Jinyenyekezeni Kwa Mungu
14:1 Tit 3:9; Rum 7:23Ni kitu gani kinachosababisha mapigano na ugomvi miongoni mwenu? Je, haya hayatokani na tamaa zenu zinazoshindana ndani yenu? 24:2 Mt 5:21, 22; Yak 5:6; 1Yn 3:15Mnatamani lakini hampati, kwa hiyo mwaua. Mwatamani kupata lakini hampati vile mnavyotaka, kwa hiyo mnajitia katika magomvi na mapigano. Mmepungukiwa kwa sababu hammwombi Mungu. 34:3 Mt 7:7; Za 66:18; 1Yn 5:14Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu.
44:4 Yak 1:27; Rum 8:7; Yn 15:19Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu. 54:5 1Kor 6:19; Mwa 6:5; 8:21; Hes 11:29; Mit 21:10Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 64:6 Za 138:6; Mt 23:12Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema:
“Mungu huwapinga wenye kiburi,
lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
74:7 Efe 6:11; 1Pet 5:6-9Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 84:8 Ebr 7:19; Isa 1:16; Za 119:113Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 94:9 Lk 6:25; Mt 5:4Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. 104:10 Ay 22:29; Mt 23:12; Lk 14:11; 1Pet 5:6Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
Onyo Kuhusu Kuhukumu Wengine
114:11 Rum 1:30; 2Kor 12:20; Mt 7:1; Yak 1:22Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria. 124:12 Mt 10:28; 7:1Yuko Mtoa sheria mmoja tu na yeye peke yake ndiye Hakimu, ndiye awezaye kuokoa au kuangamiza. Lakini wewe ni nani hata umhukumu jirani yako?
Kujivuna Kwa Ajili Ya Kesho
134:13 Lk 12:18-20Basi sikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.” 144:14 Za 39:5; Isa 2:22Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 154:15 Mdo 18:21Badala yake, inawapasa kusema, “Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.” 164:16 1Kor 5:6Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni uovu. 174:17 Lk 12:47; Yn 9:41Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.