13 Za 71:5; 73:27; Yer 14:8; 2:17; Za 69:28; Eze 13:9; Isa 12:3; Yn 4:10Ee Bwana, uliye tumaini la Israeli,

wote wakuachao wataaibika.

Wale wanaogeukia mbali nawe wataandikwa mavumbini

kwa sababu wamemwacha Bwana,

chemchemi ya maji yaliyo hai.

1417:14 Kut 15:2; Isa 30:26; Yer 15:18; Za 109:1; 119:94Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka;

uniokoe nami nitaokoka,

kwa maana wewe ndiwe ninayekusifu.

1517:15 Isa 5:19; Amo 5:18; 2Pet 3:4-5Wao huendelea kuniambia,

“Liko wapi neno la Bwana?

Sasa na litimie!”

16Sijakukimbia na kuacha kuwa mchungaji wako;

unajua sijaitamani siku ya kukata tamaa.

Kile kipitacho midomoni mwangu

ki wazi mbele yako.

1717:17 Za 88:15-16; 46:1; 18:18; Yer 16:19; Nah 1:7Usiwe kwangu kitu cha kunitia hofu kuu;

wewe ndiwe kimbilio langu katika siku ya maafa.

1817:18 Za 35:1-8; Isa 40:2; Yer 12:3Watesi wangu na waaibishwe,

lakini nilinde mimi nisiaibike;

wao na watiwe hofu kuu,

lakini unilinde mimi na hofu kuu.

Waletee siku ya maafa;

waangamize kwa maangamizi maradufu.

Kuiadhimisha Sabato

1917:19 Yer 7:2; 26:2Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Nenda ukasimame kwenye lango la watu, mahali ambako wafalme wa Yuda huingilia na kutokea, simama pia kwenye malango mengine yote ya Yerusalemu. 2017:20 Yer 19:3; 22:2; Za 49:1Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, nanyi watu wote wa Yuda, na kila mmoja aishiye Yerusalemu apitaye katika malango haya. 2117:21 Kum 5:14; Yn 5:10; Neh 13:15-21; Hes 15:32-36Hili ndilo asemalo Bwana: Jihadharini msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, wala kuingiza mzigo kupitia malango ya Yerusalemu. 2217:22 Eze 20:12; Kut 20:8; Mwa 2:3; Isa 56:2-6Msitoe mizigo nje ya nyumba zenu wala kufanya kazi yoyote wakati wa Sabato, lakini itakaseni siku ya Sabato, kama nilivyowaamuru baba zenu. 2317:23 Yer 7:26; 19:15; 2Nya 28:22; Zek 7:11; Yer 7:28Hata hivyo hawakusikiliza wala kujali, walishupaza shingo zao, na hawakutaka kusikia wala kukubali adhabu. 24Lakini mkiwa waangalifu kunitii, asema Bwana, nanyi msipoleta mzigo wowote kupitia malango ya mji huu wakati wa Sabato, lakini mkaitakasa siku ya Sabato kwa kutofanya kazi siku hiyo, 2517:25 2Sam 7:13; Lk 1:32; Yer 22:2; 30:10; 33:19; Isa 6:6-7; Eze 28:26ndipo wafalme wakaao juu ya kiti cha enzi cha Daudi wataingia kupitia malango ya mji huu, pamoja na maafisa wao. Wao na maafisa wao watakuja wakiwa wamepanda magari na farasi, wakiandamana na watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, nao mji huu utakaliwa na watu daima. 2617:26 Yer 33:14; Zek 7:7; Yer 32:44Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na chini ya vilima vya magharibi, kutoka nchi ya vilima na Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na dhabihu, sadaka za nafaka, uvumba na sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Bwana. 2717:27 Yer 22:5; 7:20; Hos 8:14; Amo 2:5; Neh 10:31; 2Fal 25:9; 1Fal 9:6Lakini ikiwa hamtanitii mimi kwa kuitakasa Sabato na kwa kutochukua mzigo wowote mnapoingia katika malango ya Yerusalemu wakati wa Sabato, basi nitawasha moto usiozimika katika malango ya Yerusalemu utakaoteketeza ngome zake.’ ”