Yeremia 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 14:1-22

Ukame, Njaa Na Upanga

1Hili ndilo neno la Bwana kwa Yeremia kuhusu ukame:

214:2 Isa 3:26; Yer 8:21; Mit 21:13“Yuda anaomboleza,

miji yake inayodhoofika;

wanaomboleza kwa ajili ya nchi,

nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu.

314:3 Kum 28:48; 2Fal 18:31; 2Sam 15:30; Es 6:12; Ay 6:19-20Wakuu wanawatuma watumishi wao maji;

wanakwenda visimani

lakini humo hakuna maji.

Wanarudi na vyombo bila maji;

wakiwa na hofu na kukata tamaa,

wanafunika vichwa vyao.

414:4 Amo 4:8; Zek 14:17; Yer 3:3; 12:11Ardhi imepasuka nyufa

kwa sababu hakuna mvua katika nchi;

wakulima wana hofu

na wanafunika vichwa vyao.

514:5 Isa 15:6Hata kulungu mashambani

anamwacha mtoto wake aliyezaliwa wakati huo huo

kwa sababu hakuna majani.

614:6 Ay 39:5-6; Yer 2:24; Za 104:11; Mwa 47:4Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kame

na kutweta kama mbweha;

macho yao yanakosa nguvu za kuona

kwa ajili ya kukosa malisho.”

714:7 Isa 3:9; Hos 5:5; Yer 2:19; 8:14; Za 25:11; 79:9; 1Sam 12:22Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu,

Ee Bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako.

Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa,

nasi tumetenda dhambi dhidi yako.

814:8 Za 9:18; Mdo 28:20; Yer 17:13; 50:7; Za 18:46; Isa 25:9Ee Tumaini la Israeli,

Mwokozi wake wakati wa taabu,

kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi,

kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu?

914:9 Isa 50:2; Mwa 17:7; Yer 8:19; 15:16; Kut 29:45; Isa 63:19; Za 27:9Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa,

kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa?

Wewe uko katikati yetu, Ee Bwana,

nasi tunaitwa kwa jina lako;

usituache!

1014:10 Yer 2:25; Za 119:101; Yer 6:20; Hes 8:13; Ebr 8:12; Amo 5:22; Hos 7:2; 9:9; Yer 44:21Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa:

“Wanapenda sana kutangatanga,

hawaizuii miguu yao.

Hivyo Bwana hawakubali;

sasa ataukumbuka uovu wao

na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.”

1114:11 Kut 32:10; 1Sam 2:25Kisha Bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. 1214:12 Kum 1:45; 1Sam 8:18; Yer 7:21; Law 1:1-17; Yer 11:11; Amo 5:22; Isa 51:19; Yer 9:16Ingawa wanafunga, sitasikiliza kilio chao; hata wakitoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za nafaka, sitazikubali. Badala yake, nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.”

13Lakini nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’ ”

1414:14 Yer 23:25; 2The 2:9-11; Eze 13:2-6; Yer 23:16; Mao 2:9; Eze 12:24; Yer 27:14Ndipo Bwana akaniambia, “Manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwatuma, wala sikuwaweka, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi, maono ya sanamu zisizofaa kitu, na madanganyo ya mawazo yao wenyewe. 1514:15 Yer 20:6; Eze 14:9; Yer 16:4; Mao 1:19; Yer 23:15; 5:12-13Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo kuhusu manabii wanaotabiri kwa jina langu: Mimi sikuwatuma, lakini wanasema, ‘Hakuna upanga wala njaa itakayoigusa nchi hii.’ Manabii hao hao watakufa kwa upanga na njaa. 1614:16 Yer 17:10; Mit 1:31; Yer 7:33; Za 79:3; Mt 15:14Nao watu hao wanaowatabiria watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga. Hapatakuwepo yeyote wa kuwazika wao au wake zao, wana wao au binti zao. Nitawamwagia maafa wanayostahili.

1714:17 Za 119:136; Yer 8:21; Mao 1:16; 2Fal 19:21; Yer 23:12“Nena nao neno hili:

“ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi

usiku na mchana bila kukoma;

kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu,

amepata jeraha baya,

pigo la kuangamiza.

1814:18 Eze 7:14-15; 2Nya 36:10; Yer 13:17Kama nikienda mashambani,

ninaona wale waliouawa kwa upanga;

kama nikienda mjini,

ninaona maangamizi ya njaa.

Nabii na kuhani kwa pamoja

wamekwenda katika nchi wasiyoijua.’ ”

1914:19 Yer 7:29; 30:12-13; 8:15; Isa 1:6Je, umemkataa Yuda kabisa?

Umemchukia Sayuni kabisa?

Kwa nini umetuumiza

hata hatuwezi kuponyeka?

Tulitarajia amani,

lakini hakuna jema lililotujia;

tulitarajia wakati wa kupona

lakini kuna hofu kuu tu.

2014:20 Amu 10:10; Dan 9:7-8; Yer 3:13; Law 26:40; 1Fal 8:47; Ezr 9:6Ee Bwana, tunatambua uovu wetu

na kosa la baba zetu;

kweli tumetenda dhambi dhidi yako.

2114:21 Yer 17:12; Yos 7:9; Isa 62:7; Yer 3:17; Kut 2:24Kwa ajili ya jina lako usituchukie kabisa;

usikidharau kiti chako cha enzi kilichotukuka.

Kumbuka agano lako nasi

na usilivunje.

2214:22 1Fal 8:36; Isa 30:23; Za 135:7; Isa 41:24; 44:10; Yer 10:15Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifa

iwezayo kuleta mvua?

Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua?

La hasha, ni wewe peke yako,

Ee Bwana, Mungu wetu.

Kwa hiyo tumaini letu liko kwako,

kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.