Yeremia 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 15:1-21

Adhabu Isiyoepukika

115:1 Kut 32:11; Hes 14:13-20; 1Sam 7:9; Eze 14:14, 20; 2Fal 17:20; Yer 16:13; 7:16Kisha Bwana akaniambia: “Hata kama Mose na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende! 215:2 Yer 42:22; 44:13; Zek 11:9; Mao 4:9; Eze 12:11; Ufu 13:10; Yer 14:12Nao kama wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe;

waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga;

waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa:

waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ”

315:3 Law 26:16; Hes 33:4; Kum 28:26; Eze 33:27; 14:21; 2Fal 9:36; 1Fal 21:19Bwana asema, “Nitatuma aina nne za waharabu dhidi yao: nazo ni upanga ili kuua na mbwa ili wakokote mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili kula na kuangamiza. 415:4 Eze 23:46; Yer 29:18; 34:17; Ay 17:6; 2Fal 21:2, 11; 23:26-27; Yer 24:9Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu.

515:5 Isa 27:11; Nah 3:7; Isa 51:19; Yer 13:14; 16:13; 21:7“Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu?

Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako?

Ni nani atakayesimama ili kuuliza

kuhusu hali yako?

615:6 Kum 32:15; Yer 6:19; Isa 31:3; Hos 13:14; Yer 7:20; Amo 7:8Umenikataa mimi,” asema Bwana.

“Unazidi kukengeuka.

Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza,

siwezi kuendelea kukuonea huruma.

715:7 Isa 9:13; Yer 18:21; Isa 41:16; 3:26; 2Nya 28:22Nitawapepeta kwa uma wa kupepetea

kwenye malango ya miji katika nchi.

Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu,

kwa maana hawajabadili njia zao.

815:8 Isa 47:9; Yer 6:4; Ay 18:11Nitawafanya wajane wao kuwa wengi

kuliko mchanga wa bahari.

Wakati wa adhuhuri nitamleta mharabu

dhidi ya mama wa vijana wao waume;

kwa ghafula nitaleta juu yao

maumivu makuu na hofu kuu.

915:9 1Sam 2:5; Yer 21:7; 25:31; 7:19; Amo 8:9; 2Fal 25:7; Yer 19:7Mama mwenye watoto saba atazimia

na kupumua pumzi yake ya mwisho.

Jua lake litatua kungali bado mchana,

atatahayarika na kufedheheka.

Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga

mbele ya adui zao,”

asema Bwana.

1015:10 Ay 10:18-19; Law 25:36; Neh 5:1-12; Ay 3:1; Yer 6:10; 1:19Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa,

mtu ambaye ulimwengu wote

unashindana na kugombana naye!

Sikukopa wala sikukopesha,

lakini kila mmoja ananilaani.

1115:11 Yer 40:4; 37:3; 42:1-3; 21:1-2Bwana akasema,

“Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema,

hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaada

nyakati za maafa na nyakati za dhiki.

1215:12 Mao 1:14; Hos 10:11; Kum 28:48; Yer 28:14“Je, mtu aweza kuvunja chuma,

chuma kitokacho kaskazini, au shaba?

1315:13 Yer 17:3; Za 44:12; Eze 38:12-13; 2Fal 24:13; 25:15Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara,

bila gharama,

kwa sababu ya dhambi zako zote

katika nchi yako yote.

1415:14 Kum 28:36; Yer 16:13; Kum 32:22; Za 21:9; Yer 5:19Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zako

katika nchi usiyoijua,

kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwa

utakaowaka juu yako daima.”

1515:15 Yn 21:15-17; Yer 12:3; Za 69:7-9; 119:84; 44:22; Kut 34:6Wewe unafahamu, Ee Bwana,

unikumbuke na unitunze mimi.

Lipiza kisasi juu ya watesi wangu.

Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali;

kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa.

1615:16 Ay 23:12; 15:11; Eze 2:8; Ufu 10:10; Za 119:72, 103; Yer 14:9; Isa 43:7Maneno yako yalipokuja, niliyala;

yakawa shangwe yangu

na furaha ya moyo wangu,

kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako,

Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

1715:17 Rut 3:3; Za 26:4-5; Yer 16:8; 2Fal 3:15Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe,

wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao;

niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu,

na wewe ulikuwa umenijaza hasira.

1815:18 Mik 1:9; Ay 6:4; Za 9:10Kwa nini maumivu yangu hayakomi,

na jeraha langu ni la kuhuzunisha,

wala haliponyeki?

Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu,

kama chemchemi iliyokauka?

1915:19 Zek 3:7; Eze 22:26; Kut 4:16Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:

“Kama ukitubu, nitakurejeza

ili uweze kunitumikia;

kama ukinena maneno yenye maana,

wala si ya upuzi,

utakuwa mnenaji wangu.

Watu hawa ndio watakaokugeukia,

wala si wewe utakayewageukia wao.

2015:20 Yer 42:11; Eze 3:8; Isa 50:7; Za 129:2; Yer 20:11Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa,

ngome ya ukuta wa shaba;

watapigana nawe

lakini hawatakushinda,

kwa maana mimi niko pamoja nawe

kukuponya na kukuokoa,”

asema Bwana.

2115:21 Yer 50:34; Mwa 48:16; Isa 49:25; Yer 1:8; Za 97:10“Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu,

na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.”