Yeremia 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 11:1-23

Agano Limevunjwa

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 2“Sikia maneno ya agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu. 311:3 Kum 11:26-28; 27:26; Gal 3:10; Kum 28:15-68Waambie kwamba hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili, 411:4 Law 26:3; Kum 4:20; 1Fal 8:51; Kut 24:8; Yer 7:23; Eze 11:20maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, kutoka tanuru la kuyeyushia vyuma.’ Nilisema, ‘Nitiini mimi na mfanye kila kitu ninachowaamuru, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. 511:5 Kum 7:12; Kut 6:8; 13:5; Za 105:8-11; Kut 3:8; Kum 27:26Kisha nitatimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali,’ nchi ambayo mnaimiliki leo.”

Nikajibu, “Amen, Bwana.”

611:6 Kut 15:26; Yn 13:17; Rum 2:13; Yak 1:22; Yer 4:5; Kum 15:5Bwana akaniambia, “Tangaza maneno haya yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu: ‘Sikilizeni maneno ya agano hili na kuyafuata. 711:7 2Nya 36:15Tangu wakati ule niliwapandisha baba zenu kutoka Misri mpaka leo, niliwaonya tena na tena, nikisema “Nitiini mimi.” 811:8 Yer 7:26; Law 26:14-43; Yos 23:15; Mhu 9:3; Yer 3:17; 2Nya 7:19; Za 78:10Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Hivyo nikaleta juu yao laana zote za agano nililokuwa nimewaamuru wao kulifuata, lakini wao hawakulishika.’ ”

911:9 Hos 6:9; Eze 1:28; 22:25Kisha Bwana akaniambia, “Kuna shauri baya linaloendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu. 1011:10 Eze 20:18; Kum 9:7; 2Nya 30:7; Amu 2:11-13; 10:13; Zek 7:11; Yer 16:11; 34:18Wamerudia dhambi za baba zao, waliokataa kusikiliza maneno yangu. Wameifuata miungu mingine kuitumikia. Nyumba zote mbili za Israeli na Yuda zimelivunja agano nililofanya na baba zao. 1111:11 Eze 8:8-18; Ay 27:9; Za 66:18; 2Fal 22:16; Zek 7:13; Ay 11:20; Yer 14:12Kwa hivyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitaleta juu yao maafa ambayo hawawezi kuyakimbia. Hata kama wakinililia, sitawasikiliza. 1211:12 Kum 32:37-38; Amu 10:14; Yer 44:17; Isa 45:20Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu watakwenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga. 1311:13 Yer 44:21; 3:24; Kut 20:3; Yer 19:4; 2Fal 17:29; Yer 7:9Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’

1411:14 Kut 32:10; Yer 7:16“Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao.

1511:15 Eze 16:25; Hag 2:12; Yer 7:9-10“Mpenzi wangu anafanya nini hekaluni mwangu,

anapofanya mashauri yake maovu na wengi?

Je, nyama iliyowekwa wakfu yaweza

kuondolea mbali adhabu yako?

Unapojiingiza katika ubaya wako,

ndipo unashangilia.”

1611:16 Yer 7:20; 21:14; Rum 11:17-24; Hos 14:6; Isa 27:11Bwana alikuita mti wa mzeituni uliostawi

ulio na matunda mazuri kwa sura.

Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuu

atautia moto,

nayo matawi yake yatavunjika.

1711:17 Kut 15:17; Isa 5:2; Yer 7:9; 12:2; 7:18Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.

Shauri Baya Dhidi Ya Yeremia

18Kwa sababu Bwana alinifunulia hila zao mbaya, nilizifahamu, kwa kuwa wakati ule alinionyesha yale waliyokuwa wanayafanya. 1911:19 Za 54:3; Yer 20:10; Ay 28:13; Za 83:4; 44:22; Yer 18:18; Ay 28:13; Isa 53:8Nilikuwa kama mwana-kondoo mpole aliyeongozwa machinjoni; mimi sikutambua kwamba walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yangu, wakisema,

“Sisi na tuuangamize mti na matunda yake;

nasi tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,

ili jina lake lisikumbukwe tena.”

2011:20 Mdo 17:31; Za 7:8-9, 11; 1Sam 2:3; 1Nya 29:17; Za 58:10; Mao 3:60Lakini, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki,

nawe uchunguzaye moyo na akili,

wacha nione ukiwalipiza wao kisasi,

kwa maana kwako nimeweka shauri langu.

2111:21 Yer 12:6; Amo 2:12; Yer 38:4; Ay 21:18; Yer 21:7; 34:20; Isa 30:10“Kwa hiyo hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’: 2211:22 Isa 9:17; Yer 18:21kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu. Vijana wao waume watakufa kwa upanga, wana wao na binti zao kwa njaa. 2311:23 Lk 19:44; Yer 6:9; 23:12Hawatasaziwa hata mabaki kwao, kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa adhabu yao.’ ”