Yeremia 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yeremia 10:1-25

Mungu Na Sanamu

1Sikieni lile ambalo Bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli. 210:2 Kut 23:24; Law 20:23; Mwa 1:14Hili ndilo asemalo Bwana:

“Usijifunze njia za mataifa

wala usitishwe na ishara katika anga,

ingawa mataifa yanatishwa nazo.

310:3 Isa 40:19; Kum 9:21; Eze 7:20; Yer 44:8; 1Fal 8:36Kwa maana desturi za mataifa hazina maana,

wanakata mti msituni,

na fundi anauchonga kwa patasi.

410:4 1Sam 5:3; Isa 41:7; Za 135:15; Hos 13:2; Hab 2:19Wanaparemba kwa fedha na dhahabu,

wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike.

510:5 1Fal 18:26; 1Kor 12:2; Isa 45:20; Hab 2:19; Isa 44:9-20; Mdo 19:26Sanamu zao ni kama sanamu

iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege

nazo haziwezi kuongea;

sharti zibebwe

sababu haziwezi kutembea.

Usiziogope; haziwezi kudhuru,

wala kutenda lolote jema.”

610:6 2Sam 7:22; Kut 8:9-10; Za 48:1Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana;

wewe ni mkuu,

jina lako ni lenye nguvu katika uweza.

710:7 Isa 12:4; Ufu 15:4; Za 22:28; Yer 5:22Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe,

Ee Mfalme wa mataifa?

Hii ni stahili yako.

Miongoni mwa watu wote wenye hekima

katika mataifa na katika falme zao zote,

hakuna aliye kama wewe.

810:8 Isa 40:19; Yer 4:22; Isa 44:18; Kum 32:21Wote hawana akili, tena ni wapumbavu,

wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote.

910:9 Dan 10:5; Za 115:4; Isa 40:19; Mwa 10:4Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi

na dhahabu kutoka Ufazi.

Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza

huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani:

vyote vikiwa vimetengenezwa

na mafundi stadi.

1010:10 1Tim 6:17; Za 76:7; Yos 3:10; Mt 16:16; Mwa 21:33; Dan 6:26; Amu 5:4; Ay 9:6Lakini Bwana ni Mungu wa kweli,

yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele.

Anapokasirika, dunia hutetemeka,

mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.

1110:11 Za 96:5; Isa 2:18“Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia kutoka dunia na kutoka chini ya mbingu.’ ”

1210:12 Ay 9:9; 38:4; Isa 40:22-28; Mdo 14:15; 1Sam 2:8; Mwa 1:1, 8, 31Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake,

akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake,

na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.

1310:13 Ay 36:29; Za 135:7; 104:13; Kum 28:12Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma;

huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia.

Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua,

naye huuleta upepo kutoka ghala zake.

14Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa,

kila sonara ameaibishwa na sanamu zake.

Vinyago vyake ni vya udanganyifu,

havina pumzi ndani yavyo.

1510:15 Isa 41:21; Yer 14; 22Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha tu,

hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia.

1610:16 Kum 32:9; Yer 32:17; Kut 34:9; Za 73:26; Yer 31:35; Za 74:2Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo,

kwani ndiye Muumba wa vitu vyote,

pamoja na Israeli, kabila la urithi wake:

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

Maangamizi Yajayo

1710:17 Eze 12:12Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii,

enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi.

1810:18 1Sam 25:29; Isa 22:17; Eze 6:10; Kum 28:52Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu

wote waishio katika nchi hii;

nitawataabisha

ili waweze kutekwa.”

1910:19 Mik 7:9; Nah 3:19; Ay 34:6; Yer 14:17; 15:18; Mao 2:13; Yer 30:12, 15Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu!

Jeraha langu ni kubwa!

Lakini nilisema,

“Kweli hii ni adhabu yangu,

nami sharti niistahimili.”

2010:20 Yer 4:20; 31:15; Mao 1:5Hema langu limeangamizwa;

kamba zake zote zimekatwa.

Wana wangu wametekwa na hawapo tena;

hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu

wala wa kusimamisha kibanda changu.

2110:21 Yer 23:2; Eze 34:6; Yer 6:22; 25:34; 50:6; Isa 56:10; Yer 22:30Wachungaji hawana akili

wala hawamuulizi Bwana,

hivyo hawastawi

na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.

2210:22 Isa 34:13; Yer 9:11; 6:22; 27:6; Eze 12:19Sikilizeni! Taarifa inakuja:

ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini!

Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa,

makao ya mbweha.

Maombi Ya Yeremia

2310:23 Ay 33:29; Yer 9:11; 6:22; 27:6; Eze 12:19Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe;

hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.

2410:24 Yer 7:20; 18:23; 46:28; 30:11Unirudi, Ee Bwana, lakini kwa kipimo cha haki:

si katika hasira yako,

usije ukaniangamiza.

2510:25 Ay 15:21; Yer 8:16; Za 69:24; 79:6-7; Sef 3:8; Yer 2:3Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa

wasiokujua wewe,

juu ya mataifa wasioliitia jina lako.

Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo;

wamemwangamiza kabisa

na kuiharibu nchi yake.