Yeremia 12 – NEN & NVI

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 12:1-17

Lalamiko La Yeremia

112:1 Ay 8:3; 12:6; Dan 9:14; Ay 21:7, 13; Ezr 9:15; Ay 5:8; Eze 18:25; Yer 5:27-28Wewe daima u mwenye haki, Ee Bwana,

niletapo mashtaka mbele yako.

Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako:

Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa?

Kwa nini wasio waaminifu

wote wanaishi kwa raha?

212:2 Isa 29:13; Eze 22:27; Yer 11:17; Mk 7:6; Ay 5:3; Yer 3:10; Mt 15:8; Tit 1:16Umewapanda, nao wameota,

wanakua na kuzaa matunda.

Daima u midomoni mwao,

lakini mbali na mioyo yao.

312:3 Yer 17:18; Za 7:9; 11:5; Yer 20:11; 16:18Hata hivyo unanijua mimi, Ee Bwana;

unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe.

Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa!

Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!

412:4 Yer 4:25-28; Yoe 1:10-12; Kum 28:15-18; Za 107:34; Yer 4:26; 9:10Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini,

na majani katika kila shamba kunyauka?

Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu,

wanyama na ndege wameangamia.

Zaidi ya hayo, watu wanasema,

Bwana hataona yatakayotupata sisi.”

Jibu La Mungu

512:5 Yer 49:19; 50:44“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda,

unawezaje kushindana na farasi?

Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama,

utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani?

612:6 Mit 26:24-25; Yer 9:4; Za 12:2Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe:

hata wao wamekusaliti;

wameinua kilio kikubwa dhidi yako.

Usiwaamini, ingawa wanazungumza

mema juu yako.

7“Nitaiacha nyumba yangu,

nitupe urithi wangu;

nitamtia yeye nimpendaye

mikononi mwa adui zake.

812:8 Amo 6:8; 2Nya 36:16; Za 17:12; Hos 9:15Urithi wangu umekuwa kwangu

kama simba wa msituni.

Huningurumia mimi,

kwa hiyo ninamchukia.

912:9 Kum 28:26; Isa 56:9; Yer 15:3; Eze 23:25; 39:17-20Je, urithi wangu haukuwa

kama ndege wa mawindo wa madoadoa

ambaye ndege wengine wawindao

humzunguka na kumshambulia?

Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni;

walete ili wale.

1012:10 Yer 25:34; Eze 33:2; Isa 5:1-7; Yer 9:10; 25:11Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu

na kulikanyaga shamba langu;

watalifanya shamba langu zuri

kuwa jangwa la ukiwa.

1112:11 Isa 42:25; Yer 23:10; Isa 5:6; 24:4; Yer 9:12; 14:4Litafanywa kuwa jangwa,

lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu;

nchi yote itafanywa jangwa

kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali.

1212:12 Kum 32:41; Eze 33:2; Yer 3:2; Eze 21:3-4; Isa 31:8; Yer 46:10; Eze 14:17Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani

mharabu atajaa,

kwa maana upanga wa Bwana utawala,

kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine;

hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

1312:13 Mik 6:15; Kut 15:7; Yer 4:26; Law 26:16-20; Kum 28:38Watapanda ngano lakini watavuna miiba;

watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote.

Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako

kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”

1412:14 Zek 2:7-9; Sef 2:8-10; Yer 32:37; 2Nya 7:20; Za 9:6; Kum 29:28Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa habari ya majirani zangu wote wabaya wanaonyangʼanya urithi ambao ninawapa watu wangu Israeli, nitawangʼoa kutoka nchi zao, nami nitaingʼoa nyumba ya Yuda kutoka katikati yao. 1512:15 Kum 30:3; Amo 9:14-15; Eze 28:25; Za 6:2Lakini baada ya kuwangʼoa, nitawahurumia tena na kumrudisha kila mmoja wao kwenye urithi wake mwenyewe na kwenye nchi yake mwenyewe. 1612:16 Yer 4:2; Yos 23:7; Efe 2:20; Isa 26:18; 49:6; Yer 18:8; 3:17Ikiwa watajifunza vyema njia za watu wangu na kuapa kwa Jina langu, wakisema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo,’ hata kama wakati fulani walifundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapofanywa imara katikati ya watu wangu. 1712:17 Mwa 27:29; Isa 60:12; Za 2:8-9Lakini kama taifa lolote halitasikiliza na kutii, nitalingʼoa kabisa na kuliangamiza,” asema Bwana.

Nueva Versión Internacional

Jeremías 12:1-17

Queja de Jeremías

1Tú, Señor, eres justo

cuando argumento contigo.

Sin embargo, quisiera exponerte algunas cuestiones de justicia.

¿Por qué prosperan los malvados?

¿Por qué viven tranquilos los traidores?

2Tú los plantas, ellos echan raíces,

crecen y dan fruto.

Te tienen a flor de labio,

pero estás lejos de su corazón.

3A mí, Señor, tú me conoces;

tú me ves y has examinado mi corazón para contigo.

Arrástralos, como ovejas al matadero;

apártalos para el día de la matanza.

4¿Hasta cuándo estará seca la tierra,

y marchita la hierba de todos los campos?

Los animales y las aves se mueren

por la maldad de los que habitan el país,

quienes se atreven a decir:

«Dios no verá nuestro fin».

Respuesta de Dios

5«Si corriste con los de a pie

e hicieron que te cansaras,

¿cómo competirás con los caballos?

Si tropiezas en una tierra tranquila,

¿qué harás en la espesura del Jordán?

6Aun tus hermanos, los de tu propia familia,

te han traicionado

y gritan contra ti.

Por más que te digan cosas agradables,

no confíes en ellos.

7»He abandonado mi casa,

he rechazado mi herencia,

he entregado al amor de mi vida

en poder de sus enemigos.

8Mi heredad se ha comportado conmigo

como león en la selva.

Lanza rugidos contra mí;

por eso la aborrezco.

9Mi heredad es para mí

como un ave de muchos colores

acosada por las aves de rapiña.

¡Vayan y reúnan a todos los animales salvajes!

¡Tráiganlos para que la devoren!

10Muchos pastores han destruido mi viña,

han pisoteado mi terreno;

han hecho de mi hermosa parcela

un desierto desolado.

11La han dejado en ruinas,

seca y desolada ante mis ojos;

todo el país ha sido arrasado

porque a nadie le importa.

12Sobre todas las lomas desoladas

vinieron depredadores.

La espada del Señor destruirá el país

de un extremo al otro

y nadie estará seguro.

13Sembraron trigo y cosecharon espinos;

¡de nada valió su esfuerzo!

Por causa de la ardiente ira del Señor

se avergonzarán de sus cosechas».

14Así dice el Señor: «En cuanto a todos los vecinos malvados que tocaron la heredad que di a mi pueblo Israel, los arrancaré de sus tierras y a la tribu de Judá la quitaré de en medio de ellos. 15Después que los haya desarraigado, volveré a tener compasión de ellos; los haré regresar, cada uno a su heredad y a su propia tierra. 16Y, si aprenden bien los caminos de mi pueblo y, si así como enseñaron a mi pueblo a jurar por Baal, aprenden a jurar por mi nombre y dicen: “Tan cierto como el Señor vive”, entonces serán establecidos en medio de mi pueblo. 17Pero a la nación que no obedezca, la desarraigaré por completo y la destruiré», afirma el Señor.